ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiziza, Jan 31, 2012.

 1. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Iwapo thread kama hii imeshakuwepo mtaniwia radhi.

  Hivi kumwalika mtu nyumbani kwako ndio lazima umuonyeshe mbele ya kadamnasi ya watu jinsi anavyokula,anavyokunywa na anavyocheza?
  Mtu unapoamua kutoa tunaambiwa hata mkono wa pili usijue.

  Nimeona jinsi EATV walivyowaonyesha wenzetu wenye ulemavu wakila na kucheza kama vile ni maajabu mtu mwenye ulemavu kucheza na kufurahi leo nimeona tena ITV wakitangazia kipindi maalum kuonesha jinsi
  walivyo waalika wenzetu wenye ulemavu kwa kweli nimeshangaa hivi kumualika mtu kwako mpaka umuwekee kipindi maalum?

  Vyama vya kutetea haki za wenye ulemavu mko wapi?
   
 2. I

  IFRS 9 Senior Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ume2mwa na Manji? Wewe umewah kuwasaidia walemavu?
   
 3. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ha ha washabiki mandazi bwana,nyie ndio mnaopiganaga mitaani kisa eti kati ya mengi na bakhressa nani tajiri...sio kuwasaidia tu ninaishi nao ndio maana nashindwa kuwaelewa hawa ITV.
  Huyu Manji mi namsikia tu tukuulize wewe unayemjua vizuri mpaka kujua kama huwa anatuma watu kuanzisha threads.
  Lakini haibadilishi ukweli ule ni udhalilishaji kwa nchi zilizoendelea itv wangekuwa kwenye matatizo makubwa.
   
 4. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  inahusiana vp na mada????? Changia mada, usilete maswali yasiyokua na uhusiano na mada lengwa
   
 5. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi wanaomlaumu Mengi wote wametumwa na Manji? Kazi ipo!!!
   
 6. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Kweli aisee, mzee mengi anawazalilisha.. Hata mimi hilo limenigusa.
   
 7. I

  IFRS 9 Senior Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  udhalilishaji kula na walemavu chakula? Kucheza nao? Kuwachangia na kuwapa baiskeli? Mafuta ya kuzuia kansa kwa albino? Think and stop acting like a fool!
   
 8. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  think ur the one whos been acting like a fool so far.... ila threads ziko nyingi sio lazima uchangie hii.
   
 9. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nadhani ilikuwa inatosha tu kuonyesha na kusema Mengi alikula chakula pamoja na walemavu na amewasaidia hiki na kile ila kutuonyesha kiiiila kitu haipendezi.
   
 10. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndio hata mi ninavyofikiri,wangeweza kuonyesha kifupi tu labda kwenye habari,lakini sio Eatv one
  hour,kisha Itv one hour tena kipindi maalum halafu bado wanaonesha na marudio tena si sawa.
   
 11. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  sioni tatizo katika hilo! ingekuwa poa kama kila mtu angewajali walemavu kama mengi at least mara moja kwa mwaka,wangejiona na wao ni part ya jamii!!!
   
 12. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu kumjali mtu mwenye ulemavu ni jambo
  ambalo kila mwanadamu anapaswa na sina shida na hilo,lakini kuna maana gani kumjali halafu kumdhalilisha.

  Muheshimiwa uliyemtaja hapo juu hatujui huenda hausiki moja kwa moja na maamuzi kama hayo ndio maana nikasema Itv nikijua kuna uongozi na watu wanaofanya maamuzi ya moja kwa moja.

  Mfano mtu anapokuwa anakula ule ni wakati wake wa privacy,kwa nini umuonyeshe kwenye Tv tena unamvuta kwenye screen,wakati chakula umemuandalia wewe mwenyewe sasa unataka nani aone?wakati wale walikuwa ni wageni wako wewe?

  Hapo kuna tofauti gani na kampuni ya simu inapotoa msaada kwa watoto yatima na kuita waandishi wa habari??
   
 13. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu haipendezi!! mimi mwenye kuna ndugu yangu flani alinipa msaada kwa kunikopesha fedha hlf akanitangaza mtaa mzima eti amenikopesha!! nimemmind mpk leo siongei nae ..........anayofanya mengi ni udhalilishaji.
  POPOBAWA.
   
 14. m

  mkatakona Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hatukatai kuwajali sasa maonyesho yote yale ya nini? Hv unazijua haki za walemavu linapokuja suala la kuwaripoti? Sheria zipo ila sema nchi yetu ukiwa na pesa basi hata akikusaidia kisha akakudhalilisha bado utalazimika kumlamba miguu!!! Penye ukweli muwe mnatafakari angalau sio kutukuza tu just b'coz ni mengi kawasaidia!!
   
 15. E

  ENGINE CONTROL Senior Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna yule kilema ambaye alikuwa hana mikono na miguu alicheza mziki mpaka anaruka na sarakasi.
  Ukifikiria kwa haraka haraka tena kwa akiri ya kimasikini hauta fikilia kama ule ni uzalilishaji.
  Aliye wapa ule msaada huwa anautumia umasikini wa walemavu kama kigezo cha kujisafishia jina.
  Kwanza mi huwa namuona ni mnafiki tu .

  TENDA WEMA NENDA ZAKO
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  we umekuja lini Tanzania? Mbona mwaka jana na mwaka juzi hukubandika mada yako hapa wakati kila mwaka hili tukio lipo? Huu unafiki
   
 17. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata hiyo mwaka jana na juzi niliona hii si sawa,na kuhusi kubandika hapa inamaana wewe ulikuwa member wa jf tangu ulipozaliwa??kama sivyo huwezi kushangaa kwa nini mwaka jana na juzi sikubandika..
   
 18. q

  qsndebile Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3  Comment yangu

  Mimi nadhani hisia zako ndio zinakufanya uone kama unadhalilishwa, kwani hakuwaalika ili kuwasaidia bali nijuavyo mimi huwa anafanya kama "Walemavi Day" kwa hiyo ni sawa kuwaonesha na kuweka kipindi maalum kwa sababu siyo kipindi rasim ITV ndio maana kinaitwa hivyo. Na lengo ni kuionesha jamii namna walemavu wanavyoweza kufanya mambo mbalimbali ya kiubunifu katika jamii, tungejuaje vikundi vya ngoma, muziki na vingine kama wasingeoneshwa?

  Pia sherehe kama sherehe ikifanywa na jumuia yoyote ya watu si mbaya kuoneshwa kwa vyombo vya habari, mfano makampuni ya Company's Day kwa kila mwaka mbona huonesha kwenye vyombo vya habari jinsi walivyosherekea?
  Mtoa maada inavyooneshwa umeathiriwa na MILA YA KUWAFICHA WALEMAVU ambayo waafrica wengi imetupotosha hata kushindwa kutembea nao na kuwaficha majumbani wasiende shule.

  Kipindi maalumu kinatuwezesha tuwaone wanavyoweza kuonesha vipaji vyao, ubunifu wao, na kutoa nafasi kwa wengine kuona kumbe ulemavu mwingine si lazima uwe ombaomba, unaweza kucheza kwenye mkusanyiko wa watu na watu wakakutuza na hiyo ikawa ajira yako kama baadhi ya walemavu wa macho pale Dodoma wafanyavyo stand na kwenye train badala ya kuombaomba


  Ushauri,
  Nadhani ni vyema mtoa mada ujikomboa kutoka kwenye Dhana ya kuwaficha walemavu kwa kuona kuwa wakionesha uwezo wao kutokana na ulemavu wao wataonekana wanajidhalilisha. Pili uwe mstari wa mbele kuwafanya walemavu waoneshe kwa umma / watu ni nini wanaweza kufanya ili watumie vipaji vyao kujipatia kipato kama wale wacheza mziki wa TOT

   
 19. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  naamini hakuna ubaya sana maadam ameshatumia jina HAFLA ina maana sherehe sasa sherehe ni vyema watu wale wanye wacheze ... ingekuwa kawaalika nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha usiku then awaonyeshe hivyo nisingekubaliana na hilo
   
 20. u

  utantambua JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe umeamua kuitafsiri kwa mtazamo hasi, huenda lengo ni kuwachochea wengine wenye uwezo na nafasi ya kuwakarimu walemavu kufanya hivyo. Hakuna ubaya wowote hapa.
   
Loading...