Issue ya RC wa Dar imefanikiwa kuzimwa

Issue ya RC wa Dar imefanikiwa kuzimwa

Kuna nurse amepigwa Mvua Saba week tatu zilizokwisha.Pole kama husomi Magazeti.

Ya yule nurse imewezekana kushtakiwa na kufungua sababu hana Pesa,mnyonge.Vibarua tu.Lakini hawa wenye pesa zao na Wenye wa kuwabeba wanapata tu.

Kuna wengine wawili kesi zao zimepelekwa Mahakama kuu Arusha. Hao wanaoshtakiqa hawana wa kuwabeba.Ati tuna Tume ya Katiba,Sheria na Haki za Binadamu.

Binadamu kwa Tanzania ni Watawala tu,wengine ni viatu.
Huyu DAB ni mpiga dili ingawa tulisema kuwa wapiga dili wamedhibitiwa, kwanza ameweza kuwaweka mfukoni viongozi wenye mamlaka ya kumdhibiti mfano Necta, Utumishi, Polisi, Mwanasheria mkuu, Uaslama wa Taifa na mamlaka nyingine husika. Huyu ni kingpin wa wapiga dili kwani ameweza kupenya taratibu mpaka akafika hapo alipo kwa kunyenyekea bila kutambuliwa, ametumia madaraka aliyopewa kujipatia mali nyingi. Hii ni changamoto kwa serikali kwani viongozi wameshindwa kutoa ukweli juu yake ilhali wazazi wake wote wapo na majina yao yanajulikana. Tuna uongozi toka kaya kijijini, serikali za mtaa, tarafa na wilaya ambao wanatakiwa wajue kila mwananchi na rekodi zake hayo yote yameshindikana ila ametumia udhaifu wa system. Wanaofanya vetting wajue itafika mahali tutachagua watu ambao si wananchi. Kwa sasa ameweza ku control mpaka mamlaka za juu na hii ni hatari wekeni vyeti vyake mezani watu wajiridhishe.Wapiga dili wapo kila mmoja na staili yake!
 
Tatizo huyu haaminiki, ataachia vitu vingine sasa hiv.
 
Ni vigumu sana kuizima ishu ya Bashite, hii ishu kisiasa ni kama kansa, inakula mtaji wa Kisiasa wa mheshimiwa, imeondoa imani za watu, na operesheni zooote za vyeti feki sasa imeonekana kuwa kumbe ni kwa wanyonge lakini vigogo hawaguswi!.

Mheshimiwa akimbuke tu, kura zake ni asilimia 58 tu, zikishuka kwa asilimia 9 tu, baaasi Magogoni anaingia mtu mwingine!. Mwenzie JK mwaka 2010 zilishuka kwa asilimia 20, kutoka 80 mpaka 60, kwa hiyo hizo kura kupungua kwa asilimia 9 ni rahisi mno!.

Katika mazingira kama haya, kuwakumbatia watu waliokosa legitimacy mbele ya umma kama Bashite, mdogomdogo kunapunguza percentages za kuungwa mkono, kunaleta manung'uniko ya kimyakimya ndani ya chama, Wadau muhimu kama vyombo vya habari nao wanaweza kufanya bad publicity ktk muda muhimu watakaouchagua wao!, hii yote inaweza kupunguza zile asilimia 58
 
Kila kitu ni upepo tu!
Hata ishu ya NJAA sijui njaa imeisha au!
 
Yawezekana uamuzi wa kususa taarifa zake kwenye vyombo vya habari ndiyo sababu kubwa. Kwa mwasiasa hali kama hiyo si ya kupuuzwa
 
Watu ndo kwanza wameanza kutoa single we unasema issue imezimwa?

Unaishi dunia gani?
 
Hivi hakuna uchawi siku hizi...Bashite apigwe stroke mambo mengine yaendelee..nipeni jina la mama yake..kama Trump analogwa ..Bashite ni nani?
 
Kusahaulika kufoji cheti kwa Bashite ni pale namba za simu zitakapobadilika mwanzoni badala ya kutumia Zero ianzie 1
 
tunataka vyeti hakuna cha mchanga wa madini wala faru john.....mjadala wa faru john ulishafungwa na serikali..
"BASHITE AWEKE VYETI MEZANI ACHENI HIZO"
 
Inasahaulikaje wakati mtoa mada mwenyewe unakumbushia
 
Huyu DAB ni mpiga dili ingawa tulisema kuwa wapiga dili wamedhibitiwa, kwanza ameweza kuwaweka mfukoni viongozi wenye mamlaka ya kumdhibiti mfano Necta, Utumishi, Polisi, Mwanasheria mkuu, Uaslama wa Taifa na mamlaka nyingine husika. Huyu ni kingpin wa wapiga dili kwani ameweza kupenya taratibu mpaka akafika hapo alipo kwa kunyenyekea bila kutambuliwa, ametumia madaraka aliyopewa kujipatia mali nyingi. Hii ni changamoto kwa serikali kwani viongozi wameshindwa kutoa ukweli juu yake ilhali wazazi wake wote wapo na majina yao yanajulikana. Tuna uongozi toka kaya kijijini, serikali za mtaa, tarafa na wilaya ambao wanatakiwa wajue kila mwananchi na rekodi zake hayo yote yameshindikana ila ametumia udhaifu wa system. Wanaofanya vetting wajue itafika mahali tutachagua watu ambao si wananchi. Kwa sasa ameweza ku control mpaka mamlaka za juu na hii ni hatari wekeni vyeti vyake mezani watu wajiridhishe.Wapiga dili wapo kila mmoja na staili yake!

Wakija kushtuka GSM in own 90% ya Biashara za Tanzania na hivyo kucontrol uchumi wa TAIFA.
 
Option ziko nyingi sio lazima maandamano!! Hapo utampa sababu avunje watu miguu.....hapana tunataka kwa amani tu amtoe!!

Amtoe kwa kosa gani? Sababu nyie mnaandika iwe hivyo. Si aliwajibu anachosimamia au mnatakaje!? hata proof hamna hata wakusema mnayosingizia ni ya kweli.

Imetoka hiyo, I guess lingine linapikwa jikoni na litagonga ukuta tu kama kawaida.

Makonda oyeeeeee
 
Sio swala la kuandamana.Ni swala la kuhakikisha watanzania wote wanaelewa kwamba kuna mtu amefoji vyeti na anaendelea kufanya kazi katika Ofisi za Serikali kwa Kodi za Watanzania.
Ni swala la Kila Mtanzania kuelewa kwamba kuna waliofukuzwa na kushatakiwa na kufoji vyeti lakini Bashite hajaguswa.
Baada ya hapo watanzania watatoa uamuzi.

Proof ya uliyoandika juu ya Kiongozi jembe la Taifa rusha humu, usisahau kunitag.

Vinginevyo kaa uendelee kukosa usingizi na wenzako, mkiwa mmejaa wivu, tamaa na uvivu.
 
hahaha sio leo mkuu...labda wasikague tena vyet
 
Tunavuta tu pumzi hawajafanikiwa kuuzima.kwa takriban mwezi1 vidole gumba vilikuwa bize sana watu tumedili naye sana,ngoja vidole vipumzike tutalianzisha kwa kasi ya ajabu
 
Back
Top Bottom