ITV MWISHO AFRIKA MASHARIKI TU

ITV MWISHO AFRIKA MASHARIKI TU

dafity

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2008
Posts
1,881
Reaction score
2,091
Habari wa JF. Kwanza nawapongeza ITV Tanzania kwa kuweka wawakilishi wao nchi kadhaa za Afrika Mashariki. Kenya-Dennis Musundi, Rwanda-Bryceson Bichu, DRC-Austerie Marivika, siwakumbuki wa Burundi South Sudan na Uganda.

Lakini ITV WAMEGOMA KABISA KUTANGAZA HABARI ZA NCHI ZINGINE NJE YA AFRIKA MASHARIKI. Kamwe hutasikia habari za Ubelgiji, North Korea, Malawi, Argentina nk. Hata kutokee habari inayoshika Dunia wao huenda usiisikie kwao. Kwa mtazamo wangu hii inawapunguzia ubora wao. Nina mashaka na u Super Brand wao huenda ukaingia dosari.

Ushauri wangu kwao: Wabadilike kulingana na wakati na kuona wateja (watazamaji) wana hitaji nini.
Nawasilisha
 
Kumbe bado huwa mnaangalia ITV? Wengine tushahamia Azam TWO kwenye habari na uchambuzi, picha clear, kuwaunganisha watu direct toka sehemu husika, habari ya popote hata Iceland, updates etc

Niliwahi angalia taarifa fulani ya migogoro ya wakulima vs wafugaji Azam, baada ya siku mbili nikiwa kwa jamaa yangu nae alikuwa anaangalia hao tukaona habari ileile nikasema hawafai kabisa
 
Wanakera balaa...juzijuzi hapa ndio walionesha ile ya Las Vegas tena kwa dakika chache...Sijui nini tatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom