Israel yapiga inapotaka haimuogopi mtu na hakuna anayewalaumu

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,918
Katika miaka hii ya karibuni inaonekana taifa dhalimu la Israel limezidi kiburi chake, linapiga linapotaka bila kumuogopa yeyote na hakuna anayeilaumu kwa matendo yake haya isipokuwa wale wanaopigwa.

Imekuwa ni habari za kawaida kusikia imepiga hapa na pale Syria na hivi karibuni inakwenda mbali mpaka Iran na Lebanon. Kuna siku wamefika mpaka Libya na hata Urusi imewahi kuonja kipigo cha Israel pale ndege yake ya kijeshi ilipotunguliwa na kuuwa askari kadhaa takriban 50.

Kwa upande wa miji ya Palestina ikiwemo Gaza ndio kabisa wanapiga na hata kufanya kama sehemu za kujaribia silaha zake.

Kinachoshangaza ni kuwa hakuna kulaaniwa kwa wazi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na hata ikifanyika basi huwa ni kwa juu juu basi na hakuna natija inayopatikana kabla hawajarudia kupiga pale pale walipopiga mwanzo.

Jambo linalotisha na kusikitisha zaidi ni kuona mataifa ya kiarabu ambayo yana udugu wa karibu zaidi na Palestina pamoja na jeuri hiyo ya Israel yapo yanayorejesha uhusiano na Israel na kupuuza wazi wazi yale yanayotendwa na Israel kwa ndugu zao wakati huo huo wanapofanya makubaliano ya kurejesha uhusiano.
 
Hizo ndizo mbinu za kivita za Israel. Wanapiga halafu wanajikausha.Na mbinu nyengine ni kujifanya wanadiplomasia sana kwa kusaidiana na Marekani. Eti Marekani watu wanaumia kila kukicha lakini wao wanawafuata kimya kimya kuwataka wasahau kila kitu waikubali Israel.
 
Bangi kweli sio nzuri kabisa.siku Israel atakapotangaza vita na Urusi basi ujue ramani ya dunia itachorwa upya maana hakutakuna na nchi inayoitwa Israel.

Israel alitungua kimakosa ndege ya Warusi, ikabidi Netanyau fasta aende moscow kuomba msamaha kwa mkubwa Putin.
Usifananishe Urusi na vitu vya kijinga ndugu
 
Bangi kweli sio nzuri kabisa.siku Israel atakapotangaza vita na Urusi basi ujue ramani ya dunia itachorwa upya maana hakutakuna na nchi inayoitwa Israel.

Israel alitungua kimakosa ndege ya Warusi, ikabidi Netanyau fasta aende moscow kuomba msamaha kwa mkubwa Putin.
Usifananishe Urusi na vitu vya kijinga ndugu
Kama Israel baada ya kudungua ndege ya kivita ya Urusi ilikwenda kuomba radhi mbona haijaacha kupiga maeneo ya kijeshi kule Syria ambako Urusi ina watu wake wengi. Na Putin alimsamehe vipi na kwa madaraka gani mtu aliyeuwa askari wake wengi namna ile. Si angemshikisha adabu kidogo halafu ndio akamsamehe. Yote hayo ni kwa vile anayetenda makosa haya ni muisrael ambaye dunia imezugwa sana naye. Kama ingekuwa ni HezboLlaah dunia yote ingepata habari na kusingekuwa na msamaha na katika kulipiza kisasi mataifa kadhaa ya magharibi yangeshiriki.
 
Picha ziko wapi sasa??
Ndege ya Urusi Illussin Il-20 aina iliyotunguliwa na Israel
1599224314918.png

1599224205666.png
 
Back
Top Bottom