ITV mnatia shaka na aibu kwa hili!

Dah kwel kabisa inashangaza kutoa taarfa za upande moja,ili hali taarifa za upande mwingne zkiweka pembeni.Ngoja 2subir pengine kesho wataonesha na vyama vngne.

Za upande mmoja kwani kulikuwa na mashitaka au malalamiko unataka kusikia upande wa pili unasemaje.....je ni lazima ukiandika habari za CDM lazima uandike na za CCM? Ulalamishi mwingine hauna miguu wala kichwa
 
Ndugu wanabodi,taarifa ya habari jioni hii,kupitia ITV tunaoneshwa taarifa ya habari.habari kuu ni tukio la mwigulu akihutubia wakazi wa karatu katika mkutano wa hadhara akiwanadi wagombea wa ccm, katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni wajibu wa media yoyote kutujulisha wananchi matukio muhimu kitaifa na kimataifa.na pia ni haki yetu wananchi kupata habari ambayo ni muhimu kwetu kama raia wa nchi hii.

Tatizo nililoliona leo tofauti badala ya ITV kutujulisha matukio mengine ya kisiasa kutoka vyama vingine kwa sababu ni vema kutupatia habari ambazo ni balanced, kwa sababu vyama vyote nchini viko katika harakati za kampeni. Na vina wafuasi nchini kote pia na hivyo tungependa kujuzwa sanjari na ccm.

Sasa leo ITV wametumia takriban dakika tano kwa habari ya mwigulu na kichekesho ni pale mtangazaji alipotangaza habari nyingine ya taarifa ikihusu tume ya uchaguzi lakini picha ya screen play ikiendelea kuonyesha tukio la mkutano wa mwigulu pale karatu,
Hii ikiendelea hadi mwisho wa taarifa iliyofuata jambo ambalo limeonekana sio makosa ya kiufundi Bali maelekezo rasmi.

My take:
Katika bunge lililomalizika kwa kashfa ya escrow account tulikuwa tunaoneshwa balanced story na hata ITV ikawa inarudia kutuonyesha usiku kwa wale ambao hawakubahatika kuliona mchana na jioni.

Sasa kulikoni ITV inageuka kuwa TBC 3???
Au ile ilikuwa sababu ya ugomvi kati ya mengi na muhongo? Na baada ya hapo mengi anarudi kundini!
Naomba tulijadili kwa kuchangia bila ugomvi
Sasa hiyo "take" yako ndio kitu gani sasa!
 
Back
Top Bottom