GAZA: Majeshi ya Israel yameiteka barabara kuu inayougawa mji wa Gaza Vipande vya Kusini na Kaskazini

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,769
Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye vifaru wameiteka barabara kuu inayounganisha GAZA kusini na GAZA kaskazini. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba jambo hilo litaifanya Israel kuugawa mji wa GAZA katika kipande cha Kusini na Kaskazini. Israel imevamia mji wa Gaza Kupitia Kaskazini ambapo raia wote wa Gaza waliamuliwa kuhamia upande wa Kusini ambao unapakana na Misri.

Wiki mbili zilizopita, Majeshi ya Israel yaliwataka raia wote waishio upande wa Kaskazini mwa GAZA kuhamia kusini kwa ajili ya usalama wao. Upande wa Kaskazini mwa Gaza ndio mji mkuu wa GAZA unapatikana. Amri hiyo ya Israel iliwalazimu Wapalestina zaidi ya Laki 6 kutii onyo hilo la kuhamia kusini licha ya Wapiganaji wa HAMAS kuwataka raia hao kupuuza agizo hilo.

Video kadhaa zinaonesha vifaru vya Israel vikishambulia magari ya Kiraia ambayo yalikiuka agizo la kuondoka, zaidi ya watu 28 wamekufa baada ya Kifaru kufyatua makombora kuelekea kwenye magari ya Kiraia ambayo yalikuwa yanataka kupita kwenye barabara hiyo kuelekea kusini.

Jeshi la Israel, IDF kupitia msemaji wake limewapa masaa 24 raia waliopo ndani ya mji mkuu wa GAZA kuondoka kabla ya Oparesheni kabambe ya kuusafisha mji huo na kuwasaka Mateka wa Israel. Wapiganaji wa HAMAS walipambana na wanajeshi wa Israel kabla ya kutelekeza Silaha zao na kukimbia.

Heavy clashes reported as Israeli armoured vehicles cut Salah al-Din Street in the middle of the Gaza City governorate. Heavy clashes as Israeli tanks briefly reach Gaza City outskirts
 
Naona majeshi ya wayahudi feki wa kizungu wamezamilia kuweka blocked gaza kwa mda mrefu ili waweze kuwafagia Hamas, ngoja tuone mwisho wa hii vita itakuaje maana sidhani Kama gaza itarudi chini ya umiliki wa wapalestina wakiongozwa na Hamas Tena.
 
Naona majeshi ya wayahudi feki wa kizungu wamezamilia kuweka blocked gaza kwa mda mrefu ili waweze kuwafagia Hamas, ngoja tuone mwisho wa hii vita itakuaje maana sidhani Kama gaza itarudi chini ya umiliki wa wapalestina wakiongozwa na Hamas Tena.
Waisrael wameshatimuliwa halo salah din,walipachukua kwa misseusiozidi saa moja
 
Naona majeshi ya wayahudi feki wa kizungu wamezamilia kuweka blocked gaza kwa mda mrefu ili waweze kuwafagia Hamas, ngoja tuone mwisho wa hii vita itakuaje maana sidhani Kama gaza itarudi chini ya umiliki wa wapalestina wakiongozwa na Hamas Tena.
Netanyahu alieleza wazi kuwa, baada ya hii vita, Gaza itakuwa na sura tofauti. Zaidi Israeli ilisema, ili kumwadhibu mwarabu, mchukulie ardhi ndio huelewa somo.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Nimeona gari likipigwa na kifaru wakati linageuza baada ya kuona kifaru,sijaona gari lililokaidi kuondoka bdo likapigwa
Hamas wanatumia magari ya kiraia na pikipiki kusafirisha anti tank teams zao. Israel imetoa nafasi ya kuondoka mapema akitokea mtu yeyote njiani haaminiki kama ni raia kweli. Si umeona waliokuwa wanarekodi kwenye ile video walitoa gari kwa kasi baada ya shell kufyatuliwa pale Salah Al Deen road
20231030_173951.jpg


Na usiku Israel imebomoa geti la kuingia kambi ya Jenin uko West Bank
20231030_174018.jpg


Na Jordan imeiomba Marekani ipeleke air defense systems kulinda anga lake. Na jana Marekani imefanya flights za ndege za mizigo kama 30 hivi.

Mambo yanaenda yanabadilika taratibu
 
Back
Top Bottom