Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Huyo mama simjui vizuri ila naibu wake nafasi hiyo ni kubwa sana,kwa kifupi angebaki kuwa mbunge tu
 
Usizungushe maneno, aliyewateua anaamini ushirikina, na vile kawashikia akili hao mawaziri ndio maana wanaongea vituko hadharani. Ndugulile alisimamia taaluma akatumbuliwa, hawa wawili wameamua kusimamia tumbo ndio maana wamegeuka vituko.
 
Kwa jinsi rais ameanika uwezo duni wa wanataaluma wetu, ni aibu hata kusema tuna wasomi nchi hii. Rais anasema hakuna corona kwakuwa tumefanya maombi, mtu ni msomi anasimama na
kusema kweli corona imeisha kwaajili ya maombi! Natamani hii corona ifyeke wahuni wote waliokuwa wanasema Tanzania hakuna corona maana taifa letu linalindwa na Mungu, na uhuni mwingine kama huo.
 
Hongera kwa Mara nyingine tena chagu wa malunde kwa kuwa mkweli. Mimi ni mkosoaji wako mkuu katika mambo mengi lakini unaposimamia ukweli lazima nikupe heko zako.

Kweli Katibu Mkuu Prof Mchembe ndiyo chanzo cha tatizo. Yeye ndiye aliyepeleka sampuli za oil chafu na mapapai kule National Health Lab.

Ni ajabu wasomi wa hali ya juu wanasaliti usomi wao kumfurahisha Meko
Always huwa nasimamia ukweli. Fuatilia kumbukumbu za huko nyuma.
 
Mtawaonea bure tu. Tatizo ni Magufuli. Magufuli ndo waziri wa wizara zote. Ukitaka results tofauti deal naye.
Kwanini tusijifunze kwa Dr Faistine Ndugulile? Yeye Kama mtaalamu wa Virology na immunology na huku Ni Naibu Waziri wa Afya alijitenga na UWONGO. Akijibu swali bungeni aliponda sana njia ya NYUNGU kuwa Ni hatari na akasema ndiyo ilimponza Mbunge Ndassa wa Sumve hadi umauti. Baada ya japo Magufuli akamtoa kwenye Baraza.

Lakini kwenye Baraza jipya kawa FULL Minister wa Mawasiliano.

Ukiamua kumsimamia ukweli bila kujali tumbo lako INAWEZEKANA
 
Wanachotaka hawa watu ni Raisi kuukubali huu ugonjwa.

Mheshimiwa Raisi Magufuli endeleza msimamo huo huo. Endapo utakanyaga huu mtego wa kutangaza huu ugonjwa tutakuwa defeated kama Nchi na utaingiza hofu katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Simamia msimamo wako hakuna haja ya kutangaza kitu kwani hata ukitangaza uwepo wa huo ugonjwa watu wataendelea kufa tuu. Simama na mawaziri wako hao ulio waamini.

Usije kuyumbishwa na hizi kelele kwani kuna ajenda kubwa na ovu sana inaendelea. Ukitaka ukose credibility kama Raisi ni utakapo tangaza huu ugonjwa. Simama na msimamo wako kama mwanaume. Na kuwa na subira sana be patient. Hili nalo litapita.
 
Waziri ni msaidizi wa rais katika wizara aliyoteuliwa na rais. Kama rais amekataa na yeye ame kula kiapo cha uaminifu, afanyeje ?. Hanakosa wala sababu ya kujiuzuru kwa matokeo mabaya. Labda angejiuzuru mapema kwa kutokubaliana na msimama wa rais. Wenzetu nchi zilizoendelea kidemkransia wana MSIMAMO WA SERIKALI yahani rais na baraza lake. SISI HAPA TZ SASA TUNA MSIMAMA WA,.... TUMERUDI ENZI ZA ZIDUMU FIKRA SAFI ZA ....
 
Waziri ni msaidizi wa rais katika wizara aliyoteuliwa na rais. Kama rais amekataa na yeye ame kula kiapo cha uaminifu, afanyeje ?. Hanakosa wala sababu ya kujiuzuru kwa matokeo mabaya. Labda angejiuzuru mapema kwa kutokubaliana na msimama wa rais. Wenzetu nchi zilizoendelea kidemkransia wana MSIMAMO WA SERIKALI yahani rais na baraza lake. SISI HAPA TZ SASA TUNA MSIMAMA WA,.... TUMERUDI ENZI ZA ZIDUMU FIKRA SAFI ZA ....
Kwani Ndugulile wakati anaeleza ukweli juu ya madhara ya kujifukiza hakuwa waziri wa serikali ya JMT?
 
Kwani inashindikana nini Viongozi kutoa Muongozo kuwa Kwenye Gari hizi iwe Level seats tu,Na barakoa kila mtu maana utajilinda wewe tena mwingine hana habari nayo ndio kuambukizana kunaendelea kuwepo tu,Maana Hali ni Mbaya tumuombe Mungu sana Na tujitahidi kuelimishana Tuchukue Tahadhari Ndugu zangu.
 
Naona unazunguka mbuyu, mtaje mhusika siyo unazunguka zunguka.

Na mtakwisha sana safari hii kwa ubishi wenu
 
Back
Top Bottom