Islam teachings has nothing to do with terrorism

Status
Not open for further replies.
Asante kwa majibu, nakuweka kwa red kwa majibu yangu:

Kwa lengo langu elimishi nililo kusudia; Ni kweli kabisa bendera nyeusi ya uislamu inapepea na si ubalozi wa us tunisia bali dunia nzima inashangaa na hiyo kero!
Sina uhakika kama unafuata habari za uwogo au unajaribu kuepukana na jibu. Lakini nilivyokuambia: hakuna bendera nyeusi juu ya ubalizo wa Marekani Tunis (jinsi ulivyotangaza) wala haikuwepo (ila kwa dakika chache juu ya ukuta wa ubalozi)

Hayo ni mafunuo ya allah kwa kipenzi chake muhammad ili waumini wayatekeleze! usipoyatekeleza, usijipe moyo kwamba nawe ni muumini bali ni kaafir tu!
Hii ilikuwa kuhusu ayat Q9:29 lakini bado hujasema ni nini unayoelewa kama amri kwa Waislamu. Wafanye nini kwa ufahamu wangu??
Na hii -jinsi unavyoelewa- inatekelezwa wapi duniani?

Hao wachache ndio waislamu na bila shaka wamepata thawabu kwa allah! Hao wengi dhamira tu iliyowasukuma, lakini siku za baadaye inshaallah nao watakuwa waumini!
Unachukua wapi kipimo kusema wale wahalifu waliomwua mbalozi walikuwa Waislamu wa kweli na unajuaje walipata thawabu?? Kwa nini hupendi kuwaamini hao wengi waliowafukuza kuwa hao ni waislamu?

Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu???
 
Asante kwa majibu, nakuweka kwa red kwa majibu yangu:Kwa lengo langu elimishi nililo kusudia; Ni kweli kabisa bendera nyeusi ya uislamu inapepea na si ubalozi wa us tunisia bali dunia nzima inashangaa na hiyo kero!Sina uhakika kama unafuata habari za uwogo au unajaribu kuepukana na jibu. Lakini nilivyokuambia: hakuna bendera nyeusi juu ya ubalizo wa Marekani Tunis (jinsi ulivyotangaza) wala haikuwepo (ila kwa dakika chache juu ya ukuta wa ubalozi)Hayo ni mafunuo ya allah kwa kipenzi chake muhammad ili waumini wayatekeleze! usipoyatekeleza, usijipe moyo kwamba nawe ni muumini bali ni kaafir tu!Hii ilikuwa kuhusu ayat Q9:29 lakini bado hujasema ni nini unayoelewa kama amri kwa Waislamu. Wafanye nini kwa ufahamu wangu??Na hii -jinsi unavyoelewa- inatekelezwa wapi duniani?Hao wachache ndio waislamu na bila shaka wamepata thawabu kwa allah! Hao wengi dhamira tu iliyowasukuma, lakini siku za baadaye inshaallah nao watakuwa waumini!Unachukua wapi kipimo kusema wale wahalifu waliomwua mbalozi walikuwa Waislamu wa kweli na unajuaje walipata thawabu?? Kwa nini hupendi kuwaamini hao wengi waliowafukuza kuwa hao ni waislamu? Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu???
Mkuu habari ndio hiyo na kama huamini basi subiri waumini wa uislamu wakuaminishe! Uislamu usingekuwepo bila Ukristo kuwepo! Habari njema ilipapaswa kwao, toka mfalme Nagus wa ethiopia hadi hivi sasa! Mkuu aya iko bayana na wale walio waamini,WAAMINI! Wanaitendea kazi kwa siri ima dhahir! Mwenye macho aidha ya kiroho hata ya kidunia ananaona!muhammad mwenyewe hakuwaani alipo waambia kwamba; "Nyinyi ni waislamu bali sio waumini!" Imani bila matendo ya imani si bure tu? Biblia Takatifu imenifundisha kwamba; "Jaribuni yote bali shikeni yaliyo mema!" Nimeuishi uislamu nikampokea Bwana Yesu, Amina!Mkuu, asante kwa changamoto!
 
Mpendwa nimekupa maswali badala ya jibu napata ,mahubiri?

Maswali yangu katika majadiliano ni yafuatayo (chekundu maneno yako):
Hayo ni mafunuo ya allah kwa kipenzi chake muhammad ili waumini wayatekeleze! usipoyatekeleza, usijipe moyo kwamba nawe ni muumini bali ni kaafir tu!
Hii ilikuwa kuhusu ayat Q9:29 lakini bado hujasema ni nini unayoelewa kama amri kwa Waislamu. Wafanye nini kwa ufahamu wangu??
Na hii -jinsi unavyoelewa- inatekelezwa wapi duniani?

Hao wachache ndio waislamu na bila shaka wamepata thawabu kwa allah! Hao wengi dhamira tu iliyowasukuma, lakini siku za baadaye inshaallah nao watakuwa waumini!
Unachukua wapi kipimo kusema wale wahalifu waliomwua mbalozi walikuwa Waislamu wa kweli na unajuaje walipata thawabu?? Kwa nini hupendi kuwaamini hao wengi waliowafukuza kuwa hao ni waislamu?

Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu???
 
Mpendwa nimekupa maswali badala ya jibu napata ,mahubiri?Maswali yangu katika majadiliano ni yafuatayo (chekundu maneno yako):
Hiyo sio hesabu yenye mtindo wa majibu!Nimekujibu sawia kabisa!
 
Swali kuu ilikuwa: Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu??? Hapa hujajaribu hata kugusa-
Basi kama hupendi au huwezi - tumalize.
 
Swali kuu ilikuwa: Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu??? Hapa hujajaribu hata kugusa-Basi kama hupendi au huwezi - tumalize.
Nimekujibu kwamba; "Imani yangu imenifundisha kwamba jaribuni yote laki mshike yaliyo mema!" Hivyo basi hata wewe usie muislamu umekuja na nadhani kuwa waislamu miongoni mwao si wote wanaokubaliana, na baadhi ya vitendo! Hilo ni sawa kabisa ktk uislamu! Sababu hata muhammad aliwaambia kwamba; "allah angependa wangeku kundi moja na mchungaji mmoja lakini hitlafu miongoni mwenu LAZIMA ziwepo." kuujua uislamu gharama yake ni kusoma quran, hadith, au sunna za mtume wao, na kuwaangalia wanavyouishi ujahidina wao basi. Haihitajiki uwe muislamu ndipo uelewe na kuhitimisha!
 
Swali kuu ilikuwa: Namna gani wewe usiye Mwislamu unapenda kujivalia kofia ya mwalimu na hakimu na kuamua ni nani Mwislamu??? Hapa hujajaribu hata kugusa-
Basi kama hupendi au huwezi - tumalize.

Hao wayatendayo hayo wayatenda wakidai ni waislamu. Haya, ni swali ngapi ziliswaliwa hapa Tz kumuunga mkono sheikh Osama bin Laden? Tena ni watanzania wangapi waliojitolea kupigania uislamu katika nchi ya kiislamu huko Somalia (along Alshabab)?
 
Nadhani unauliza maswali ya maana. Bila shaka wako Waislamu katika nchi nyingi wanaoona hii kazi ya Al Qaeda au Al-Shabab ni wajibu kwa Waaislamu lazima kuwasaidia au kujiunga nao. Hakika watu hao watafungua kitabu cha cha Quani na ndani yake -pale wanapofundishwa kutafuta pamoja na namna ya kuielewa- wataona maagizo kwa ajili ya mapambano yao.

Halafu? Je hii inatuambia chochote kuhusu Uislamu kwa jumla au hali ya robo ile ya wanadamu wanaojiita Waislamu?
Sidhani.

Tafakari yafuatayo:
1) Kwa miaka mingi nchi moja katika Ulaya iliteswa na matendo ya kigaidi. Watendaji walikuwa magaidi wakatoliki na waprotestanti. Je, hii inatuambia nini kuhusu ukatoliki na upotestanti?

2) Kwa karne kadhaa walowezi wazungu walienea Amerika na Afrika hasa kusini. Wengi wa walowezi hao walikuwa wacha Mungu waliosoma Biblia kila siku. Walirejea hasa vitabu kama Yoshua na kadhalika walipoona amri ya kuteka nchi iliyokuwepo mbele yao kwa jina la Mungu Bwana na kuwaangamiza wale wenyeji waliotaka kuwazuia.
Je hii inatuambia nini kuhusu Biblia kama mwomgozo kwa ukatili na mauaji halafu Ukristo kwa ujumla?

3) Tukiangalia matendo ya akina AlQaida na Al-Shabab na kutazama wale waliouawa na kuteswa nao tunaona ya kwamba wengi walioathiriwa na ukatili wao walikuwa Waislamu - si wazungu wala Wamarekani wala wanajeshi wa magharibi bali Waislamu waliopinga namna yao ya kufundisha na kusoma Qurani na kupanga maisha ya kijamii.
Je hii inatuambia nini kuhusu Uislamu?

Kama unapenda kuchukua msimamo wa akina mgen na T1N1 na kuwatangaza hao AlQaeda kuwa "waislamu wa kweli" - unapata jibu eti Qurani ni kitabu cha ugaidi na imani ile vilevile.

