Vyombo vya habari vina nguvu sana katika jamii. Vinaweza kuelimisha na kupotosha. Kwa msingi huu, vyombo vya habari vinatakiwa kuwa makini pale wanapoelimisha jamii.
Hapa nilipo naangalia kipindi cha watoto cha ITV. Katika eneo la watoto kujifunza mafumbo, kuna mtoto ametoa fumbo "Mama yake anaumwa dawa yake ni karoti"
Watoto wote pale studio wamenyoosha mkono wakimaanisha kuwa wanalijua jibu. Matokeo yake walipoambiwa wajibu, wakatririka mashairi ya wimbo. Jibu lake ni "nipe karoti maharage sijazoea kiokote"
Cha kushangaza, wale watangazaji walicheka, fumbo limepata jibu. Kwa kuwa huwa nawajenga watoto kufuatilia vipindi vya TV nikiwa nyumbani, hii si mara ya kwanza watoto kuibuka na vitu vya hatari wakiwa live.
Kuna wakati wanaimba nyimbo zisizo na chembe ya maadili. Chonde ITV, wekeni utaratibu wa kulinda maadili. Kama hamuwezi ombeni ushauri, la sivyo ondoeni vipindi mubashara.
Leo nimemwambia mwanangu hali ikiendelea hivi hatutaangalia tena hiki kipindi. Hii inanikumbusha sehemu fulani, mbele ya Mkuu wa Wilaya, kwenye sherehe, watoto walikuwa wanaigiza athari za ulevi kwa familia alafu kuna mtoto aliigiza mzazi mlevi 😉 akiporomosha matusi ya uchi.
Watu walipigwa ganzi. Kabla ya kuchukua hatua, mtoto akayapiga mengine makali zaidi, ikabidi MC aweke muziki na igizo likaishia hapo!
Sijui Afisa Elimu walimbebea mbeleko gani DC!