ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

Hivi kumbe kumuona mlemavu akila na kucheza ni vibaya? Kwani mlemavu si mtu,je twatakiwa tufiche wafanyayo?
 
Kuonyesha walemavu wanafanyiwa tafrija ni fundisho kwa jamii kwamba walemavu wanahitaji kusaidiwa. Namshukuru Bw Mengi kwani anafanya kile Mwenyezi Mungu anapenda tufanye yaani tusaidie wanaohitaji misaada. Tusikatishe tamaa watu wa aina hii. Huenda hata huyo Bakresa unayemtaja alipata ushawishi kusaidia maskini baada kuhamasishwa na alichoona kwenye vyombo vya habari kama TV.
 
Hivi kumbe kumuona mlemavu akila na kucheza ni vibaya? Kwani mlemavu si mtu,je twatakiwa tufiche wafanyayo?

Issue sio kumuona mlemavu lakini nini maana ya kumkaribisha mtu nyumbani kwako kwa nia ya kumuonyesha upendo kisha kuwaonesha watu wengine,kwani yule uliyemualika akiridhika yeye sisi wengine unahitaji tuone ili iweje??hapo kuna tofauti gani na makampuni kwenda kutoa msaada kwa watoto yatima na kuita media waonekane kwenye TV nini maana ya kutoa hapo??
 
Kuonyesha walemavu wanafanyiwa tafrija ni fundisho kwa jamii kwamba walemavu wanahitaji kusaidiwa. Namshukuru Bw Mengi kwani anafanya kile Mwenyezi Mungu anapenda tufanye yaani tusaidie wanaohitaji misaada. Tusikatishe
tamaa watu wa aina hii. Huenda hata huyo
Bakresa unayemtaja alipata ushawishi
kusaidia maskini baada kuhamasishwa na
alichoona kwenye vyombo vya habari kama
TV.

Mimi sikatishi tamaa na nafahamu ni wajibu wa kila mwanadamu.
Ila sikubaliani na aina hii ya utoaji hata kidogo.
Hivi lini ulienda msikitini au kanisani ukaweka sadaka yako juu ili watu waone kiasi unachotoa?hii si kati ya wewe na Mungu wako?
 
Mnanifurahisha sana mengi kuonyesha mi udhalilishaji na ninyi ndo mnalipia pesa nyingi tu kuonyesha harusi zenu tbc, kwa upande wangu nilifurahi sana kuona wenzetu wamefurahi vile.
 
Mnanifurahisha sana mengi kuonyesha mi udhalilishaji na ninyi ndo mnalipia pesa nyingi tu kuonyesha harusi zenu tbc, kwa upande wangu nilifurahi sana kuona wenzetu wamefurahi vile.

Kuonesha harusi Tbc wanafanya biashara ndio maana wanalipa na anayeonyesha harusi yake anajua kabisa ameenda kushow off.

Lakini ile ni ghafla ya wafanyakazi wa ipp wamewafanyia watu wenye ulemavu wamewaalika kwa hiari haikuwa na haja ya kuonyesha kwenye Tv,jamii yetu haijajua nini maana ya kutoa bado.
 
Mkuu naona umeelewa ninachomaanisha.
Hasa hiyo namba saba mimi nashindwa kuelewa,inakuwaje mtu amekaa anakula unakuja kumuonyesha kwenye tv,wakati wewe ndio uliomualika sasa unamuonyesha nani?

Watu wengi wanashindwa kuona tatizo lilipo kwa mapenzi yao juu ya Mengi.

Wao wameamua kujumuika nao kwa nia ya kuwaonyesha upendo,sasa kama huyo muhusika umeshamkarimu kuna haja gani kuonyesha ulimwengu mzima.

Mbona wapo watu wengi wanasaidia watu bila kujitangaza?
Mf Regia alikuwa anamsaidia mwanamke mlemavu anayeishi bukoba akamfungulia account kila mwezi alikuwa anamuwekea fedha sh 100,000 si ndugu yake ila ni kwa upendo wake tu lakini ni nani aliyekuwa anajua?hiyo ndio maana ya kutoa na kusaidia
kwamba atakushukuru mwenyewe muhusika
huna haja ya kuonyesha uma kwa details tena kwenye tv zote mbili
Mkuu Kiziza, niliangalia kipindi cha eatv na kile cha jana cha ITV kuna tofauti kubwa, kile cha eatv ndicho kilichokuwa na udhalilishaji ila hiki cha ITV kilikuwa very profesional save for clips mbili tatu ambazo ni za udhalilishaji.

Kipindi cha jana kilijikita katika dhana mzima ya shughuli hiyo na concentration ilikuwa ni kwenye matukio bila kuonyesha sana maumbile ya wenye ulemavu wanakulaje au wanachezaje.

Kusema ukweli kuna contrast kubwa kati ya itv production na ile ya eatv. Ile itv ndio ile good publicity niliyoizungumza yenye nia njema na ile ya eatv ndio ilikuwa show off!.

Pia nakuomba usimuhusishe Mengi kwenye output kwa sababu naamini sio yeye anayesimamia production.

La mwisho ni kwa Mzee Mengi kuitumia hafla ile kisiasa kuhubiri kuhusu jinsi asivyoridhishwa na kasi ya JK kwenye vita vya ufisadi haswa alivyoshindwa kuwawajibisha mafisadi wa EPA. Japo ujumbe umefika ila it was a wrong audience of all the people wenye ulemavu?!. Ujumbe mzito kama ule alitakowa autoe kwenye zike high profile events wanasiasa, mabalozi na viongozi wa taasisi za umma wapo kama CTI events ndipo akomelee misumari ile, Kuwahubiri wenye ulemavu kuhusu ufisadi wa EPA ni kuwazidishia machungu!.
 
Mnaolinganisha sherehe za kawaida na hizi za Mengi na ndugu zetu hawa mnamis point sana. Kwanza katika jamii ya kiafrika kumpa mtu chakula tena asiyenauwezo kilsha ukatangaza ni kosa kubwa kimaadili. Pia kudai eti anafanya hivo ili na wengine waige mfano nalo si sawa kwani ukimsaidia mtu (tofautisha michango ya Twiga stars) usikomalie na wengine wasaidie.Na istoshe ni jambo lililowazi kuwa Mengi anatafuta popularitry ila kupitia matatizo ya walemavu si sawa. By the way mlo mmoja kwa mlemavu kwa mwaka unamuondoleaje matatizo yake mwaka mzima. FAFAKALI
 
hakuna tatizo, kila mtu anahitaji furaha, sasa kama kuonyesha furaha ya mtu ni tusi, basi mwenzetu umepotea
 
Mkuu Kiziza, niliangalia kipindi cha eatv na kile cha jana cha ITV kuna tofauti kubwa, kile cha eatv ndicho kilichokuwa na udhalilishaji ila hiki cha ITV kilikuwa very profesional save for clips mbili tatu ambazo ni za udhalilishaji.

Kipindi cha jana kilijikita katika dhana mzima ya shughuli hiyo na concentration ilikuwa ni kwenye matukio bila kuonyesha sana maumbile ya wenye ulemavu wanakulaje au wanachezaje.

Kusema ukweli kuna contrast kubwa kati ya itv production na ile ya eatv. Ile itv ndio ile good publicity niliyoizungumza yenye nia njema na ile ya eatv ndio ilikuwa show off!.

Pia nakuomba usimuhusishe Mengi kwenye output kwa sababu naamini sio yeye anayesimamia production.

La mwisho ni kwa Mzee Mengi kuitumia hafla ile kisiasa kuhubiri kuhusu jinsi asivyoridhishwa na kasi ya JK kwenye vita vya ufisadi haswa alivyoshindwa kuwawajibisha mafisadi wa EPA. Japo ujumbe umefika ila it was a wrong audience of all the people wenye ulemavu?!. Ujumbe mzito kama ule alitakowa autoe kwenye zike high profile events wanasiasa, mabalozi na viongozi wa taasisi za umma wapo kama CTI events ndipo akomelee misumari ile, Kuwahubiri wenye ulemavu kuhusu ufisadi wa EPA ni kuwazidishia machungu!.
Kati ya mambo yanayo niboa na huyu mzee ni kutoa toa tu vitamko kuhusu nchi hii. bahati nzuri kwake anapata audience ila watu wangetafakali wangejua ni mnafiki tu anayetumia kisingizio cha kuipenda nchi yake kupambana na wafanyabiashara mahasimu zake. Yaani anatumia kisingizio cha uzalendo kwa maslahi binafsi. kama Mengi anachukia ufisadi mbona ankomaaa na EPA tu. Wizi umejaa tele mbona hasemi? Napenda sana wafanyabiashara style ya Bakhresa mambo makubwa afu kimya. Tungekuwa nao kama kumi hivi nchi yetu ingekuwa mbali sana sio hawa kutwa kujionyesha kwenye Tv.
 
...mleta mada,umekosa mada. Nenda kalale!! Kivipi kumwonyesha mtu kukawa ni kumdhalilisha? Your thread lacks credibility,nenda kasinzie mbele huko!!
 
Ukimsoma Pasco utaelewa Kiziza...

Nakushauri pia usipende kuwa conclusive.. Eti watu wanampenda tu Mengi..

Mimi sikuangalia hicho kipindi.. Ila nadhani ni suala la watu wenye profession hiyo ndiyo wanaojua picha gani sahihi ili zisilete maana tofauti na ile iliyokusudiwa..
Hujawahi kuona picha nyingine watazamaji wanaombwa radhi..? Vitu kama hivyo..
 
Naichukia hii thread sababu imekaa kimbeambea, kimajungumajungu na kinafkinafki. Kwani hao walemavu waliitwa? Na kama unaona mzee Mengi kawadhalilisha mwakani fanya pati wewe uwaite?.
Najua watu kama wewe hamkosekanagi ila ni aibu sana kiutumika na mdosi kumchafua Mtanganyika mwenzio. Kweli njaa mbaya!.
 
Hehehe!! Kuna watu mnachekesha humu ndani!!
 
...mleta mada,umekosa mada. Nenda kalale!! Kivipi kumwonyesha mtu kukawa ni kumdhalilisha? Your thread lacks credibility,nenda kasinzie mbele huko!!

Na wewe ni kwa nini umechangia nikikwambia na wewe umekosa la kufanya..nitakuwa nimekosea??
 
mbona waliopeleka misaada kwa wahanga wa mafuriko hukuwasema kwani wanaenda kuuza sura kwenye ma Tv ya bongo. Mengi siku zote ni mtu wa kutaka sifa.
 
Mkuu Kiziza, nadhani ulieleweka tangu mwanzo concern zako ni valid, ila usielekeze mashambulishi kwa Mzee wetu, ni wale vija wake wa EATV ndio waliharibu, ukizidi kukomalia, itakuja kuonekana ni chuki binafsi maana humu jf, ma haters na ma hate preachers wametamalaki sana, usije kuongeza idadi yao!.
 
Mkuu mimi sijamlaumu Mengi hata mahali pamoja na ndio maana nimesema ITV nikijua kuna uongozi na kuna wanaofanya maamuzi ys moja kwa moja ingekuwa Mengi ningetaja moja kwa moja Mengi,ila watu wameng'ang'ania
mara sijui wivu kwa Mengi mara nimetumwa na Manji vitu vya ajabu kabisa.

Watu wengi tunadhani kukosoa ni kuchukia,binafsi kwangu Itv ndio Tv yangu ya kwanza na bila kuangalia habari Itv naona bado sija angalia habari,lakini haya ndio maoni yangu juu ya swala hili hivyo kusema ni haki pia.
 
Nadhani ilikuwa inatosha tu kuonyesha na kusema Mengi alikula chakula pamoja na walemavu na amewasaidia hiki na kile ila kutuonyesha kiiiila kitu haipendezi.

Tena hiyo ishu sio news tena ya kufanya mpaka ipewe airtime ya kipindi maalum inatakiwa wa edit na ku make it KISS
 
Back
Top Bottom