La ITV kufungiwa halimo, serikali haiwezi kuifungia, ila Mzee Mengi, ana ajenda yake na anaitumia ITV kama moja ya strategies za kuifikia ajenda hiyo. Kitu ninachojua, ITV haitafungiwa bali itakufa natural death baada ya ajenda ya mmiliki kutokamilika.
Ajenda hiyo haitokamilika kwa sababu anatumia mlango wa nyuma kutimiza malengo yake.
Wengi wanamuona Mzee Mengi kama mkombozi fulani kwa mtindo wake wa kuuma na kupulizia, amamuuma adui fisadi papa, huku anampulizia mlezi wa fisadi papa kwa kisingizio cha kutaka kumsaidia.
Tatizo atakalokumbani nalo mzee wetu huyu ni kuwa hawa anaojidai anataka kuweasaidia, ndio hao hao wanaomuona kuwa yeye ni adui na kwa hakika, watammaliza.
Vita dhidi ya ufisadi ni vita kubwa inayohitaji kupigwanwa from within. Mzee Mengi kwa kutumia media yake, anataka kuwashawishi watanzania tukae nyuma yake kuelekea kwenye ukombozi wa kweli dhidi ya ufisadi. Tatizo watu anaotaka kupigana nao, wana nguvu zaidi yake, hivyo he is fighting a loosing battle na ndipo atakapoangamia na ITV yake na familia nzima ya IPP.
Mimi naungana na ile filosofia isemayo 'If you can't beat them, join them', vita hii ndio mwanzo wa mwisho wa Mengi kwa sababu nchi iko mikononi mwa mafisadi Left, Right and Centre.
Mtazamo wako Pasco sio. Mapambano, hasa haya magumu ya kupambana na ufisadi na mafisadi yana strategies nyingi; Mfano Kule Bungeni wapo wawakilishi wanaopambana, wengine ndani ya CCM mf. Dk. Mwakyembe, Anne Kilango, Selelii, Shelukindo, Spika Sitta na wengineo. Wengine wapo nje ya CCM mf. Dk. Slaa na wengine. Mengi na yeye anatumia nafasi yake kupambana kwa upande mwingine. Tukubali kuwa Mengi amepata ujasiri wa hali ya juu sana kuwataja kwa majina hao aliowatuhumu kuwa ni Mafisadi Papa hapa nchini, huku akifahamu nguvu zao, hasa za huyo RA a.k.a Kingmaker.
Hebu tuache unafiki, na tuongelee reality, hivi nani asiyejua jinsi baadhi ya wafanyabiashara waliowahi "kutembelewa" na TRA baada ya kujionyesha waziwazi kuitupa mkono Serikali na kuelemea upinzani? Au mfano wa Thomas Mollel a.k.a Askofu wa Arusha na Mirerani ilivyotangazwa kuwa anafilisiwa mali zake ikiwemo hotel ya Pallsons baada ya kuamua kuwa mfadhili wa NCCR Mageuzi enzi za Mrema? Alipoelewa somo akarudi kwenye mstari, matatizo yake yakaisha.
You win by right strategies man, and use your brain, not just feelings/heart. For Mengi to say that he named and shamed the "corruption sharks" in order to help Kikwete is a strategy because Kikwete can't say "No no no, I am not fighting against corruption in Tz". JK has to use proxies, as you heard, those who criticized Mengi are the members of "mtandao". But note that they (especially Sophia Simba and Mkuchika) couldn't criticize Rostam's counter-accusations because they are "his" people. Shame on them!
This is a multi-pronged war:
Some fighters are within CCM,
Some fighters are with other Political parties,
Some fighters are not affiliated with any political party,
Some fighters are media practitioners and owners,
Etc, etc, etc.
Aluta Continua!