Mkuu, unachanganya sana historia.
Wafilisti ndio hao Wapelestina, wapalestina ni Waarabu wa kale sana miongoni mwa Waarabu na walikuwepo kabla hata ya ujio wa waarabu wa Saudia, waarabu wa Saudia ndio uzao wa Ismail Mwana wa Ibrahimu kwa maneno Mengine Sio Waarabu wote ni uzao wa Nabii Ibrahimu au unaweza kusema kwamba kabla ya Nabii Ibrahimu "Bara arabu" tayari kulikuwepo na Makabila ya Waarabu miongoni mwao ndio hao Wafilisti (Wapalestina).
Nabii Musa (as) aliamrishwa na Mungu awaokoe Wana Wa Israeli kutoka Misri na awaingize hapo Palestine ambamo alitakiwa awapige hao Wafilisti ili achukue udhibiti wa hiyo nchi kwani wao Waisreali kuingia hapo isingekuwa jambo rahisi bila kupigana na utawala wa Wafilisti katika zama zile ingawa Musa as alishindwa kuwashawishi Waisraeli kupigana lakini baadaye baada ya miaka 40 kizazi kipya cha Waisraeli chini ya (Joshua??) Waliweza kuingia na kuwapiga Wafilisti (Wapalestina) na kuchukua mamlaka ya nchi hiyo, katika zama hizo kukawa na Makabila matatu makuu yaliyokuwa yakiishi katika eneo hilo; Wafilisti (Wapalestina walionyanganywa mamlaka), Waisraeli na Makabila mengine ya Waarabu kama Mabedui (Bedouins) hawa Wapalestina ndio waliokuwa wakiitwa Wasamaria (Samaritans) katika Biblia.
Zama Yesu alipotokea hapo Palestine kulikuwepo na Makabila mawili tu kati ya Makabila 12 ya Waisreali makabila hayo ni Judea na Benjamin makabila 10 yalikuwa yametawanyika sehemu.mbalimbali duniani mfano Ulaya, India, Afghanistan, Bara Arabu yote, Iran nk, na haya makabila yalikuwa yamechukuliwa utumwani na mfalme Nebuchadnezzar wa Babylon na alipowaacha huru kutoka utumwani ndipo hawakurudi Palestine wakaamua kutawanyika katika sehemu mbalimbali za dunia.
Yale makabila mawili yaliyobaki ya Waisraeli yaliyobaki Palestina yakamezwa na Makabila ya Waarabu yaliyokuwepo wakati huo na identification yao ikafutika baada ya miaka 2000 na ushee kupita ndiyo maana mwaka 1948 umoja wa mataifa kwa kuwaonea huruma Waisreali baada ya kuuwa sana na Wazungu wa ulaya na hasa Nazi ya Hitler ikaona ili kuwafariji itabidi watafutiwe nchi ya kuishi, option zilikuwa; Argentina , Uganda, Canada, Marekani na Palestine kipindi hicho Palestine ilikuwa inatawaliwa na Waingereza na James Balfour Muingereza ndiye aliyepeleka UNO azimio la kuanzishwa taifa la Israel --- Wakafanya ujanja kutokuipa Uhuru nchi ya Palestine na hapo hapo kumega kipande cha nchi hiyo na kuanzisha taifa la Israeli ili hapo baadaye Israeli iimeze Palestine yote kitu ambacho Israeli leo ndicho anachofanya.