ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

vipi wale jamaa wa mabaga fresh wanajidhalilisha bila kujua?? na wale wanaochukuliwa kucheza shoo .acheni dharau .mengi kaweza na wewe jaribu acha wivu na fikra hasi.


Eti wivu,kumsaidia mtu ndio mpaka uonyeshe kwenye TV?kwani wasingeonesha wangekuwa hawajawafanyia hiyo party?Kwani kuna ajabu gani wao kufurahi mpaka uwaoneshe kwenye TV.
Halafu kama mtu umemualika mtu nyumbani kwako kuna haja gani wengine kuona??
 
Mbona BARESA anawasaidia kila ijumaa pale kwnye msikiti wake k/koo sijawahi kuona akiwatangaza alowasaidia kwnye tv!!
POPOBAWA.
 
Hivi Prince Charles anasikia kunyanyapaliwa au kutengwa na jamii??

Nini maana ya kumualika mtu kwa kusema unamuonyesha ukarimu ili asijisikie ametengwa halafu unamuonesha kwa kadamnasi jinsi ulivyomuhudumia?
Kwani wangesema tu walikula na kunywa na walemavu isingetosha?
Wanamuonyesha nani wakati wale walikuwa wageni wao?
Kumkarimu mtu mpaka uonyeshe kwenye tv??

Mbona hujibu hoja? Iweje mlemavu kuoneshwa anakula anakunywa iwe kudhalilishwa lakini Prince Charles akioneshwa na TBC akila na kunywa isiwe udhalilishwaji?
 
Eti wivu,kumsaidia mtu ndio mpaka uonyeshe kwenye TV?kwani wasingeonesha wangekuwa hawajawafanyia hiyo party?Kwani kuna ajabu gani wao kufurahi mpaka uwaoneshe kwenye TV.
Halafu kama mtu umemualika mtu nyumbani kwako kuna haja gani wengine kuona??

Wewe una lako jambo! Mbona madaktari wanawake wanapotoa msaada wa matibabu ya bure ya kansa ya matiti kwa wanawake na kuoneshwa footage zake ktk TV hupingi?
 
Mkuu Kiziza, tulio kuelewa tumekuelewa!.

Mimi nakuunga mkono kiasi fulani na kiasi fulani nakubaliana na ITV isipokuwa baadhi ya maeneo.
1. Kwanza kitendo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Mengi kuwafanyia tafrija jamii ya watu wenye ulemavu ni jambo jema, la kupongezwa na kuungwa mkono na kina mwenye mapenzi mema kwa sababu lengo ni kuwaonyesha hao wenye ulemavu jinsi unavyo wathamini. Big up Mengi for that!.
2. Kitendo cha kuionyesha hafla hiyo kwenye news kama tukio jingine lolote pia its right.
3. Kitendo cha kuandaa kipindi maalum kuhusu hafla hiyo kwa lengo la kuhamasisha wengine pia wawajali wenye ulemavu its a good move as well sambamba na kuonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo walemavu.
4. Kitendo cha kusaidia wenye ulemavu na kuwafanyia tafrija ili kuonyesha watu waone jinsi unavyosaidia, hiyo ni show off na ni wrong!. Kuna watu kibao wanaosaidia bila kufanya show off!.
5. Kitendo cha kuwaalika wenye ulemavu halafu kuwarekodi tena with close-up ili kuonyesha wenye ulemavu wanakula vipi au ili kuonyesha umma wenzetu wenye ulemavu wa viungo wanacheza vipi muziki licha ya mapungufu yao, huu kwa kweli ni kuingilia right to privacy ya wenye ulemavu na kuonye prolonged shots na close-ups za maumbile yao wakila au wakicheza, huku ni kuwadhalilisha!.
6. Kwa vile the deviding line betwen publicity ya kusaidia ili uonekane unasaidia (show off) na kuonyesha ili kuhamasisha wengine wasaidie is very thin, na kwa sababu Mzee Mengi kusaidia wenye ulemavu haajaanza leo nawaombeni tuendelee kumuaminia anasaidia in good faith na sio for show off, ila hao wanaofanya hiyo huo udhalilishaji sio yeye as Mengi bali watendaji wa vyombo vyake vya habari!.
7. Hafla hiyo bado ingeweza kurekodiwa kipindi maalum bila ya udhalilishaji wa watu wenye ulemavu kwa production team kuwa a bit considarate warekodi nini na kuonyesha
nini na kwa muda gani. Kitendo cha
kiyaonyesha maungo ya wenye ulemavu for
too long sio kuwapublicise bali
kuwadhalilisha!.



Mkuu naona umeelewa ninachomaanisha.
Hasa hiyo namba saba mimi nashindwa kuelewa,inakuwaje mtu amekaa anakula unakuja kumuonyesha kwenye tv,wakati wewe ndio uliomualika sasa unamuonyesha nani?

Watu wengi wanashindwa kuona tatizo lilipo kwa mapenzi yao juu ya Mengi.

Wao wameamua kujumuika nao kwa nia ya kuwaonyesha upendo,sasa kama huyo muhusika umeshamkarimu kuna haja gani kuonyesha ulimwengu mzima.

Mbona wapo watu wengi wanasaidia watu bila kujitangaza?
Mf Regia alikuwa anamsaidia mwanamke mlemavu anayeishi bukoba akamfungulia account kila mwezi alikuwa anamuwekea fedha sh 100,000 si ndugu yake ila ni kwa upendo wake tu lakini ni nani aliyekuwa anajua?hiyo ndio maana ya kutoa na kusaidia
kwamba atakushukuru mwenyewe muhusika
huna haja ya kuonyesha uma kwa details tena kwenye tv zote mbili
 
Kwa mtazamo wangu

nana sawa tu hawa wenzetu pia wanajiskia faraja
na wao kujiona kwenye tv wakiburudika

mbona kwenye makoktail pati watu hamnangi
kwani inawapunguzia nini wakionyeshwa

chuki binafsii makazini,
majumbani na mitaani ,
mpaka ni kero inaweza kuzua tafarani!!!!!!!
 
Ume2mwa na Manji? Wewe umewah kuwasaidia walemavu?

jadili hoja iliyopo mezani.
Kuanza kushambulia mtu ni dalili ya kukosa cha kuchangia.
You'd better shut up your big stinky mouth.
Sawasawa?
 
Kwa mtazamo wangu

nana sawa tu hawa wenzetu pia wanajiskia faraja
na wao kujiona kwenye tv wakiburudika


mbona kwenye makoktail pati watu hamnangi
kwani inawapunguzia nini wakionyeshwa

chuki binafsii makazini,
majumbani na mitaani ,
mpaka ni kero inaweza kuzua tafarani!!!!!!!

Kwanza kunanga sijui maana yake nini.

Na hiyo chuki binafsi kwa ITV,kwa wenzetu wenye ulemavu walioalikwa,kwa Mengi mwenyewe au kwa nani!
Na kwa nini kukosoa watu mnaambatanisha na chuki hilo nalo ni tatizo kubwa.

Kumualika mtu au kumpa msaada kuna ulazima gani kutangazia wengine,kwani wangecheza na kula na kufurahi wao na wenyeji wao isingetosha
mpaka wawaonyeshe watu??Nini maana ya kumsaidia mti halafu unaonyesha ulimwengu mzima?
 
Kwani katika kujibu hilo swali kulikuwa na ulazima wa wewe kusema kuwa "ninawasaidia na kuishi nao"?

Hata ITV ukiwauliza kwanini walionesha hafla hiyo ya walemavu watakua na jibu la kuridhisha kama wewe ulivyoweza kujustify hapa kuwa ni kwa sababu uliulizwa na mwanaJF hapa!

Nadhani umeelewa ila hapo unafanya mashindano ya kisecondary na pia unaamini kukosoa ni kumchukia mtu au watu ndio maana hapa wewe unaamini unamprotect
Mengi na ITV kwa ujumla ,ila ungekuwa
unafikiri nje ya hapo lazima ungeona ninachosema.
 
Ni mtazamo wangu naona ni chuki tu
kwani kuna ttzo gani mtu akionyesha alivyofrahi na wenzie
mi nimeona kama ni chuki tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

sasa hiyo chuki binafsi kwa itv,kwa wenzetu wenye ulemavu walioalikwa,kwa mengi mwenyewe au kwa nani!
Na kwa nini kukosoa watu mnaambatanisha na chuki hilo nalo ni tatizo kubwa.
 
Ni mtazamo wangu naona ni chuki tu
kwani kuna ttzo gani mtu akionyesha alivyofrahi na wenzie
mi nimeona kama ni chuki tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Basi na undelee kuona ni chuki.
 
Kila msaada una malengo yake, kwani kabla ya kumlau Mengi na TV zake, unajua orodha ya malengo ya msaada huo? kama hujui ni vema kukaa kimya maana debe tupu lisipopiga kelele huonekana limejaa.

Kama kuna mtu anayo orodha ya uhakika ya malengo ya msaada huo, basi ni Mzee Mengi labda tumwombe hiyo orodha harafu ndo tuweze kujua wapi yuko sawa na wapi kakosea kulinga na malengo yaliyopo.
 
ITV mnapaswa muelewe kama kumkarimu mtu sio lazima utangaze.
Unamwalika mtu halafu unamuanika hadharani akila na kunywa si sawa,kwani msingetuonyesha sisi isingetosha?
 
Mimi nadhani mantiki ipo lakini you can agree to disagree, well

I don't see the logic at all,
He has been trying to seek public sympathy in every thing he is doin or whatever is facing him,sasa kuwaonyesha watu wale ili iweje?

Kuna connection ya Mengi na Matukio yanayompata ikiwa ana Kesi basi atatumia media ku sympathise na public ,kuna kipindi alishawahi kuwapanga maustadh Fulani aonekane nae habagui anachangia jenzi za misikiti na madrasa ili Kuwa dhohofisha wapinZani wake kibiashara....

Hoja ni kua unapoamua kutoa na kulia kushoto kusijue hili ndio funzo, sAsa Kama unadhani kuna alietumwa na Manji wengine hata hatumjui.


Lakini kingine ni kua huyu Mhe Mengi kuna watumishi wake wanalalamika maslahi Yao angeboresha kwanza!

Na pia apunguze kujipendelea air time kwa masuala yanayomhusisha yeye ili kuondoa dhana kua anajaribu kutafuta huruma ya jamii !
 
Nadhani umeelewa ila hapo unafanya mashindano ya kisecondary na pia unaamini kukosoa ni kumchukia mtu au watu ndio maana hapa wewe unaamini unamprotect
Mengi na ITV kwa ujumla ,ila ungekuwa
unafikiri nje ya hapo lazima ungeona ninachosema.

Wivu tu, huna lolote, mbona kipindi hicho pia kimeonesha speech toka kwa watu mbalimbali, yote hayo huyaoni wewe unakomalia msosi tu!
 
Kuna chama cha kutetea walemavu.,.kama mzee MENGI anawadhalilisha walemavu akashtakiwe huko. Kuhusu kutolipa workers nao wana haki ya kwnda media company inayolipa vizuri coz hawajafungwa na misumari hapo ipp!
 
Wivu tu, huna lolote, mbona kipindi hicho pia kimeonesha speech toka kwa watu mbalimbali, yote hayo huyaoni wewe unakomalia msosi tu!

Huenda kwako hicho ni kitu cha kuonea wivu
lakini haiondoi ukweli kwamba unapomkarimu mtu huna haja ya kuonesha kwa ulimwengu wote huo ndio uungwana.
 
Back
Top Bottom