ITV majadiliano ni moto kuhusu sukari

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
479
1,253
Wachangiaji malumbano ya hoja kuhusu sakata la sukari ITV ni Moto, wachangiaji wamejitoa mhanga kuchangia , kuna magiant 4 wanaoshikilia uchumi wa sukari na ni matajiri kama wauza unga

Wachangiaji wanashtumu kauli ya Bashe kuhusu sakata la sukari kwa kutoa lugha ya kejeli kwa wananchi kwamba hawawezi kumhoji isipokuwa Rais, Makamo wa Rais, Waziri mkuu na naibu Waziri mkuu

Mchangiaii mwingine anatoa tahadhari kwa jinsi sukari ilivyo hali itakuwa tete kipindi cha kwaresma na Ramadhani na anaongezea kuwa shida ya sukari ni Bodi ya sukari

Wachangiaji wanaona hata teuzi mbalimbali zinasababisha hali kuwa mbaya kwa sababu watu wanateuliwa kwa kufahamiana

Mchangiaji anakiri hata mwananchi wa kawaida akipewa bilioni 20 kuleta sukari nchini, hawezi akaingiza kwa sababu figisu zitaanzia bandarini na TRA

Wachangiaji wanaonesha maeneo mbalimbali bei ya sukari ni kuanzia elfu 5 na kuendelea na wiki ijayo itakuwa imefikia elfu 10 kwa kilo
 
Pongezi kwa dr Janabi kwa kuepusha magonjwa na vifo vya kizembe kwa kuishauri na kuishinikiza Serikali kuongeza bei ya sukari na mafuta ya kula na asiishie hapo nyama iende kilo elfu 30.
Utaua
 
Pongezi kwa dr Janabi kwa kuepusha magonjwa na vifo vya kizembe kwa kuishauri na kuishinikiza Serikali kuongeza bei ya sukari na mafuta ya kula na asiishie hapo nyama iende kilo elfu 30.
Mbadala wa hivyo vitu wameweka nini?
 
Pongezi kwa dr Janabi kwa kuepusha magonjwa na vifo vya kizembe kwa kuishauri na kuishinikiza Serikali kuongeza bei ya sukari na mafuta ya kula na asiishie hapo nyama iende kilo elfu 30.
sigara pia hamna wavutaji wanahaha
 
Sukari ni sumu katika mwili wako
Lini waafrika mtajua hili
Anza kunywa chai bila sukari na pia kula vyakula visivyo na sukari
Ndio maana nguvu za kiume zimekuwa mgogoro kwa wanaume na vitambi vimeongezeka kwa wanawake
 
Wanajipigia tu kwakua wanajua KIZIMKAZI hajui chochote kuhusu watanganyika.yy apewe safari za nje y nchi TU.
 
Sukari Tanzania inafanywa kama madawa ya kulevya na wauzaji wana mifumo ile ile tu...Serikali kama inasema kuna uhaba na wakati Zambia,Uganda na Malawi zipo za kuzoa tu si warehouse yeyote mwenye mtaji akachukue alete kuuza kuliko kila mwaka wanatengeneza deal nani apewe kwa kutoa rushwa kubwa kubwa hakuna tatizo la Sukari Tanzania hilo Tatizo linatengenezwa ili wachache wapewe vibali tu...Nakonde tu hapo Sukari bei yake ni ya kuokota..
 
Dom bei 5000 bila woga. NAKAZIA 'the controlled price is a price at which the commodity in question is not available"
 
Sukari ni sumu katika mwili wako
Lini waafrika mtajua hili
Anza kunywa chai bila sukari na pia kula vyakula visivyo na sukari
Ndio maana nguvu za kiume zimekuwa mgogoro kwa wanaume na vitambi vimeongezeka kwa wanawake
Sumu zipo nyingi si sukari tu hadi mafuta ya kupikia, shida kuepuka hivyo vitu si rahisi ukitaka kuzingatia mambo ya afya kwa ukamilifu unaepuka vp ngano na mafuta?
 
Back
Top Bottom