ITV mnatia shaka na aibu kwa hili!

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,116
2,000
Ndugu wanabodi,taarifa ya habari jioni hii,kupitia ITV tunaoneshwa taarifa ya habari.habari kuu ni tukio la mwigulu akihutubia wakazi wa karatu katika mkutano wa hadhara akiwanadi wagombea wa ccm, katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni wajibu wa media yoyote kutujulisha wananchi matukio muhimu kitaifa na kimataifa.na pia ni haki yetu wananchi kupata habari ambayo ni muhimu kwetu kama raia wa nchi hii.

Tatizo nililoliona leo tofauti badala ya ITV kutujulisha matukio mengine ya kisiasa kutoka vyama vingine kwa sababu ni vema kutupatia habari ambazo ni balanced, kwa sababu vyama vyote nchini viko katika harakati za kampeni. Na vina wafuasi nchini kote pia na hivyo tungependa kujuzwa sanjari na ccm.

Sasa leo ITV wametumia takriban dakika tano kwa habari ya mwigulu na kichekesho ni pale mtangazaji alipotangaza habari nyingine ya taarifa ikihusu tume ya uchaguzi lakini picha ya screen play ikiendelea kuonyesha tukio la mkutano wa mwigulu pale karatu,
Hii ikiendelea hadi mwisho wa taarifa iliyofuata jambo ambalo limeonekana sio makosa ya kiufundi Bali maelekezo rasmi.

My take:
Katika bunge lililomalizika kwa kashfa ya escrow account tulikuwa tunaoneshwa balanced story na hata ITV ikawa inarudia kutuonyesha usiku kwa wale ambao hawakubahatika kuliona mchana na jioni.

Sasa kulikoni ITV inageuka kuwa TBC 3???
Au ile ilikuwa sababu ya ugomvi kati ya mengi na muhongo? Na baada ya hapo mengi anarudi kundini!
Naomba tulijadili kwa kuchangia bila ugomvi
 
Silvano Sange

New Member
Nov 21, 2014
1
0
Dah kwel kabisa inashangaza kutoa taarfa za upande moja,ili hali taarifa za upande mwingne zkiweka pembeni.Ngoja 2subir pengine kesho wataonesha na vyama vngne.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Tatizo liko wap hapo mkuu?
Tatizo ni pale Mwigulu anaposema eti waliohusika na wizi wa fedha za ESCROW watashughulikiwa kulingana na ukubwa wa kosa lake na eti anashangaa kwa wapinzani kuwataka wananchi wasiwachague wenyeviti kutoka CCM kwa sababu ya ESCROW kwani hao wagombea wanahusika vipi na ESCROW? kauli hiyo imenisikitisha sana hata kama ni kujitetea huo ni upumbavu kwani wizi umefanywa na viongozi wa CCM akiwemo na yule mkubwa wao na wahusika wengine na watumishi ndani ya serikali ya CCM nafikiri Mwigulu amesahau ule msemo wa wahenga kuwa SAMAKI MMOJA AKIOZA UOZA WOTE
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,604
2,000
Ndugu wanabodi,taarifa ya habari jioni hii,kupitia ITV tunaoneshwa taarifa ya habari.habari kuu ni tukio la mwigulu akihutubia wakazi wa karatu katika mkutano wa hadhara akiwanadi wagombea wa ccm, katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni wajibu wa media yoyote kutujulisha wananchi matukio muhimu kitaifa na kimataifa.na pia ni haki yetu wananchi kupata habari ambayo ni muhimu kwetu kama raia wa nchi hii.

Tatizo nililoliona leo tofauti badala ya ITV kutujulisha matukio mengine ya kisiasa kutoka vyama vingine kwa sababu ni vema kutupatia habari ambazo ni balanced, kwa sababu vyama vyote nchini viko katika harakati za kampeni. Na vina wafuasi nchini kote pia na hivyo tungependa kujuzwa sanjari na ccm.

Sasa leo ITV wametumia takriban dakika tano kwa habari ya mwigulu na kichekesho ni pale mtangazaji alipotangaza habari nyingine ya taarifa ikihusu tume ya uchaguzi lakini picha ya screen play ikiendelea kuonyesha tukio la mkutano wa mwigulu pale karatu,
Hii ikiendelea hadi mwisho wa taarifa iliyofuata jambo ambalo limeonekana sio makosa ya kiufundi Bali maelekezo rasmi.

My take:
Katika bunge lililomalizika kwa kashfa ya escrow account tulikuwa tunaoneshwa balanced story na hata ITV ikawa inarudia kutuonyesha usiku kwa wale ambao hawakubahatika kuliona mchana na jioni.

Sasa kulikoni ITV inageuka kuwa TBC 3???
Au ile ilikuwa sababu ya ugomvi kati ya mengi na muhongo? Na baada ya hapo mengi anarudi kundini!
Naomba tulijadili kwa kuchangia bila ugomvi
Kumbe ITV ni maalum kwa chadema tu! siku zote wamekuwa mstari wa mbele kurusha habari za chadema muda mrefu hii leo moja ya Mwigulu imewatoa imani! dah! wachaga bana!
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,604
2,000
Tatizo ni pale Mwigulu anaposema eti waliohusika na wizi wa fedha za ESCROW watashughulikiwa kulingana na ukubwa wa kosa lake na eti anashangaa kwa wapinzani kuwataka wananchi wasiwachague wenyeviti kutoka CCM kwa sababu ya ESCROW kwani hao wagombea wanahusika vipi na ESCROW? kauli hiyo imenisikitisha sana hata kama ni kujitetea huo ni upumbavu kwani wizi umefanywa na viongozi wa CCM akiwemo na yule mkubwa wao na wahusika wengine na watumishi ndani ya serikali ya CCM nafikiri Mwigulu amesahau ule msemo wa wahenga kuwa SAMAKI MMOJA AKIOZA UOZA WOTE
Hebu muwe na hoja za 2015-2020 vision na sio kuitegemea hoja ya escrow kama mtaji wa chadema wakati kamati ya PAC ilisheheni wana ccm mahiri kama Filikunjombe,kigwangala,Lugora ambao ndio wamewabana walaji wale na CAG aliteuliwa na serikali ya ccm ambaye kaibua madudu haya sasa chadema mna sera gani mkiacha kudandia hoja ya escrow kama mtaji!?
 
MTONILIST

Member
Apr 20, 2012
77
70
Jaman mbona tuna ushabiki mbaya hivi. ITV sio ya chama chochote cha siasa na msikariri kwamba lazima waoneshe taarifa ya chama chenu. Hiki ni chombo cha habari siku zote kinatangaza habari zinazoletwa na waandishi wa mikoani ambazo zimeshahaririwa na ambayo bado haitangazwi sasa usilazimishe taarifa ya chama chako itangazwe inawezekana haijaletwa. Jaman humi ndani ni sehemu maalumu kwa wale watu wanaoitwa Great Thinkers sasa tunapojadili jambo tuoneshe ukomavu wetu katika kuchanganua mambo.
 
commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,116
2,000
Suala hapa ni kuhusu ulinganifu wa habari mlingano.kwa sababu suala hili liko nchi nzima na tuna haki ya kujulishwa kwa usawa,maana TBC imekuwa advocate wa mafisadi na kutuacha solemba walipa kodi wanaoiwezesha
Nahisi hata kwa hili labda na ITV wameishapewa maelekezo.... Maana kama tumefikia mahali tunaweka wanajeshi kwenye bvr sintashangaa kwa hili
 
commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,116
2,000
ha ha ha ha waliizoea kama TV maalum ya chadema leo wanashangaa.
Suala sio kuzoea.issue ni balanced storry..na ----- alioongea mwigulu kuhusu,watu wa karatu wasiwalaumu wenyeviti Bali walaumu waliokula escrow.kwa sababu wenyeviti hawafanyi kazi Benji kuu wala tegeta.

Huyu ndio majibu katibu mkuu chama tawala?
 
2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,549
2,000
Mkuu ni kweli kabisa taarifa za habari za ITV kipindi hichi zinatia shaka sana.Mzee Mengi anatutumia kwa manufaa yake..
Sasa amehamia kwenye suala la ardhi nafikiri pia huko ana maslai pia,maana kila siku ni mgogoro wa ardhi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom