Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,555
Nimetokea kumfahamu Jussa kwa karibu, huyu ni hazina kubwa kwa CUF, kama alivyo Zitto ni hazina Chadema, au January ni hazina CCM, hawa ni kizazi cha wanasiasa wa .com. Kielimu Jussa ni mwanasheria hivyo sio kilaza!.Kitendo cha Naibu katibu mkuu wa CuF kulalamikia matokeo ya kidato cha nne eti wanzanzibari wanabaguliwa kwa kuwa katika shule kumi bora ya Zanzibar ni moja tu (Lumumba sekondari) na eti shule nyingi zilizofutiwa matokeo ni za kutoka Zanzibar pia. Mimi natilia shaka uwezo wake wa kufikiri pamoja na kiwango chake cha elimu kwani sidhani kama NECTA huwa wanasahihisha mitihani kwa kuangalia unatoka upande gani wa muungano. Mimi nashauri kama anaona hawakutendewa haki awashauri wanafunzi wakate rufaa NECTA mitihani yao irudiwe kusahihishwa badala ya kuingiza siasa kwenye suala nyeti kama hilo. Nawasilisha
(Source: Nipashe Radio one)
Kwa historia ya Zanzibar na siasa za Zanzibar, wanaopinga muungano ni wengi kuliko mnavyowadhania, hata huyu Makamo wetu wa Rais, Dr. Bilal, ndie alikuwa timu ya Comandoo kutaka kubadili katiba ya Zanzibar Komandoo agombee tena, Bara ikikataa, wauvunjilie mbali muungano!. TISS wakastukia hiyo deal na kumshughulikia ipasavyo Komandoo na watu wake, wote wakatupwa nje!. Leo makamo rais anapohubiri muungano ni unafiki mtupu, wanaowajua Wanzanzibari tunawajua!.
Jussa ni bold kama Zitto na Januari, sio mnafiki, watu hawapendi kusikia ukweli mchungu!, kama Tanzania na Zanzibar zina haki sawa ndani ya muungano, iweje Zanzibar kila siku inanyanyasika kielimu?!. Anachopigania Jussa ni haki sawa kwenye mtihani wa kidato cha nne!. Kama Nyerere aliweza kulazimisha jamii zilizoachwa nyuma kielimu, zilishushiwa pass mark ili watoto wa jamii hizo waingie sekondari, kuna ubaya gani kufanya affimative action kwa Wanzanzibari ili nao wajiunge vyuo vikuu kama UD, kuliko kuendelea kunyanyasika!.
Its a fact watu wa Kanda ya Kaskazini, Ziwa na Kusini Mashariki, (Mbeya na Iringa), wako sharp upstairs kuliko Kanda ya Kati, Mashariki na Kusini!. Hii inamaanisha wengi wanaofanya vizuri hapa jijini, sio watu wa asili, Wazaramo, Wandenge, Wakware etc, wasipofanyiwa any affimative action, they will be reduced to beggers!.
Wazanzibari ni hivyo hivyo na ndicho anachokipigania Jussa!.