It is wrong to instigate chaos for political ambition | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

It is wrong to instigate chaos for political ambition

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amanibaraka, Jan 14, 2011.

 1. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  DSC04540.JPG ni wazi kuwa viongozi na wanachama wa chadema wanaombea nchi isitawalike, uchumi uharibike, mambo yaende vibaya ili waseme ccm wameshindwa na baadae waje ku claim ushujaa. This is wrong and very unacceptable. Hivi hakuna ethics katika siasa?
  Chadema wajue kuwa wakishajiisha hilo likafanikiwa na wao hawatatawala nchi hii. Wote tunapenda mabadiliko lakini this is not the way to go. Tuwape nafasi ccm watawale washindwe kwa halali ili 2015 slaa awe raisi. Tusi instigate fujo.
  Nanyi viongozi wa dini acheni kujiingiza katika siasa mnatugawanya waumini.
  Yakiharibika isisemwe kuwa hatukuonya tunaoona mbali.


   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini usisme kuwa ni baadhi ya watu wa CCM na serikali ambao wanafanya mambo ili CCM ionekane haiwezi kutawala? Walioingia mikataba mibovu ni Chadem? Walioshindwa kesi ICC kwa hoja nyepesi ni wanasheria waliokodiwa na Chadema? Waliouawa raia Arusha ni polisi wanaotekeleza sera za Chadema? Unachojaribu kufanya ni kutonyoshea kidole mahali panapostahili na badala unajaribu kutafuta kisingizio. Chadema ikijijenga kwa sababu ya uzembe na makosa ya CCM.. ndio sehemu ya siasa na itakuwa ajabu chama cha siasa kisichotaka kutumia nafasi za kisiasa zinazowekwa miguuni pake kama zawadi.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mengine yote nachukulia kama hujasema maana sijaona point ya maana!Ila hapo unaposema "ccm waachwe mpaka 2015 washindwe KIHALALI" will they ever?Huo uhalali ulikua wapi uchaguzi uliopita?Kama bado hujagundua..kwenye siasa za bongo hamna uhalali wowote..mabavu ndio yanayotawala!Na ndio maana polisi wameua wananchi bila hatia na hamna yeyote kwenye hiyo serikali aliweza kusimama na kuonyesha makosa yaliyofanywa na polisi!Wanaoinstigate vurugu hapa ni serikali tawala na sio vinginevyo!
   
 4. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuona mbali umeanza jana sio?

  Basi ndiko ulikokosea ulipashwa uwe umeanza tangu miaka 50 huku ya utawala wa kidhalimu na mauaji ya CCM. Yaani unataka CCM iendelee mpaka 2015 ili fungu uliloahidiwa litoke sio?

  Sisi tayari tumeshaanza kuchoka kuzika kila leo. Mbona CHADEMA kuokota na kuzika kwa heshima zote za kibinadamu maiti ya wenzetu mliowaua na kuwatelekeza kwenye mitaro ya maji machafu Arusha iwe inawauma kiasi hiki?

  Kaa pembeni acha longolongo zako hizo.
   
 5. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa yako mpaka CCM inachinjwa shingoni na jopo kubwa la watu wake wenyewe na kwa kisu kile kile na ukatili ule ule ambao chama chako hiki kimekua kikiwatendea wadau wake wengi tu.

  Hivi unayaonea hurua haya tu, makubwa, bora uanze mapema kuvuta bangi au kubwiya unga ili usije ukayashuhudia mazito zaidi kabla ya mwezi wa sita mwaka huu.

  Jitapishage maji ya bendera mapema kwani hutuzidi kitu kwa kuwekeza CCM na baadaye kuonekana mbwa mwizi. Angalia mashuwa isije ikazama kwa mbinuko juu chini ukaja ukashindwa pa kutokea.

  Na wewe usije ukasema hatukukuonya mapema.
   
 6. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Najua nyote u see my point lakini mmeamua kukandia. So mbaya. Lakini the triumph of Chadema will definitely be at a cost of dividing this great nation!!
   
 7. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  hapo ndio ncha ya akili yako imefikia...... siku zote CDM wakifanya efforts zao husemi.... leo umeona majeneza ndio umepata point ya kuleta chuki dhidi ya CDM .....
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya Tena. Makada wa CCM Mtawadanganya Wasio na Akili Sio Wananchi Tulio na Macho. Alie Wapiga Risasi Raia Wasio na Silaha ni Nani? au ni JK?
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hivi ni Chadema ndio walipull the trigger na kuua watu? Muuaji unamjua ila unajifanya unapenda mabadiliko, anza na mabadiliko kichwani kwako kwanza.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CCM imepewa nafasi sana tangu iliporithishwa na TANU madaraka mwaka 1977, nchi imekuwa miongoni mwa nchi maskini duniani licha ya kuwa na raslimali nyingi sana kuliko nchi nyingi za Afrika na duniani! Badala ya kuijenga nchi hiyo imeuzwa kwa wageni kwa bei ya kutupa kupitia kwa mafisadi ambao wanaonekana un-touchable kwa CCM! Licha ya kupigiwa sana kelele kuhusu ufisadi wa MEREMETA, TANGOLD, MWANANCHI GOLD, DEEP GREEN FINANCE, RICHMOND, DOWANS, EPA, nk CCM imekuwa ikijifanya kuficha kichwa kwenye mchanga kama afanyavyo mbuni huku kiwiliwili kikiwa kinaonekana!

  Right, unafikiri CCM wakipewa miaka mingine mitano watashughulikia ufisadi wa MEREMETA, TANGOLD, MWANANCHI GOLD, DEEP GREEN FINANCE, DOWANS, EPA, MIKATABA MIBOVU YA MADINI, MBOLEA ZA RUZUKU, nk na hatimaye kulinda raslimali za nchi zisiende mikononi mwa mafisadi wa ndani na nje ya nchi?

  Hata kama na wewe unafaidika na matunda ya ufisadi, ndio maana bila aibu unatetea mauaji ya raia wasio na hatia, wenye raslimali wameshaamka, muda wenu wa kuwa CHAMA CHA UPINZANI hauko mbali! Stay tuned!
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mbona unafumba macho ili usiyaone majambazi yaliyovaa magwanda ya kijani yanayotafuna uchumi wa nchi hii bila aibu ndiyo yanayogawanya nchi? Na wapi umeona kwamba PASIPO NA HAKI KUKAWA NA AMANI?
   
 12. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM walishinda uchaguzi, wana mandate ya kutawala. let them. Kuinstigate migomo, fujo, chaos, mauaji, chuki, sio jambo sahihi.
  Role ya opposition ni kuelekeza, kukosoa, kutoa mbadala wa sera, kuwabana watekelezaji wa mipango ya serikali. lkaini unapoinstigate fujo ina maana unataka ufanye mapinduzi kwa nguvu ya umma. kwa nchi kama Tanzania ambayo tumejiwekea utaratibu wa kujitawala hilo sio sahihi.
  Hivi kwa mfano, hii sheria inayowapa polisi haki ya kuzuia maandamano obviously ni mbaya, lakini ni sheria halali. Hivi kwa nini Chadema na ma CUF wassipinge bungeni?   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hapa ndio nashindwa kuelewa... yupi anayeistigate chaos...

  anayenyayasa au anayenyanyaswa??
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mtu kaweka post nzuri sana ya kutotaka nchi kupelekwa katika kutokutawalika kwa ajili tu Chadema wamekosa madaraka. Wangoje 2015 na wasitake kutupeleka kwenye fujo. Hamna nchi iliyotwaliwa kwa fujo ikatawalika.

  Ni watu kama wewe ambao hukaa na kuchochea fujo wakati wewe uko mbaali. "Mnakaanga Mbuyu kisha mnaachia wenye meno watafune".

  Huoni hata haya kushadidia fujo na vurugu za Chadema zilizopelekea watu kupoteza maisha kwa sababu tu ya uchu wa watu wachache kutaka madaraka? Madaraka na mabadiliko mnayoyshadidia muyapate na myalete kwa njia ya amani na si kwa kushadidia fujo.

  Nasema, kwa kura mlizopata kwenye uchaguzi uliopita. Mmeshaona kuwa hata ikipigwa tena kura na mpate 100% nyingine ya hizo, itakuwa bado hamkubaliki, jee, hicho ndicho kinachowafanya muanzishe fujo na vurugu?
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unashangaa nini? Kwani hujui nani aliyewaambia watu waandamane?
   
 16. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe huna tofauti na wale makada njaa ambao ukiangalia nyumba zao ka zinataka kudondoka, huku zikipepea bendeza za CCM huku wakiwa hawawezi ku-afford gasi (sasa hivi ni sh 70,000 badala ya 36,000), umeme ni issue kwao (nao umepanda bei) na bado hawaamini tatizo ni CCM. Mkisikia ngeleja akisema lazima Dowans walipwe mnapiga makofi, pambaf, bila kujua actually ni sisi ndo tunalipa ... kweli kiongozi hiyo post imetoka from moyoni au unataka uone tuta-react vipi?
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umasikini wa nchi hii, unajuwa chanzo chake ni nini. Au hujui?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huna hoja, ikiwa hoja ni Dowans, umekosa hoja.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Let me guess? Wagalatia na Nyerere..lol.
   
 20. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  You want me to mention chanzo kimoja cha umaskini? "No" it is not done that way sir especially in academics. Kuna vyanzo vingi vikiwemo uongozi mbovu, sababu za kihistoria, sera mbovu, rushwa, ufisadi nk

   
Loading...