ITV wanadhoofisha bomoabomoa ya Magufuli?

ITV wanadhoofisha bomoabomoa ya Magufuli?

Katika taarifa ya habari iliyosomwa jana usiku saa mbili na kurudiwa leo asubuhi ITV imeripoti kuwa hata nyumba ambazo zilikuwa maeneo ya juu ambazo hazijawahi kukumbwa na mafuriko nazo zimebomolewa.

Taarifa hii wameipata kwa kuwahoji waathirika pekee bila kuwahoji wasimamizi wa ubomoaji kama zina ukweli wowote au ni malalamishi yasiyo na msingi.

Kwa mtazamo wangu nadhani walipaswa kuwahoji na wasimamizi wa bomoabomoa ili kupata habari iliyokamilika vizuri.

ITV kurusha taarifa kama hii kwa upande wangu naona kama ni kudhoofisha bomoa bomoa inayoendelea kwa kuwa itaonekana kama ni zoezi ambalo halikufanyiwa utafiti wa kina kujua ni nyumba zipi zinapaswa kubomolewa hivyo kuonekana kama serikali ilikurupuka na inachofanya ni uonevu kwa baadhi ya watu.

Naomba kuwasilisha.
Ni kama wanakauchonganishi flan kati ya wananchi na serikali yao
 
Ishu sio ilio mabondeni tu..sheria inasema ujenzi wa makazi haurusiwa eneo ndani ya mita60 kutoka mto au chazo cha maji..so ata km nyumba ipo juu mafurko hayafki lkn km ipo ndani ya mita60 hakuna namna itavunjwa tu
 
'' ITV imeripoti kuwa hata nyumba ambazo zilikuwa maeneo ya juu ambazo hazijawahi kukumbwa na mafuriko nazo zimebomolewa.''
Ukiwa ndani ya mita sitini tu inatosha Nemc kukuamuru utoke eneo husika. Si unajua waandishi wetu na elimu zao za ''hapa na pale'' Kubenea-style.
 
Hapa kazi imekuwa haps kilio tu, ila serikali ina nia ya dhati kuokoa maisha yenu maana kipindi cha mafuriko tunapoteza nguvu kazi kubwa kutokana na mauti yanayoikumba jamii ya mabondeni na pia huwa mnatia hiruma sana sasa sijui kwa nini hamtaki kuondoka mnaleta lawama mwingine ataniuliza tutaenda wapi na mimi namwambia nenda ulikotoka. Serikali haitavumilia tena kwenda kuopoa maiti kwenye maji tena na kutuchafulia mabonde ambayo ndio njia kuu ya maji kipindi cha mvua nyingi.
Asante sana Muumba was mbingu akuzidishie utajiri ulio nona na sisi wa mabondeni aturudishe mavumbini tuliko toka Amina
 
Mtu anaishi mkwajuni anafanya kazi ya kuuza vitu vidogo vidogo Posta...mtoto wake anasoma magomeni we unampeleka Mabwepande alafu unamuwekea nauli ya magari 1400.

Usipotoshe. Nauli inapitiwa upya.

Hivi zinakutosha? Kwahiyo anayechuuza karibu na hispitali, anatakiwa apewe chuba hapo hospitali ili tu haki izingatiwe?

Duuuh!!
 
Hivi kwa akili yako unadhani ITV wataonesha mema ya Serikali ya Magufuli? Unamjua mmiliki wa ITV? Ni nani na anatoka wapi?

Hivi Magufuli nae anapenda tabia kama za yule aliyemaliza? Maana naona wengine hambadilishi mienendo, kama vile kujipendekeza au ccm ni ile ileeee
 
Binafsi naona hawatendi haki hata kidogo kwasababu sehem zingine wanazobomoa ni zaidi ya mita60 utakuta sehem labda mita150 na zaidi lakini bado wanabomoa wanatakiwa watende haki kabla ya kubomoa wanatakiwa wapime wajue hii sehem sahihi au hapana hao wanabomoa bomoa sio haki kabisa wanawaonea wananchi wengine
 
Nyumba ya Machache kule msese nayo imetiwa x
 
Hivi kwa akili yako unadhani ITV wataonesha mema ya Serikali ya Magufuli? Unamjua mmiliki wa ITV? Ni nani na anatoka wapi?
Mkuu kwa hili tusipende kushangilia walisema wataboboa nyumba zilizomo ndani ya mita60 kutoka kwenye kingo za mito sasa kwa jinsi ulivyofuatilia hivyo ndivyo wanavyofanya au kwa sababu magufuli anashangiliwa kuna wengine wanatumia nafasi hiyo kumfitinisha na wananchi?
 
nyie mnafuraia watu kubomolewa bila kuelekezwa pakwenda, watakao faidi ni wenyenyumba wapangaji wajiandae kodi kupaa tz
 
Katika taarifa ya habari iliyosomwa jana usiku saa mbili na kurudiwa leo asubuhi ITV imeripoti kuwa hata nyumba ambazo zilikuwa maeneo ya juu ambazo hazijawahi kukumbwa na mafuriko nazo zimebomolewa.

Taarifa hii wameipata kwa kuwahoji waathirika pekee bila kuwahoji wasimamizi wa ubomoaji kama zina ukweli wowote au ni malalamishi yasiyo na msingi.

Kwa mtazamo wangu nadhani walipaswa kuwahoji na wasimamizi wa bomoabomoa ili kupata habari iliyokamilika vizuri.

ITV kurusha taarifa kama hii kwa upande wangu naona kama ni kudhoofisha bomoa bomoa inayoendelea kwa kuwa itaonekana kama ni zoezi ambalo halikufanyiwa utafiti wa kina kujua ni nyumba zipi zinapaswa kubomolewa hivyo kuonekana kama serikali ilikurupuka na inachofanya ni uonevu kwa baadhi ya watu.

Naomba kuwasilisha.
How!
 
Back
Top Bottom