Mimi sijali swali la "Uislamu wa kweli". Waamini jnsi wanavyotaka. Ila tu mimi sipendi utembelea kama kipovu na kubana akili yangu. Naona Waislamu walio wengi ni watu wazuri na watulivi wenye maadili mema. Wako tayari kuwasaidia wengine. Inawezekana bila shaka kushirikiana na kuishi pamoja nao. Na wale wenye tabia njema wanasoma Qurani ila tu kwa njia tofauti kuliko magaidi.
Mimi napenda kuishi pamoja na kushirikiana na Waislamu wote wenye maadili mema na utu (pia sipendi kukaa pamoja na Wakristo wakorofi).
 
Mkuu! Mbona hapa penye kutenda matendo ya Imani huniweki sawa?
Hebu tuone alichovuna Bwana Yesu baada ya kuithibitisha Imani yake kwa matendo, anafundisha na kuwajenga wanaomfuasa; "Amani nawaachieni; Amani yangu nawapa; Niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga." Yn14:27!
wafuasi ndicho walicho kiona kwa yesu through matendo yake!

Muhammad anajenga hofu na woga kwake mwenyewe na wafuasi wake! anaogopa giza inapoingia, anaogopa watu, mashetani na majini, walozi, wanawake.... ni woga kwa kwenda mbele soma suratul falaq:1-5 pia soma sura ya mwisho ya qaraa!
suratul nas:1-6
Wafuasi ndivyo walivyo muona muhammad through matendo!
Si hata huku kwetu Uswazi wanasema alivyo shehe sawa na waumini!
 
Wandugu naomba mada hii isichukuliwe kama ya uchochezi BALI hoja mahsusi inayohitaji mjadala kwa mustakabali mwema wa dunia yetu!

Ugaidi umekua ni aina ya uhalifu na unyama wa hali ya juu duniani leo na unaogharimu sio tu maisha ya watu wasio na hatia bali pia unaohujumu na kukwamisha jitihada za mwanadamu yeyote kujiletea maendeleo.

Mbaya zaidi wanaopanga na wanaotekeleza unyama huu wamekua wakijitambulisha kwa Waislam wanaopigania ukombozi wa waislam na uislam.

. Maeneo yanayolengwa na unyama huo yamekua yakihusisha Ukristo kama vile makanisa na majengo ya biashara za wakristo lakini pia maeneo yanayomilikiwa au kuhudhuriwa sana na watu wa asili ya magharibi kwa sababu ya labda Ukristo wao. Na sasa unyama huu umepiga hatua zaidi kwa kulenga mtu mmojammoja kwa mfano kuwamwagia tindikali.

Tokea harakati za Osama hadi leo katlka unyama huu, neno Uislam na waislam haliko nyuma.

Juzi tumeshughudia watoto wakimiminiwa risasi kama mvua pale WEST GATE - Kenya baada ya kushindwa kujibu maswali kadhaa ya kupima uelewa wao wa masuala ya uislam! This is Pathetic.

Ipo mifano mingi tu ya aina na namna hiyo. Sisi waislam tunajua tunalo jukumu la kuhubiri na kuleta amani duniani!

Swali linaumiza vichwa ni:-

Je kwanini Uislamu na Waislamu kila siku ndani ya Ugaidi?
 
Umejitambulisha wewe ni muislamu nilitegemea jibu litoke kwako kwakuwa unaufahamu juu ya imani yako.Labda ungeanza kutuhabarisha kama kuna mafundisho ndani ya uislam yanayo promote ugaidi au kuna udhaifu katika kuufahamu uislamu na mafundisho ya Mtume Mohammed SAW kuanzia hadith .....
 
Wandugu naomba mada hii isichukuliwe kama ya uchochezi BALI hoja mahsusi inayohitaji mjadala kwa mustakabali mwema wa dunia yetu!

Ugaidi umekua ni aina ya uhalifu na unyama wa hali ya juu duniani leo na unaogharimu sio tu maisha ya watu wasio na hatia bali pia unaohujumu na kukwamisha jitihada za mwanadamu yeyote kujiletea maendeleo.

Mbaya zaidi wanaopanga na wanaotekeleza unyama huu wamekua wakijitambulisha kwa Waislam wanaopigania ukombozi wa waislam na uislam.

. Maeneo yanayolengwa na unyama huo yamekua yakihusisha Ukristo kama vile makanisa na majengo ya biashara za wakristo lakini pia maeneo yanayomilikiwa au kuhudhuriwa sana na watu wa asili ya magharibi kwa sababu ya labda Ukristo wao. Na sasa unyama huu umepiga hatua zaidi kwa kulenga mtu mmojammoja kwa mfano kuwamwagia tindikali.

Tokea harakati za Osama hadi leo katlka unyama huu, neno Uislam na waislam haliko nyuma.

Juzi tumeshughudia watoto wakimiminiwa risasi kama mvua pale WEST GATE - Kenya baada ya kushindwa kujibu maswali kadhaa ya kupima uelewa wao wa masuala ya uislam! This is Pathetic.

Ipo mifano mingi tu ya aina na namna hiyo. Sisi waislam tunajua tunalo jukumu la kuhubiri na kuleta amani duniani!

