ITV, Mengi to be dealt with soon


Wakuu,
Kama kuna MewanaJF mwenye details zaidi kuhusu huyu jamaa Nkoma na atupe data hapa ili tuzifanyie kazi mapema please,
Nawakilisha
 

toka nimejiunga hapa JF nimepata ufahamu ambao sikuwahi kuhupata sehemu yoyote hile.Napata uchungu sana na nchi yangu Tanzania hasa ninapo ona viongozi wetu tulio wachangua kwa kuamini wata badilisha maisha yetu na kutuletea maendeleo kiujumla,kinyume chake wao ndio wamekuwa vinara wa kutuangamiza kwa masilahi yao binafsi.

Ndugu zangu wanaJF hii vita ni ngumu sana,tusi subiri mtu au kiongozi aje atusaidie kwenye vita hii bali mimi na wewe! tuna paswa kupambana na huu uaramia unaofanya na watu wa chache kwa manufaa yao na familia zao.
 

 
A wrong move at the wrong time....trust me, it could be a blessing in disguise for RM. Serikalini kuna baadhi ya watu wameamua kupumzika kufikiri. Hawasomi public mood
 
Hivi hao jamaa walipotuma hizo barua walikuwa wanajua kuna kesi mahakamani? au wanafikiri wao wanaishi kwenye parallel universe; au dhana ya subjudice hawaifahamu? Maana, kulikuwa pia na kikao cha kamati ndogo ya ulinzi na usalama ambayo nayo ilitaka maelezo na ushahidi kutoka kwa Mengi kwa sababu za kiusalama wa taifa! siku mbili baada ya hii barua kutolewa..
 
Maana, kulikuwa pia na kikao cha kamati ndogo ya ulinzi na usalama ambayo nayo ilitaka maelezo na ushahidi kutoka kwa Mengi kwa sababu za kiusalama wa taifa! siku mbili baada ya hii barua kutolewa..
Na Mengi alienda? Ningekuwa mshauri wake ningemzuia...!
 
Mkuu, wacha ubaguzi 🙁

Theoretically, Yes!
In Practice, kila nchi ina ubaguzi ktk mambo ya aina fulani. Wa-Asia kaka hata siku moja hawatakupa nafasi kama hiyo.

Uliza Uambiwe jinsi Wasidi wanavyoishi India.
 
Pundamilia,
Naona wikiendi uliianza toka jana, ....

Niko gado na ninakataa isuue.

Hupendelea kungalia maswala in 3D.

Hili jamvi halinogi bila ya changamoto.

Unakumbuka enzi za midahalo shuleni?

Endelea kufurahia mapumziko yako ya mwisho wa juma.
 

Na wewe mkuu achana na Punda jadili hoja za Punda.

Huna haki ya kuhoji kwanini Punda anahoji.

Mimi na wewe tuko huru kujieleza, kama hukubaliani na hoja zangu hujalazimishwa kuzijibu.

Ni nini motive ya Mengi kuanika barua hadharani?
 
Mkuu yamekuwa hayo tena,umepiga bonge la U-Turn,polepole tutafika tu na ukweli siku zote utasimama

Hoja hujibiwa na hoja.

Maelezo yangu yapo sawa kabisa, kama kuna mahali hujaelewa, tafadhali nijulishe.
 
Wakuu naomba niulize, TCRA (serikali) wamemlima Mengi barua kwa sababu na makosa waliyoyaona wao, sasa je kwa kitendo ambacho Habari corporation ilikifanya cha kuchapisha matoleo mawili ya RAI kwa tarehe moja na namba zilezile, hivi serikali imechukua hatua gani kwa Kampuni hiyo na mmiliki wake? Au ndo mambo ya kulindana na kumuonea mnyonge???
 


Mkuu je wadaganyika wametoa malalamioko yao kuhusu suhala hili kwenye vyombo husuka??
 
Na wewe mkuu achana na Punda jadili hoja za Punda.

Huna haki ya kuhoji kwanini Punda anahoji.

Mimi na wewe tuko huru kujieleza, kama hukubaliani na hoja zangu hujalazimishwa kuzijibu.

Ni nini motive ya Mengi kuanika barua hadharani?

nani kakuambia ni Mengi ndiyo ameanika hiyo barua? Umeona nakala zimetumwa kwa watu wangapi? Umeona maelekezo ya barua ya kwanza kuhusu nakala? Unless kuna unachojua kuwa ni yeye ndiye aliyeanika hadharani maana hapa imewekwa na Invisible ambaye kwa kadiri ninavyojua siyo Mengi!
 
Mimi nadhani watu humu tunatumia emotions bila kuangalia mambo kwa undani . Mengi amekosea katika hili, huwezi kutumia vyombo vyako vya habari kumuattack mtu mwingine. Nakubalina kile anachosimamia vita vya mafisadi , lakini kitu alichofanya ni kosa. Tuache ushabiki usio na msingi tuangalie hiko kipengele cha 22 kilichotajwa hapo juu kinasemaje .

Hivi itakuwaje kama kesho na mimi nitaanzisha TV yangu na kuanza kusema watu fulani ni mafisadi . SO where are we going to draw a line. Hili ni tatizo , na ninaishukuru bodi ya utangazaji kwa kum-summon Mengi.
 

Nimeambiwa na Mengi

Uliza swali jingine.
 

Mkuu tena habari nyingine ya kushambualia watu vile vile? Nakwambia bongo tusiponyanyua mawe tukatoana meno ili adabu ichukue mkondo wake, tutaendelea kuburuzwa tu!
 
Nimeambiwa na Mengi

Uliza swali jingine.



Mtoto wa kuumeni kuwa mpole punguza taharuki, si wewe uliyesema hoja inajibiwa kwa hoja kwenye post yako hapo juu au?? sasa mbona unaleta mambo ya akina khadija kopa??? Mipasho kwa kwenda mbeleee, i wish mods wangeanzisha kundi la taarabu hapa nafikiri tungekuwa na waimbaji wazuri sana.. hahaha
 
Serikali hii imejaa vilaza wengi, wao wanafikiri kwa kuifungia ITV ndio wanamkomoa Mengi kumbe unknowingly ndio wanamjenga! Wananchi sasa wanajua kua watoto wao wanasoma kwenye mchanga bila madawati kwa sababu wajanja wengi ambao ndio hao mafisadi wamekuwa wakiibia nchi hii toka enzi ya mzee RUKSA ; kuanzia kwenye mpango wa DEBT conversion ambayo baadae ikezaa EPA; sasa mapesa waliokomba hawa watwana yangeliweza kutupatia dawa kwenye zahanati zetu na maman na dada zetu wasingekuwa wanazalia barabarani au kulala wawili wawili huko kwenye maternity wards.Hivyo basi mtu yeyote atakayekuwa upande wa mafisadi na kuwapiga vita wapinga ufisadi [akiwamo Reginald Mengi] atakuwa anapambana na nguvu ya umma!!
 

Mkuu Pundamilia, kwanza naomba nitambue uhuru wako wa kikatiba wa kutoa maoni. Pili naomba niungane na Kapinga, Mzee MM na wengine juu ya yale waliyochangia. Pia nami nikuulize hapa:

  1. Unauhakika gani kuwa Mengi ndiye anayezifikisha docs hapa JF?Kama ni Mengi then ni Mengi pia kakwambia kuwa hawaamini maAdvocates wake?Asingewaamini angewapa hiyo kazi?
  2. Unaona Ubaya gani kwa Watanzania kupata info kama hizo za kwenye barua za Sakata la M na TCRA humu mtandaoni?Do u have good intentions na JF au nawe ni walewale mamluki tu?


Kuhusu Mengi kutaka kuonewa huruma na Wananchi, kwa mtizamo wangu, sidhani kama biashara za Mengi na mambo yake mengine yanahitaji huruma ya Watanzania ili kufanikiwa. Ila hayo ya Mafisadi kwa sasa yatahitaji huruma ya Wananchi, kama ambavyo tumekuwa na huruma hata wakaendelea kutunyanyasa na kutunyonya ndani ya ThiThiEm.


Let it be so said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…