ITV mnatia shaka na aibu kwa hili!

ITV mnatia shaka na aibu kwa hili!

Ndugu wanabodi,taarifa ya habari jioni hii,kupitia ITV tunaoneshwa taarifa ya habari.habari kuu ni tukio la mwigulu akihutubia wakazi wa karatu katika mkutano wa hadhara akiwanadi wagombea wa ccm, katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni wajibu wa media yoyote kutujulisha wananchi matukio muhimu kitaifa na kimataifa.na pia ni haki yetu wananchi kupata habari ambayo ni muhimu kwetu kama raia wa nchi hii.

Tatizo nililoliona leo tofauti badala ya ITV kutujulisha matukio mengine ya kisiasa kutoka vyama vingine kwa sababu ni vema kutupatia habari ambazo ni balanced, kwa sababu vyama vyote nchini viko katika harakati za kampeni. Na vina wafuasi nchini kote pia na hivyo tungependa kujuzwa sanjari na ccm.

Sasa leo ITV wametumia takriban dakika tano kwa habari ya mwigulu na kichekesho ni pale mtangazaji alipotangaza habari nyingine ya taarifa ikihusu tume ya uchaguzi lakini picha ya screen play ikiendelea kuonyesha tukio la mkutano wa mwigulu pale karatu,
Hii ikiendelea hadi mwisho wa taarifa iliyofuata jambo ambalo limeonekana sio makosa ya kiufundi Bali maelekezo rasmi.

My take:
Katika bunge lililomalizika kwa kashfa ya escrow account tulikuwa tunaoneshwa balanced story na hata ITV ikawa inarudia kutuonyesha usiku kwa wale ambao hawakubahatika kuliona mchana na jioni.

Sasa kulikoni ITV inageuka kuwa TBC 3???
Au ile ilikuwa sababu ya ugomvi kati ya mengi na muhongo? Na baada ya hapo mengi anarudi kundini!
Naomba tulijadili kwa kuchangia bila ugomvi

Acha addiction wewe au usipoona/sikia habari za chadema huwezi kulala?
 
Habari za Mengi Mwenyewe hupewa Nafasi kubwa sana hata kama anachokizungumzia ni cha kawaida sana,Mbona wamiliki wengine wa Tv na Radio huwa hawajipi nafasi kubwa iwe Tv zao?

mnataka ajibane na huku yeye ndio mwenye mali jmn!!??
 
Nyinyi wengine huwa mnaakili kama kuku. soma hii posti niliyoiandika jana. kama unaakili fupi na husomi unabisha tu nimpumbavu wewe.

We umeshapakuliwa sana umechoooka akili na makalio.
 
Nadhani hivyo vyama vingine havikualika waandishi toka itv, maana waandaishi wanaalikwaga wanapewa na posho ndio habari inatoka....
Mwandishi haendi tu kwenye mkutano, mara nyingi wanakua wamealikwa na maslahi juu
 
Acha addiction wewe au usipoona/sikia habari za chadema huwezi kulala?

Wewe ndio addicted ccm member, maana hata unapoonyeshwa njia sahihi bado una kuwa na" arosto" ya ccm:thumbdown::thumbdown:
 
mnataka ajibane na huku yeye ndio mwenye mali jmn!!??

Acha ujinga wewe. Hivi uliishamjua mkurugenzi wa vituo kama mfano,Chanel ten,au ulishamuona mwenye azam
tv,akiuza sura Kila siku kwenye vituo wanavyomiliki?

Au Kenya ulishamjua mmiliki wa citizen tv,au ntv?
Bila shaka umeelewa maana ya mmiliki biashara yenye maslahi ya umma
 
Acha ujinga wewe. Hivi uliishamjua mkurugenzi wa vituo kama mfano,Chanel ten,au ulishamuona mwenye azam
tv,akiuza sura Kila siku kwenye vituo wanavyomiliki?

Au Kenya ulishamjua mmiliki wa citizen tv,au ntv?
Bila shaka umeelewa maana ya mmiliki biashara yenye maslahi ya umma

Kwani ni sheria au uamuzi wa mtu? Kwikwikwi Bavicha bwana
 
Kwani wale jamaa waliosema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania vinaubaguzi,watu si walibisha na wale jamaa wakaitwa wachochezi.
 
Wewe ndio addicted ccm member, maana hata unapoonyeshwa njia sahihi bado una kuwa na" arosto" ya ccm:thumbdown::thumbdown:

Tanzania kuna chama kimoja tu cha siasa chenye mapungufu mengi wengine wote wanatimiza tu masharti ya world bank. Bahati mbaya sina hata kadi ya chama hicho
 
Back
Top Bottom