ISRAEL v/s IRAN.

ISRAEL v/s IRAN.

Status
Not open for further replies.
Mkubwa take your time kusoma historia ya Iran kianzia mapinduzi ya 1979 then vita ya Iran na Iraq. Vile vile inaonekana hujui kuwa wa Iran sio waarabu. Swali jingine, unajua kilichowakuta waisrael kwenye ile vita na Hizbolah Lebanon? Try to find out from neutral sourses kwa nini walisitisha their ground invasion.
Washia sio waarabu?
Uanaweza ukaniambia wakina nani nyuma katika vita ya miaka8 Kati ya Iraq na Iran?
Ungeweka wazi wewe kwanza kile Israel ilichokipata kwa Hizbolah kule Lebanoni!
Labda nikuulize unafahamu Lebanon ilipata athali gani kutokana na Ile vita?
Lengo na Israel la kwanza katika ile vita ilikua ni kumuokoa Yule Askari wa kiisrael alietekwa akiwa doria baada ya kushambuliwa na Hizbolah. Katika Hilo waisrael walifeli!
Lengo la pili lilikua ni kuwaamisha Hizbolah maeneo ya mpakani mwa Lebanon na Israel na kusambaratisha harakati za kivita dhidi ya Israel na kwa hili Israel walishinda vizuri na Kama ni mfatiliaji mzuri unaweza ukaona hakuna tena urushwaji wa maroketi kuelekea upande wa Israel.
Yale maeneo ambayo Hizbolah waliokua wanakaa kabla ya Ile vita hawawezi tena kurudi na kukaa kwa Zaidi ya miaka30. Kumetegwa mabomu ardhini ndani ya Lebanon km50 kutoka mpakani mwa Israel Na Lebanon na shuguli ya kuyategua hayo mabomu itachukua Zaidi ya miaka hiyo! Na Hizbolah kwa Sasa kutokana na kusukumwa ndani Zaidi hawana tena silaha za kuweza kurushwa na kufika ndani kabisa ya Israel! Na ndio Maana hatuoni tena haya maroketi! Labda wajipange tena na Pia ule mpaka wa Lebanon unalindwa usiku na mchana na una fensi na Askari na vifaa vya tecnology ya Hali ya juu.
Israel Ina jeshi bora kabisa tena lenye uzoefu mkubwa na vifaa vya kijeshi vya kisasa kabisa na vya technology ya Hali ya juu kabisa kwa majeshi yake yote! Ya angani na majini na nchi kavu!
National military service: hii waisrael wote lazima wapitie wakimaliza kusoma shule na vyuo kabla ya kuajiriwa na kufanya kazi. Ni mlemavu tu na taahira wa aikili ndio hawapitii hii kitu na ndio Maana linapotokea shambulio lolote, waisrael wanafahamu kujiokoa na wapi wakimbilie. Kwakifupi waisrael karibu wote ni maaskari.
Ramani ya vita tu Bado haijakaa vizuri Kwani Siku zote Marekani na Israel wanapopigana vita hawataki kabisa mazara ya vita yawaguse Raia wao! Na Siku wakikamilisha Ramani ya vita vizuri basi Iran itashambuliwa kwa nguvu sana na itajibu hayo mashambulizi kwa asilimia ndogo sana!
 
Mkuu yaelekea Hukuwaelewa wa Israel............
.................Kwa taarifa TU Siasa za mashariki ya kati ni MGUMU SAANA Tambua hata IRAN kwa sasa inaivuruga saana Mashariki ya kati....hata WaSaudia wanawashawishi waisrael wanataka waitandike IRAN refer WIKLeak........................

Back to the topic..........NETANYAHU jana alikuwa anaongea kwa fact...alikuwa hutumii lugha ya siasa Hata kidogo....alikuwa anatoa ushahidi.......na ndio kila mara alikuwa ananukuu.....na mpaka anaongea tambua wanaushahidi wote....ni juzi walimkamata MUIRAN na picha za ubalozi wa Marekani ....na kwa taarifa za kijasusi alikuwa anapanga shambulizi.....Mpaka wakuambie wanataka kushambulia TAMBUA wameshajiandaa........hawa jamaa kumbua wako vitani KILA SIKU.....na usibeze umahiri wao hata kidogo ktk vita.......hawababaishi......tambua hata ndani ya IRANI wana operatives wao......kama ni mfuatiliaji wa mambo....ni miezi tu imepita walikuwa na program ya kuwaua wanasayansi wanaohusika na nuclear program ndani ya IRAN.......Nahata mpaka jamaa anaongea jana ndani ya UN kumbuka ni VITA.....KUMBUKA IRAN Wanakusudia kuifuta Israel ndani ya ramani ya DUNIA......na Waisrael kwa akili zao..maarifa ..na ujasiri hawatakubali litokee......Hitler aliwapa somo la kutosha..........

Wakumbuka mwaka jana alisema nini?? na hata ktk hotuba yake ya jana alikumbushia aliyoyasema mwaka jana.........kwa kifupi.....hata wamarekani wanawagwaya Waisrael......na bila Israel, Marekani hakuna kitu......


Kwa Mwenye kupenda kuelewa na kukubali basi anaweza akakubali haya ulioandika Mkuu!
Hiyo ndo israel mbambe wa mashariki ya Kati na mataifa ya kiarabu!
 
Nafikiri hulijui taifa la israeli, ki ukweli israel inaweza pigana na taifa lolote lile duniani bila ya msaada wowote kutoka kwa taifa lolote lile. Israel ni taifa teule na ni taifa la mungu

Taifa teule maana yake nini?? Na hata kama ni teule ndio lipige mataifa mengine???
 
Kwa Mwenye kupenda kuelewa na kukubali basi anaweza akakubali haya ulioandika Mkuu!
Hiyo ndo israel mbambe wa mashariki ya Kati na mataifa ya kiarabu!
hizbollah bado wako pale boarder na juzikati hapa wameweka biliboard kubwa pale mpakani linasomeka .WE ARE COMING.,wamewaandikia waislael.
 
Iran ana technolojia kubwa sana sanaa,, wala sio mambo ya ushabiki, yeye mwenyewe anaweza hata kudaka drone ya MAREKANI na kuishusha chini sasa ukiongelea Iran usifikirie ni Nchi ndogo kijeshi,,ndio maana hawa Israel wako makini, mbona wanapiga Syria wakijisikia tu kwanini hawapigo Iran, wanajua Iran sio lelemama...
 
Mkuu yaliyo tokea mwaka 1967 hayawezi kujitokeza tena, na Netanyahu akiendeleza ufedhuli wake wa kumdharau Baraka Obama na kutaka kuvuruga mazungumzo ya amani baina ya Merikani na IRAN kwa kutoa visingizio kibao kuhusu IRAN, basi ajue atajimaliza mwenyewe kisiasa na wala hana njia ya kujua vita itakwishaje kama akivianzisha! Netanyahu hasitegemee kwamba Merikani inaweza kutoa misaada kwa mtu ambaye ni jeuri na mpenda vita kama nini, akianzisha vita vya kijinga Mashariki ya kati atapata wakati mgumu sana. Netanyahu ni kiongozi erratic sana - atafakali mambo kwa kina unlike waziri wake wa ulizi Eliud Barak mwenye busara na maona mbali, bila ya Eliud Barak kuwepo kwenye baraza la mawaziri nchini Israel saa hizi Netanyahu ange piga mabomu IRAN na Syria bila ya kujali mtu yeyote, anacho sahau ni kwamba Iran sio Lebanon au Gaza, ajifunze kuishi na majirani zake kwa amani ahache kupora aridhi ya Waarabu na kuheshimu haki za binadamu wenzake, dunia itaendelea kupigana vita on behalf ya Waisrael mpaka lini?

Mkuu umetoka nje kidogo nadhani Kwa hakina israel sio mchokozi bali majirani zake ndio wachokozi usiwe kama mtu anayeshabikia tu.... fuatilia habari zinavyokwenda na vita zote alizopigana Israel kachokozwa.... au una lingine? Netanyau ndio kila siku anacholalamika wapelelezi wake wanaona kila kinachopangwa na majirani zake na ushahidi huwa anatoa au huwa hamuelewi lugha? mweleweshe vizuri watu....

Tusiwe kama watu wanaoongea maredioni kuwa hii ni nchi ya amani na tusikubali kuwasikiliza watu wanaotaka kutuondolea amani... wakati wale wanaosababisha hali mbaya ambayo inaweza kuharibu amani wananyamaziwa kimya
 
Kwa hali ilivyo kwa sasa hivi Israel haiwezi kuipiga Iran peke yake vivyo hivyo na Iran haiwezi kuipiga Israel peke yake kwa Dunia ya leo haiwezekani ukajitosheleza kwa kila kitu lazima uitegemee nchi nyingine ili uweze kupata ushindi katika kila vita,Hata Marekani hawezi kuipiga nchi yoyote bila kutaka suport kutoka nchi zingine,hata alipotaka kuipiga Syria Marekani ilitaka na ilitafuta washirika wa kuweza kusaidia aidha kwa technology au ardhi ambayo anaweza kufanya kama kambi.
Harafu kuna kitu lazima watu wajue kuwa kuna mambo mengine huwezi kuyatenganisha hata iweje mfano hata siku moja Israel na Marekani hawezi wakaachana katika jambo kubwa kama la vita hata kama hajatangaza utakuwa anasaidia kwa njia moja au nyingine vivyo hivyo na Marekani maana nchi hizi kutokana na Historia wanategemeana kwa nyanja zote,na huu ndiyo ukweli Marekani haiwezi kuishambulia Irani bila ya kuipa taarifa kwanza Israel vivyo hivyo na Israel haiwezi kuishambulia Iran bila kuipa taarifa ya mapema Marekani
 
Mkuu israeli sio mbwa wa marekani lile nitaifa teule marekani watu wenyemamlaka makubwa watu wanao amua rais wa marekani awe nani ni wayahudu from Israel makapuni makubwa ya marekani,tasisi nyeti kama nasa n.k vinaongozwa na wayahudi,wale watu wamebarikiwa na sir GOD. Ndio watu wenye uwezo mkubwa xana wa kufikiri chini ya jua marekani analitambua hilo ndio maana yuko karibu yao sana anajua bila wao si kitu kabsaaaaaa!
 
hizbollah bado wako pale boarder na juzikati hapa wameweka biliboard kubwa pale mpakani linasomeka .WE ARE COMING.,wamewaandikia waislael.

Unaweza ukaweka Bango lakini si kufanya harakati zako katika maeneo hayo! Ifaamike kwamba Hizbolah ni kikundi tu kidogo ambacho hakina wanamgambo Zaidi ya 1o elufu pamoja na kua Iran Yuko nyuma ya Hizbolah lakin kwa miaka ya hivi karibuni kimedhoofika na ndio Maana Hilo bango Lao lasomeka We are coming. Wanajipanga tu na mikwara Yao mingi lakini Muisrael Yuko pale Tayari na kwa lolote na mtu yeyote! Ukitaka kujua mtafute Askari yeyote Yule wa Tanzania aliewahi kwenda kuhudumu chini ya umoja wa mataifa Lebanon akupe habari za Hawa Israel!
Hizbolah pamoja na Kiongozi wao wanaijua mziki wa Israel.
 
Iran ana technolojia kubwa sana sanaa,, wala sio mambo ya ushabiki, yeye mwenyewe anaweza hata kudaka drone ya MAREKANI na kuishusha chini sasa ukiongelea Iran usifikirie ni Nchi ndogo kijeshi,,ndio maana hawa Israel wako makini, mbona wanapiga Syria wakijisikia tu kwanini hawapigo Iran, wanajua Iran sio lelemama...


Kudaka Drone haina Maana Yuko juu kitechnology. Ukiwa na rada kubwa unaziona drone! Swali ni kwamba huo mfumo wa anga wa Iran unaweza kuzuia mashambulizi ya anga ya kutosha?
Mfano kule Afghanistan mwanzo wa vita walipelekewa mashambulizi ya anga 700 ndani ya masaa24 kwa muda wa wiki nzima!
Sasa piga hesabu mwenyewe chukua hiyo idadi ya mashambulizi 700 ugawe kwa masaa24 na mikoa au majimbo then uzididhe mara wiki nzima!
Yani wakishaanza hivo wanahakikisha nchi na mfumo wote wa anga na mawasiliano na Umeme na mabarabara Na ata Maji viko nyang'anyang'a ndio wanaanza kuvinjari Na Drone zao na Askari wa miguu! Na hivi ndio Israel ilimfanyia Lebanon huo Mwaka wa 2006 dhidi ya Hizbolah.
Kwahiyo tusidanganyane tu hapa! Israel na Marekani wana uwezo mkubwa sana wa kijeshi hapa duniani! Na Iran kwa Israel haiwezi kusimama.
Tujikumbushe kile kisa cha Askari wa majini wale 14 wa Ungereza waliotekwa na maaskari wa Iran baada ya kuvuka mpaka na kuingia katika eneo la Iran mwaka2007. Ni nini mataifa ya kiarabu yalimshauri aliekua rais wa Iran muda ule juu ya kadhia ile na mpango wake wa nyuklia?
 
Nafikiri hulijui taifa la israeli, ki ukweli israel inaweza pigana na taifa lolote lile duniani bila ya msaada wowote kutoka kwa taifa lolote lile. Israel ni taifa teule na ni taifa la mungu

taifa teule maana yake nn na taifa la mungu maana yake nn mbona unajichanganya,who iz mungu?
 
what makes you think this is possible?

Mkuu Hekimatele, hoja yangu imetokana na mtazamo wangu kuhusu hizi nchi mbili based on their geographical location, size, population na war strategy. Iran ina ukubwa wa 1,648 km2 na Popn. ya takribani watu Miliono 80. Israel in ukubwa wa 20, 770 km2 na Popn. ya watu milioni 8. Kwa akili ya kawaida nadhani unaweza kuona kwamba, kivita, hizi nchi mbili haziwiani hata kidogo.

Ukiangalia ramani hapo chini, utaona kwamba kutoka Israel mpaka Teheran, kuna umbali wa takriban kilometa 1500. Ili Israel aishambulia Iran na kutoa pigo takatifu, inabidi ndege zake zicross anga ya nchi kama 4, ambazo zote ni za Kiarabu. Sidhani kwamba hili ni jambo rahisi.

Technologically, Israel hana ndege za kivita zinazoweza kwenda km 1500 kupiga target (na kutoa pigotakatifu in order to destroy Iranians Nuclear facilities). Mwenye hizo ndege za ku refill ndege juu kwa juu ni Marekani, na mbaye kwa sasa hivi hayupo tayari kuanzisha vita nyingine ndani ya Ghuba ya Uajemi. Anajitayarisha kuondoka Iraq na Afghanistan.

On June 7th, 1981, Israel destroyed Iraq's Osirak Nuclear Plant, shambulio ambalo liliungwa mkono na Iran, ambaye alikuwa adui mkubwa wa Iraq kipindi hicho. Lakini shambulio hilo ndilo lilomfungua macho Iran. Sasa hivi Iranian Nuclear plants zote zipo Underground and scattered kiasi kwamba ni vigumu kwa Israel, peke yake kushambulia successfully six targets at once. Uncle Sam assistance is necessary, kama ikibidi kufanya hivyo, tena sana tu.

Most likely, shambulio lolote la Israel kwa Iran litazaa vita kati ya hawa wababe wawili. Na hapa tena Uncle Sam lazima aweke kifua. Maana yake ni kwamba, kwenye strategy za kivita, hauwezi kuziweka hizi nchi mbili kwenye ulingo moja. Its unrealistic. Kama Saddam Hussein angekuwa hai angetoa ushuhuda.

Vita vya Iraq/Iran vilichukua miaka karibia 8. Na pamoja na misaada aliyopata Iraq kutoka kwa U.S.A, Britain, Germany na France lakini Iraq alishindwa kuwin ile vita. Ni kama nilivyosema hapo mwanzo, size na population ni moja ya vigezo muhimu kwenye vita (TAFADHALI TUSIANGALIE CONGO).

Kwa sababu ya popn. size ya Iran (WATU MILIONI 80), kupoteza raia million kadha kwenye vita kwao sio big deal. Pengine hata kwa Israel itakuwa sio big deal, hosusani inapokuja kwenye suala la UTAIFA NA KUILINDA NCHI YAO.

Huu ni mtizamo wangu tu. Inawezekana nikawa wrong kwenye assessment zangu. Lakini kila ninapoangalia kasheshe ya Ghuba ya Uajemi, huwa nabaki mdomo wazi.



IRAN-and-its-neighbors.jpg
 
Mkubwa take your time kusoma historia ya Iran kianzia mapinduzi ya 1979 then vita ya Iran na Iraq. Vile vile inaonekana hujui kuwa wa Iran sio waarabu. Swali jingine, unajua kilichowakuta waisrael kwenye ile vita na Hizbolah Lebanon? Try to find out from neutral sourses kwa nini walisitisha their ground invasion.

Mkuu Israel hawasitisha (retreat) walimaliza vita kabisa (total withdrawal) baada ya jeshi la ardhini kupata kichapo cha karne kisha makomandoo wao wengi sana kuuliwa na barobaro wa Hizbullah. Halafu eti wanawezapigana na Iran wenyewe. Wajaribu waone. Hizbullah halikuwa jeshi la taifa ni militants lakini imewaamgamuza Israel mpaka jeshi la UN lilipelekwa kuweka buffer pale ili Hizbullah wasiichokoze tena Israel. Na kwa taarifa tu Israel ilitumia silaha za phosphorus ambazo haziruhusiwi kwa mujibu wa sheria za silaha za UN
 
Mkubwa take your time kusoma historia ya Iran kianzia mapinduzi ya 1979 then vita ya Iran na Iraq. Vile vile inaonekana hujui kuwa wa Iran sio waarabu. Swali jingine, unajua kilichowakuta waisrael kwenye ile vita na Hizbolah Lebanon? Try to find out from neutral sourses kwa nini walisitisha their ground invasion.

Aisee afathali umejaribu kumpa hints huyo muumini wa Israel..
 
Nafikiri hulijui taifa la israeli, ki ukweli israel inaweza pigana na taifa lolote lile duniani bila ya msaada wowote kutoka kwa taifa lolote lile. Israel ni taifa teule na ni taifa la mungu

Si na ndio hao hao walimkataa kuwa Yesu si Mungu?

Vipi tena awateue kuwa "taifa teule na ni taifa la mungu"?
 
Isoliwaya naweye pia huijui au umejib kiushabiki lakin vuta kumbukumbu kias cha mwaka mmoja au miwili walipopigana na Hizbullah alifanywa nin Izrail mpk UN ikaingilia kati,Iran labda nikwambie aliwambia ni nin Usa walipotaka kuivamia Siriya kabla ht Rashia hajamstopisha Usa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom