Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,491
- 2,355
Katika taarifa ya habari iliyosomwa jana usiku saa mbili na kurudiwa leo asubuhi ITV imeripoti kuwa hata nyumba ambazo zilikuwa maeneo ya juu ambazo hazijawahi kukumbwa na mafuriko nazo zimebomolewa.
Taarifa hii wameipata kwa kuwahoji waathirika pekee bila kuwahoji wasimamizi wa ubomoaji kama zina ukweli wowote au ni malalamishi yasiyo na msingi.
Kwa mtazamo wangu nadhani walipaswa kuwahoji na wasimamizi wa bomoabomoa ili kupata habari iliyokamilika vizuri.
ITV kurusha taarifa kama hii kwa upande wangu naona kama ni kudhoofisha bomoa bomoa inayoendelea kwa kuwa itaonekana kama ni zoezi ambalo halikufanyiwa utafiti wa kina kujua ni nyumba zipi zinapaswa kubomolewa hivyo kuonekana kama serikali ilikurupuka na inachofanya ni uonevu kwa baadhi ya watu.
Naomba kuwasilisha.

Last edited by a moderator: