ITV na isidingo the need???

ITV na isidingo the need???

Hapa Papa G pale slu.. hapa Baka hends pale matabane... and Mrs matabane.. pale muhindi... sijaichoka. Nawachukia wanapoingiza na ushoga na kuhalalisha.
 
Tamthilia ya tangu mwaka 1995 mpaka sasa zaidi ya miaka 20.kweli kama naangalia ITV ukifika mda wa isidingo huwa nahamia channel nyingine.tumeichokaaaa
 
Hivi jamani kuna kitu sijakielewa hapa kuhusu hii isdingo the need, kwanini huwa haishi?? Ina maana itv wamekosa kipindi kingine cha kuelimisha jamii zaidi ya hiki cha isdingo?? Au kuna percent wanapata kutoka kwa hao isdingo wenyewe???? Isdingo yenyewe haina mashabiki hata kidigo, maisha gani ya ki miner yasiyo na mwisho?? Itv
muache kutuzingua banaaa!!!

toka mwaka 1999 nikiwa primay mpaka leo bado naiona Isidingo.
 
Letti Matabane alifariki ki tamthilia kitambo lakini hivi karibuni amefariki ki ukweli kwa HIV
 
hahahahaha hivi ilianza mwaka gani
Navokumbuka miss neddy, Isidingo ilianza baada ya tamthiliya nyingine maarufu sana kumalizika
mwaka 1998 iitwayo 'Egoli, place of Gold' iliyopendwa sana ITV.
 
Last edited by a moderator:
Navokumbuka miss neddy, Isidingo ilianza baada ya tamthiliya nyingine maarufu sana kumalizika
mwaka 1998 iitwayo 'Egoli, place of Gold' iliyopendwa sana ITV.

Iliyopendwa na itv??? Au watu waliipenda???
 
Last edited by a moderator:
Ila kiukweli Isidingo inagusa kwenye maswala yapi hasa???? Tushazoea kuangalia series tofauti zenye lengo maalum. Yaweza kuwa ushushu ama waokoaji huru, ama ujambaz wa mtandao ama mapenzi nk. Lakin hawa jamaa siamini kama kuna mtu ambae alianza kufuatilia kipindi kile mpaka leo anafuatilia yani sielewi. Nikiangalia waliokuwepo kule 2001 leo hii siwaoni yani washapotea nadhani wamebaki wa4 hivi.

isidingo ina address different issues tena zenye nafasi kubwa kwenye MAISHA kama sasa kuna issue ya breast cancer..gambling. .drugs na impact zake in real life ....ni tamthilia Nzuri na mafunzo pia. ..
 
Iliyopendwa na itv??? Au watu waliipenda???
Samahani Kifai kama sijaeleweka, ila nilitaka kusema kwamba 'Egoli, the place of gold'
ilipendwa sana na watazamaji wa kituo cha ITV.
 
Last edited by a moderator:
Hivi jamani kuna kitu sijakielewa hapa kuhusu hii isdingo the need, kwanini huwa haishi?? Ina maana itv wamekosa kipindi kingine cha kuelimisha jamii zaidi ya hiki cha isdingo?? Au kuna percent wanapata kutoka kwa hao isdingo wenyewe???? Isdingo yenyewe haina mashabiki hata kidigo, maisha gani ya ki miner yasiyo na mwisho?? Itv
muache kutuzingua banaaa!!!

Mkuu maisha huwa yanakuwa na mwisho? Watu ndio wana mwisho lakini maisha huwa yanaendelea na ndio maana kwenye Isidingo watu wanabadilika. Soap Opera nyingi huchukua muda mrefu sana kuonyeshawa kwa sababu zinasimulia maisha ya jumla ya mahali fulani na sio kisa fulani specifically. Days of Our Lives ambayo hapa kwetu iliwahi kuonyeshwa na Channel 10 kama sikosei, ilianza kuonyeshwa mwaka 1965 na mpaka leo bado inaonyeshwa.

Mimi mwenyewe niliifuatilia nikachoka lakini siwezi kulalamika kwa nini wanaendelea kuonyesha, inaonekana kuna watu wengi bado wanaipenda.
 
Alijisemea binti yangu, hii isidingo nimezaliwa nimeikuta hadi saa hizi niko darasa la sita, haiishi tu!

Hivi jamani kuna kitu sijakielewa hapa kuhusu hii isdingo the need, kwanini huwa haishi?? Ina maana itv wamekosa kipindi kingine cha kuelimisha jamii zaidi ya hiki cha isdingo?? Au kuna percent wanapata kutoka kwa hao isdingo wenyewe???? Isdingo yenyewe haina mashabiki hata kidigo, maisha gani ya ki miner yasiyo na mwisho?? Itv
muache kutuzingua banaaa!!!
 
Isidingo nzuri sana. Btw... imenisaidia kuchelewa kwenda baa. Lincoln na Baker nawakubali. Lerato ni kifaa hasa cha kiafrika (no offence)! Na walivomweka kwenye kansa inaniumaje?

Kulikua na nyingine Mnet inaitwa Jacob's Cross. Ila sijaiona kitambo.
 
nampenda Lerato anayoumwa cancer nataman hadi kulia........ ni makeke fulan sa hivi kapoa huyooo
 
Isidingo inapendwa sana toka imeanza mwaka 1997 sijaacha kuiangalia mpaka leo. We kama huipendi angalia kipindi cha mapishi hapo ITV ndio kinakufaa wewe....Mbafu
 
Mtoa uzi ni mvivu wa kuchunguza,na anashangaa tu kwa sababu inaoneshwa hapa kwetu,Jaribu kuangalia tv stations za nje utaona tamthilia za THE BOLD AND THE BEAUTIDUL,bado inaoneshwa muda mrefu tu,kuna Passions,Scandal na zingine zisizoisha na ni muda mrefu tu umepita bado hazijaisha,au umezoea Kaole
 
Back
Top Bottom