Babati: Gurtu Sirro ahukumiwa miaka 20 jela kwa kuuza meno ya tembo

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Gurtu.png

Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Victor Kimario.

Kimario, akisoma hukumu hiyo ya uhujumu uchumi ya mwaka 2023, alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 17 katika Kijiji cha Matufa, wilayani Babati.

Alisema mshtakiwa alikutwa amebeba meno matatu ya tembo yenye uzito wa kilogramu 35 ambayo tham ani yake ni Sh. milioni 45.114.

Aidha, alisema shahidi namba tatu, nne na tano walimkuta mshtakiwa akiwa amebeba mzigo huo na shahidi wa tatu alijifanya mteja na kumnasa mshtakiwa.

“Nakutia hatiani pasipo kuacha shaka baada ya kujiridhisha kusikiliza upande wa mashtaka ambao umethibitisha kuwa ulikutwa na meno matatu ya tembo,” alisema Kimario.

Kimario alisema mshtakiwa alikiuka Sheria ya Wanyama pori kifungu cha 86(1)(2)(b) sura ya 283 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022, ikisomeka na aya ya 14 na kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Awali, Wakili wa Serikali, Rusticus Mahundi, akisaidiana na wakili mwenzake wa serikali, Abood Komanya, alidai kuwa mshtakiwa hana kumbukumbu za makosa ya nyuma kwa kuwa tembo ni wachache na ni kivutio cha utalii na watalii wanaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni na kutaka mahakama itoe adhabu stahiki ili iwe fundisho.

Mahundi, aliiomba mahakama irudishe nyara hizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wanyamapori ili itumiwe kwa usahihi.

Alipopewa nafasi ya kujitetea, Gurtu Sirro, alisema anategemewa na familia na ana watoto wanne ambao mama yao alishafanyiwa upasuaji mara nne hivyo hawezi kufanya kazi yoyote anamtegemea yeye, aliomba mahakama imwachie huru.


Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom