Israel imekamilisha ujenzi wa barabara Gaza

Papasa

JF-Expert Member
Nov 2, 2018
1,948
4,133
Jeshi la Israel limekamilisha ujenzi wa barabara mpya inayopita katitaki ya eneo la kaskazini mwa Gaza kutoka mashariki hadi magharibi mwa eneo hilo. Haya ni kwa mujibu wa picha za satelaiti zilizodhibitishwa na kitengo cha uchunguzi cha BBC verify.

Jeshi hilo limeiambia BBC kuwa linajaribu kuhakikisha kwamba linapata udhibiti wa eneo husika na kuwawezesha wanajeshi wake kusafiri kwa magari na silaha zao katika eneo hilo kwa usalama na bila changamoto.

Lakini baadhi ya wataalamu wanahofu kwamba huenda barabara hiyo ikatumika kama kizingiti cha kuwazuia wapalestina kutorejea katika makazi yao kaskazini mwa Gaza.

Wengine wanasema kwamba inaonekana kuwa nisehemu ya mipango ya Israel ya kuendelea kuwa ndani ya Gaza, hata baada ya vita vinavyoendelea kukamilika.

Mnamo Februari mwaka huu, Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alizindua ruwaza ya baada ya vita ambayo inaonyesha jinsi Israel inanavyoweza kuchukua jukumu la kusimamia ukanda wa Gaza kwa muda usiojulikana.

Viongozi wa kimataifa wameionya Israel dhidi ya kufanya mipango ya kikamilifu itakayo wapotezea makao Wapalestina au kupunguza eneo la ardhi ya Ukanda huo wa Gaza.

Ni kipi tunachokifahamu kuhusu barabara hii?

  • Inapita katikati kati ya eneo la kaskazini la Gaza, na kuwa kati kati ya eneo la kaskazini lililoko juu yake na la kusini lililoko chini yake.
  • Inaanzia kwenye mpaka wa Gaza na Israel karibu na mji wa Nahal oz Kibbutz na kumalizikia karibu na bahari.
  • Inaungana na barabara za salah al din na ile ya nahal oz Kibbutz, ambazo ni barabara mbiili kubwa zinazotumika katika eneo hilo kuu.
Picha za Satelaiti ambazo zimefanyiwa uchunguzi na utafiti wa kina na BBC, zimeonyesha kwamba jeshi la Israel limejenga barabara mpya yenye umbali wa kilomita zaidi ya tano ya maeneo mapya ya barabara ili kuuunganisha barabara zingine ambazo hazikuwa zimeshikana.
Screenshot_20240311-064439_1.jpg
 
Tayali bunge lao limeidhinisha ujenzi kwenye maeneo ndani ya Gaza ambako umoja wa mataifa uliwakataza kujenga kwa muda mrefu sana
Yap! Hiyo ni sehemu ya malipo kwa gharama ya vita. Haileti maana, eti walisafishe eneo hilo kwa kuwaondoa magaidi kwa gharama ya kodi za Waisraeli halafu mambo yaishe/iishie hivi-hivi tu. Hiyo sio sadaka. Lazima malipo yawepo na kwa kuwa Wapalestina hawana uwezo wa kulipa, basi Israeli atajiongeza na Kujilipa mwenyewe.
 
Kabisa, Wapalestina wanaporwa tena ardhi yao na dunia imebakia kimya.
Sikubaliani hapo. Wapalestina hawajaporwa ardhi yao hata kidogo ila wameiuza wenyewe kwa hiari yao asubuhi ya tar.07 Okt. 2023 (na ushahidi upo) kwa sababu wanazozijua wenyewe. :D Dunia iliwapa uhiari wa kuchagua, na walichagua fungu walilolitaka wenyewe ndo mana dunia imekaa kimya ili Wapalestina wakiongozwa na HAMAS, walinywe kama walivyoligema.
 
Back
Top Bottom