Exaud Mamuya
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 403
- 243
Katika hali ambayo imenishangaza ni vituo hivi vya habari yaani ITV na Channel 10 kutoonyesha habari za press iliyoitishwa na Chadema makao makuu kuhusiana na sakata la katibu wa Chadema kanda maalumu ya Dar es salaam bwana Henry Kileo pamoja na makamanda wengine wanaoshikiliwa na polisi kwa wanachodai kummwagia kada wa ccm tindikali. Imenishangaza sana kuona habari hii ikirushwa na kituo cha Star tv peke yake.
Angalizo langu katika vyombo hivi vya habari ni kwamba wajitathmini na kufanya kazi zao kwa uhuru pasipo kukubali mashinikizo ya ccm na vyombo vyake la sivyo tutavisusia kama ilivyo kwa TBC.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums