Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,055
- 79,399
Habari za Sabato!
1. Ndugu Watanzania nichukue nafasi hii Kwa sehemu yangu kama raia wa Nchi hii kama mlivyo nyie. Kuzungumza machache kama sehemu ya maoni na mchango wangu.
2. Binafsi nipo kwenye hali ya Wasiwasi mkubwa na hali inayoendelea. Naamini sio mimi pekee yangu nipo katika hali hii. Wote tuliona yaliyotokea na tunaona hali ilivyo. Hatuwezi kujidanganya hatupo kwenye uelekeo mzuri.
3. Kila mtu naamini anatamani afanye kitu ili mambo yakae sawa.
4. Wale wenye Imani sana wanaomba. Wale waandishi tunafanya sehemu yetu kuhakikisha tunakuwa sawa. Vyombo vya usalama nao vivyo hivyo.
Kila mtu Kwa sehemu yake anafanya kuhakikisha Nchi yetu inakuwa sawa na kurejea katika hali ya utulivu.
5. Tusiwe kama tunajenga Mnara wa Babeli. Yaani machafuko. Kutokana na lugha gongana.
Lengo letu wote ni Moja. Ndugu Watanzania wote lengo letu ni Moja Kujenga Taifa letu.
Tusigongane lugha kama tunajenga Mnara wa Babeli. Unatumwa kijiko unaleta beleshi.
6. Binafsi kama Mtibeli nimeona Kila mtu anataka aonyeshe yeye ni Mzalendo. Kuna mashindano ya Kujiona Mwema hali inayopelelea dhulma kufanyika.
7. Imefikia hatua mpaka sasa watu wapo tayari kupigana vita.
Sisi wote ni ndugu. Sisi ni ndugu jamani. Amkeni.
Polisi na vyombo vya Dola nyie ni Watanzania.
8. Tumewezaje kufikia hatua ya kushikiana bunduki na kupigana risasi. Tunafikaje huko?
Kisa Nini? Kujenga Nchi?
Mliona wapi Nchi inajengwa Kwa kushikiana silaha. Wapi?
9. Lazima tunyenyekee. Lazima haki itendeke.
10. Kujiona Mzalendo kuliko wengine huleta maumivu.
Kila mtu ni Mzalendo Kwa kiwango chake alichojaliwa. Na kila uzalendo wa mtu ni muhimu ndani ya Taifa hili.
11. Imefikia hatua watu wanatekwa na kuuawa kisa neno uzalendo. Nope! Mambo hayaendi hivyo. Huko ni kuharibu Nchi.
12. Yawezakuwa wapo wazalendo wakubwa kuliko wengine lakini haiwapi uhalali wa kufikia kiwango Cha Kujiona wao ndio VVIP Citizens. Lakini lazima waheshimu wengine na kufuata Sheria.
13. Vyama vya upinzani Kwa miaka mingi vimeilalamikia serikali kuhusu Madai kadhaq ya HAKI za kisiasa na uadilifu wa viongozi hasa wa CCM. Mwanzoni ilikuwa haki Yao kukosoa lakini mambo yalibadilika ukosoaji ukageuka kuwa kosa baya likaitwa ugaidi na likafikia kwenye uhaini.
14. Upande huu wanaona hawa sio Wazalendo na maadui wa Taifa upande huu nao wanaona vivyohivyo.
15. Ndugu Watanzania, tukishafikia hatua ya kushikiana bunduki na silaha huo sio wakati wa malumbano Tena. Ni jukumu la wazee, vyombo vya Dola na watu wenye ushawishi kufuata malalamiko ya pande zote mbili.
16. Kama ishu ni katiba mpya na haki sawa za kisiasa na tumefikia kiwango Cha kumwagana ubongo. Ni akheri watu wakae chini hiyo katiba na michoro ya haki sawa ifanyike.
17. Tusiwe vipofu na kujifanya hatuoni nini kipo mbele yetu. Tupo kwenye hatari kubwa.
18. Oooh! Taikon Mimi naogopa nikitoa katiba mpya au kuleta HAKI za kisiasa wakiingia wengine watalipa kisasi. Tutaishi maisha magumu.
19. Sikiliza, Kuna stage ikifika njia pekee ya kupunguza madhara ndani ya Taifa ni kujishusha chini ya makubaliano ya kuhakikishiwa usalama wako na familia Yako.
20. Tusisubiri maji yakafika puani. Maji yakifika puani wahanga watakuwa wengi na Taifa litakuwa rehani kuanguka.
21. Fikiria Kikosi ni kilekile Tena kinaongezeka. Huku Kuna CHADEMA, na Kikosi chake kinachoongozwa na Tundu Lisu. Ameongezeka Gwajima, kaongezeka Kakaake Polepole, wameongezeka wanaharakati wako pande zote.
22. Hatujui kesho ataongezeka nani. Huku upande wa serikali Kikosi kikibaki kilekile na zaidi kinapungua au kinafanya kazi Kwa sababu ya mshahara.
23. Ongezeko la vijana wa Gen Z ndio Kabisa unafanya hofu na Wasiwasi vishamiri. Ukizingatia vijana wengi wamesoma na wapo wapo hawana Maisha.
24. Vita hivi haviwezi kuisha ikiwa Kikosi ni kilekile.
Ni kama vita ya shetani na Mungu. Haviwezi kuisha bila mmoja kuangamizwa au wakae meza Moja wapatane.
25. Sasa tutaishi hivi mpaka lini. Kila siku matamko. Kila siku tarehe za maandamano. Mpaka lini Maisha haya? Unaweza ukasema ni hangover ya uchaguzi lakini sivyo hata kidogo. Lock ilishatolewa tarehe 29oct.
26. Kuna vijana wengi sana wasio na kazi ambao haya maandamano kwao huyaona kama mkombozi wa Maisha Yao.
27. Jana nilikuwa Manzese pale Kuna kitu nilienda kununua. Katika kudodosa dodosa niligundua Watanzania sasa tunaenda kugawanyika katika makundi makuu mawili. Jambo ambalo kiusalama sio zuri.
28. Kundi la kwanza ni kundi la waliojiriwa au kujiajiri. Hili wamejipata na hawapendi maandamano kutokana wanashughuli za kufanya. Na wanaogopa mifumo Yao ya kiuchumi inaweza kuathirika na maandamano.
29. Kundi la pili ni kundi la ambao hawana kazi za kufanya, hawana kazi au wanakazi lakini kipato chao ni duni. Kundi ni kundi kubwa sana kutokana na janga la ukosefu wa ajira. Hawa wanataka maandamano.
30. Kiusalama isije tokea vita ya walionavyo na wasionavyo. Na viashiria tumeviona kwenye Ile Mo29. Pia huko mtandaoni wenye biashara zao wakilaani na kutoa mkwala Kwa waandamaji.
31. Chakufanya;
a) Wale wanaochukiwa na waandamaji wasipewe maiki ya kuzungumza mara Kwa mara.
Kila wanapozungumza wanachochea hasira za wanaotaka kuandamana. Huona hiyo kama dharau.
b) Kutumia watu ambao jamii inawajua kwa Haki au uadilifu.
Mnawajua. Angalieni watu ambao wanazungumzwa Kwa mazuri kutokana na kazi zao au uadilifu wao. Watu wasio na Scandal za hovyohovyo.
Kina Anthony Mtaka.
Kina Mwalimu Mwakasege
Kina Sheikhe Ponda. Haohao wenye misimamo mikali wakitumiwa wanaweza kutuliza mambo.
Kuna Mamiss Tanzania wenye heshima. Tumieni hao.
Kuna Wachungaji wa Kisabato maarufu wasiojihusisha na siasa tumieni hao.
Tumieni wakina Ney Wamitego, tumieni haohao. Wanasema dawa ya moto ni moto.
Tumieni wale watu wanaowaheshimu na kuwapenda.
Msitumie nguvu na vitisho. Sisi ni ndugu. Wewe jaribu kumtisha mdogo wako au kakaako akutishe wakati unadai haki yako utaelewa wao wanahisi na kufikiria Nini.
Kuwa na silaha hakuwezi kuwatuliza. Zaidi Kuna chochea mzozo na uasi.
c) Tumieni Wanasiasa wa Upinzani Kwa nia ya dhati na sio kuwatapeli au kuwazuga.
d) Wapeni nafasi waandamane ila jukumu la ulinzi wa hayo maandamano Wapeni viongozi wa upinzani kama CHADEMA. Ni rahisi sana.
Waambieni mnahaki ya kuandamana kudai haki zenu na serikali ipo kwaajili ya kusikiliza raia wake ikiwemo wanachadema au wapinzani. Lakini viongozi wa CHADEMA mnajukumu la kulinda na kuhakikisha hamleta vurugu na uvunjifu wa amani. Kazi kwisha.
Wanasema mchawi mpe mtoto alee
Kuwazuia viongozi wa CHADEMA au upinzani ni kutengeneza bomu la maandamano yasiyoweza kudhibitiwa bila kuleta maafa.
Mbona Kina Lisu waliandamana nafikiri mwaka jana hapa. Kulitokea Nini.
Sasa unazuia viongozi wa upinzani wote alafu wakumpa lawama pakitokea matatizo mtampa nani?
Kwa sababu mkisema CHADEMA utaambiwa sio ya CHADEMA bali walikuwa ni wananchi.
Au ndio kusema Wameshawishiwa na Mange Kimambi sio? Hiyo haiingii hata akilini.
Mnaweza kukamata Kwa muda viongozi wenye misimamo mikali lakini sio mkamate viongozi wote wakubwa.
32. Sasa utazuia maandamano Leo. Shughuli za kiuchumi zitasimama. Utazima mtandao. Siku mbili tatu kutakuwa kawaida. Uchumi umesimama na wageni na wawekezaji wanakuwa wanaona hatari ya kiusalama.
33. Baada ya siku kadhaa inatangazwa tarehe nyingine ya maandamano.
Mambo yanakuwa yaleyale.
Uchumi unasimama
Wageni wanakimbia
Gharama za Doria na ulinzi zinaathiri bajeti.
Hofu inakuwa kubwa na watu wanaathirika kisaikolojia.
Nchi inatrend Tena huko duniani Kwa sifa mbaya.
Mpaka lini?
34. Tusisubiri haya mambo yakawa ndio culture mpya ndani ya Taifa letu. Yakizoeleka hapa tutatafutana. Kama hapakuwa na maandamano na Bado maendeleo ndio yakusua sua. Tujiulize pakiwa na maandamano Kila mwezi au Kila baada ya miezi miwili tutatoboa?
35. Msifikiri watakaoumia ni wananchi pekee Yao. Nope! Wananchi wengi ni Gen Z ambao wamekata tamaa. Hawana Chakupoteza. Washazoea maisha ya kuungaunga.
Bhana eeh! Nimechoka kuandika.
Msisahau HAKI, UPENDO, AKILI NA UKWELI huo ndio utibeli.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam