CHADEMA Hawamtukani Hayati Magufuli bali wanazungumzia mateso waliyotendewa wakati wa Urais wake

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Watanzania wenzangu nawasalimu. Nirudi kwenye Mada hapo juu CHADEMA ni Chama kikuu cha Upinzani Tanzania. Chadema mwaka 2015 kilishiriki Uchaguzi Mkuu ambao kilimsimamisha Mzee Edward Lowassa kama Mgombea wake wa Urais na CCM ilimsimamisha John Magufuli na Matokeo yake CCM ilishinda.

Mara tu Baada ya Magufuli kuapishwa PILIKAPILIKA za KUISAKAMA CHADEMA zikaanza zikiwemo za Kuwakamata Wanachama wafuasi na Viongozi na kuwabambikizia Kesi za Uhujumu uchumi mauaji Utakatishaji fedha ili mradi Wakajazwa Magerezani.

Kila kukifanyika Uchaguzi mdogo basi Wafuasi wa Chadema watakamatwa na kupewa hizo kesi. Ulifanyika uchaguzi mdogo Kinondoni uliopekekea Mwanachuo kupigwa Risasi na Polisi lakini Viongozi wa Chadema toka Mwenyekiti na Wajumbe wake Walipewa kesi ya Mauaji ya huyo Binti Akwilina na Kutozwa Faini ya Sh Milioni 320. Kama haitoshi siku ya kwenda kumtoa Mbowe Gerezani Halima Mdee na Wenzake Walipigwa sana na Askari Magereza bila kosa la msingi.

Mikutano ya Hadhara ilizuiliwa Kinyume na KATIBA ila CCM ilikuwa inafanya. Mikutano ya Ndani nayo CHADEMA ikifanya wanakamatwa. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 ilikuwa Vioja Uchaguzi Mkuu 2020 hata Mabango ya Kampeni Chadema Walizuiliwa Nchi nzima ni Mabango ya Picha ya MAGUFULI Wagombea wa Chadema Walikatwa Majina yao Wagombea wa CCM wakapita bila Kupingwa ili mradi Ulikuwa ni UCHAFUZI na Sio UCHAGUZI na MAGUFULI akashinda jwa ASILIMIA 90 Bado ktk utawala wake Wanachama wa Chadema wamepotea mpaka leo hawajulikani walipo kama vile Ben saanane Azory Gandwa na Wengineo.

Tundu lissu alipigwa risasi mchana kweupe Wabunge na Wanachama wa Chadema kununuliwa na kuhongwa Vyeo Kina Halima Mdee kupewa ubunge Viti maalum bila chadema kuhusika na Mbowe kubambikiziwa Kesi ya Ugaidi ili mradi MATESO kwa Chadema.

Leo CHADEMA wanawasimulia WANANCHI MATESO waliyopitia Wanatokea WAJINGA na WAPUMBAVU wachache wanasema CHADEMA wanamtukana MAGUFULI ukweli ni kwamba CHADEMA wanawaeleza WANANCHI namna RAIS MAGUFULI alivyoWATESA Ktk UTAWALA wake wa MIAKA 6.
USHAURI

Binadamu ni Muhimu Uwapo DUNIANI Ukatenda MEMA na MAZURI kwa Watu wote kwani Siku UKIFA watakusema VIZURI lakini Ukitenda MABAYA hakika WATAKUSEMA VIBAYA

1652427482224.jpg
 
Mateso gani?

Kikwete aliwazoesha chadema juice za ikulu, Magufuli akawabania akawa anawapa kina Mrema na kina Shibuda, hicho ndio kiliwauma Chadema.

Kwa kua sasa mama amewaruhusu kunywa juice ya ikulu tena hutasikia wakisema chochote.

Chadema ni wivu tu ulikua inawasumbua kuona Shibuda anakunywa juice ya miwa ikulu wao wanakosa.
 
Hao wahafidhina wanao mtetea Magufuli na matendo yake barbaric wanadhani kama waathirika na matendo yake wangekuwa na visasi pangekalika?

Mnadhani familia yake ingeishi kwa furaha na kula kodi zetu kwa raha?

Ndugu na jamaa zake waliokuwa wanufaika na wanafahamika wangeendelea kutamba kila walipo?

Acheni tuu watu waseme mabaya yake nyongo iishe maisha yaendelee tu, na msiwazuie kusema maana mtaacha familia nayo igeukiwe na hakika itakosa raha kama wengine walivyo kosa raha wakati kosa sio lao.
 
Watanzania wenzangu nawasalimu. Nirudi kwenye Mada hapo juu CHADEMA ni Chama kikuu cha Upinzani Tanzania. Chadema mwaka 2015 kilishiriki Uchaguzi Mkuu ambao kilimsimamisha Mzee Edward Lowassa kama Mgombea wake wa Urais na CCM ilimsimamisha John Magufuli na Matokeo yake CCM ilishinda....
ENDELEENI kumkomoa huyo mnaedhani aliwapa mateso mpaka akome kabisa. Na huyu ambae yupo ENDELEENI kumtukuza na kutangaza sifa zake nzuriii ili 2025 TUUUNGANE wote apite bila kupingwaa Kwa kuwa anafanya ambayo na nyiee mnayapendaaa.
 
Magufuli hakuchukiwa na upinzani tu bali hata CCM wenyewe walikuwa wanamchukia ila walikuwa tu wanaogopa kusema na wengi walikuwa wanamuunga mkono kinafiki kwasababu alikuwa hana mzaha kwenye kazi na kitu ambacho kiliwakera sana mafisadi
 
acha kuwaza kwa kutumia makalio mkuu.mfano ungepitia mateso waliopitia ungejisikiaje bwashe.heri wapatanao kuliko wagombanao
 
Mateso gani?

Kikwete aliwazoesha chadema juice za ikulu, Magufuli akawabania akawa anawapa kina Mrema na kina Shibuda, hicho ndio kiliwauma Chadema...
Ni mpumbavu na Mjinga ndio hajui Mateso waliyopitia Chadema
 
Watanzania wenzangu nawasalimu. Nirudi kwenye Mada hapo juu CHADEMA ni Chama kikuu cha Upinzani Tanzania. Chadema mwaka 2015 kilishiriki Uchaguzi Mkuu ambao kilimsimamisha Mzee Edward Lowassa kama Mgombea wake wa Urais na CCM ilimsimamisha John Magufuli na Matokeo yake CCM ilishinda....
Lema aliwahi kusema ni heshima mbele za Mungu kumtukana Lowassa, lakini Lema huyo huyo juzi kati kakataza wanachadema kumtukana Rais Samia.

Napata tabu kuelewa hii ishu ya kutukana na chadema kwamba kuna baadhi ya viongozi huwa wanatukanwa au wana stahili kutukanwa?
 
Magufuli hakuchukiwa na upinzani tu bali hata CCM wenyewe walikuwa wanamchukia ila walikuwa tu wanaogopa kusema na wengi walikuwa wanamuunga mkono kinafiki kwasababu alikuwa hana mzaha kwenye kazi na kitu ambacho kiliwakera sana mafisadi
Yeye mwenyewe alifika hatua akawa analia kama mtoto baada yakuona ametengeneza maadui kibao akaanza kuwabrmbeleza akina rostam wakati tayari kasharikoroga
 
Back
Top Bottom