[[Wangekuwa hawakamatwi ungeona hao wachungaji wanaotumia viungo vya albino wakishikwa? hujasoma? hivi kanisani huwa mnavitumia viungo vya albino kufanyia nini?
Hayo mengine yote porojo na nimeshayajibu, kama ni wizi ujambazi, rushwa, ufisadi, uongo, uvivu, yalikithiri wakati wa Nyerere kuweka misingi mibovu ya nchi.
Chakula hakuna, ufanye nini ukae na njaa? unakwenda RTC unahonga unapewa chakula, hapo ndipo rushwa ilipoanza.
Nguo hamna unafanya nini? unakwenda Kenya unanunuwa unazipitisha kimagendo, ukishkwa unahonga khanga doti moja unaachiwa, hapo ndipo mianya ya rushwa ilipoanzia.
Watu wanakamatwa hovyo wanapelekwa vijiji vya ujamaa, huko shida, porini, wanaoumwa na nyoka haya wanaliwa na simba haya, wanaokufa kwa kukosa matibabu haya. Wengine wanatoroka na kuanza ujambazi.
Huo ndiyo wakati wa Nyerere.