Uchaguzi 2020 Itakuwaje kama Lissu akashinda Urais bila kupata Wabunge wa kutosha?

Anao uwezo wa kuitisha uchaguzi mpya wa wabunge , hapo ndio kifo cha mende
 
Ni dhahiri shayiri kuwa uchaguzi huu umekuwa mgumu sana kwa CCM kuliko miaka yote. Mwaka 95 ulikuwa mgumu ila hayati Mwl. Nyerere alikuwepo kuokoa jahazi, na mwaka 2015 ulikuwa mgumu ila Mkapa alikuwepo kuokoa jahazi.

Mwaka huu sijaona wa kuokoa jahazi, hata hao wastaafu waliingizwa kwenye kampeni wamekosa mvuto tofauti na ilivyotarajiwa.

Swali langu ni kuwa: Itakuwaje kama Lissu akashinda kisha akakosa kupata wabunge wa kutosha? Si CCM wataamua kumkwamisha?

Jibu liko wazi na alishatamka mwenyewe.
Akishinda maana yake majimbo yote ambayo CCM wamepita bila kupingwa uchaguzi unarudiwa. Hapo lazima akina Nape wakajikojolee. Pili, hayo majimbo unayodhani CCM watashinda wabunge wengi, kama walishinda kwa kuiba kura lazima ngoma iende mahakamani, kuna watu watavuliwa ubunge.
 
Back
Top Bottom