Swali linaumiza vichwa ni:-

Je kwanini Uislamu na Waislamu kila siku ndani ya Ugaidi?

Asante kwa kuleta mada hii. Nakuomba usigadhibike pale watu wa dini nyingine watakapoibuka na kueleza hisia zao kuhusu uislamu. Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa uislamu upo nyuma ya matukio ya ugaidi unaolenga wakristo. Kwenye mitandao kama hii baadhi mmejitokeza kueleza uzuri wa dini yenu na kwamba haya yanayoendelea yanafanywa na watu wasioujua uislamu. Waislamu mna umoja sana duniani kote. Mmekuwa mkitumia maandamano popote duniani kupinga vitendo msivyokubaliana navyo. Lakini mmekuwa kimya kwa hili la dini yenu kutumiwa kuhalalishia ugaidi. Hakuna maandamano wala kauli za kukemea waislamu wenzenu wanaofanya matendo haya. Hii inanifanya nihisi pengine ni maandiko yenu yafundisha hivi.
 
Mkuu umeongea kweli mtupu.
Hatujawahi sikia waislam kokote duniani wakiandamana kupinga hawa magaidi kutumia jina la mwamedi kuahalisha ugaidi wao.
Ila akichorwa tu, utasikia kila siku maandamano.
 
Muislam ambaye mpaka sasa haamini Uislamu na waislamu wanapigwa vita hapa duniani namuonea huruma, hao mnaowaita magaidi ndo waislam sahihi kabisa, mauaji wanayoyafanya pia yanafanywa na majeshi ya serikali nyingi tu dhidi ya waislamu.
 
Naamini waumini wa Uislamu wana uweledi mkubwa juu ya dini yao hadi kufikia kutaka kulazimisha waumini wa dini nyingine wawe waislamu.Ajabu ni kuwa wanaohamasisha ugaidi,hawaelezi kwa uwazi uhusiano kati ya dini yao na ugaidi.Na kama hayafai,kwa nini hawakemei?
 
Wandugu naomba mada hii isichukuliwe kama ya uchochezi BALI hoja mahsusi inayohitaji mjadala kwa mustakabali mwema wa dunia yetu!

Ugaidi umekua ni aina ya uhalifu na unyama wa hali ya juu duniani leo na unaogharimu sio tu maisha ya watu wasio na hatia bali pia unaohujumu na kukwamisha jitihada za mwanadamu yeyote kujiletea maendeleo.

Mbaya zaidi wanaopanga na wanaotekeleza unyama huu wamekua wakijitambulisha kwa Waislam wanaopigania ukombozi wa waislam na uislam.

. Maeneo yanayolengwa na unyama huo yamekua yakihusisha Ukristo kama vile makanisa na majengo ya biashara za wakristo lakini pia maeneo yanayomilikiwa au kuhudhuriwa sana na watu wa asili ya magharibi kwa sababu ya labda Ukristo wao. Na sasa unyama huu umepiga hatua zaidi kwa kulenga mtu mmojammoja kwa mfano kuwamwagia tindikali.

Tokea harakati za Osama hadi leo katlka unyama huu, neno Uislam na waislam haliko nyuma.

Juzi tumeshughudia watoto wakimiminiwa risasi kama mvua pale WEST GATE - Kenya baada ya kushindwa kujibu maswali kadhaa ya kupima uelewa wao wa masuala ya uislam! This is Pathetic.

Ipo mifano mingi tu ya aina na namna hiyo. Sisi waislam tunajua tunalo jukumu la kuhubiri na kuleta amani duniani!

Swali linaumiza vichwa ni:-

Je kwanini Uislamu na Waislamu kila siku ndani ya Ugaidi?

Kweli kabisaa matukio mengi ya kigaidi yanahusiana na uislam na waislam.Mimi siyo muumini wa dini hiyo na sielewi sana juu ya mafundisho ya dini hiyo,lakini ukweli huu hautanifumba mdomo nisitoe hisia zangu.
Dini ya kiislam inawaminisha waamini wake kudai haki kwa njia ya "violence",hili linajidhihirisha kwa kuangalia mifano michache iliyowahi kutokea hapa nchini kwetu.
La kwanza;waislamu walivyochapana bakora Kyela ktk ibada ya Idi mwaka huu.
La pili,vurugu za mwembe chai.

Hii ni mifano michache achia mbali mafundisho yao tunayoambiwa kuwa hata mtoa mawaidha msikitini akipotosha hata kama ni kwa bahati mbaya adhabu yake ni bakora,kama hii haitoshi hata mwizi kwa mujibu wa sharia anatakiwa kukatwa mkono.Sasa kwanini tusiamini kuwa hii dini ikifuatwa bila kupindapinda inafundisha mapigano na kukuza chuki.Mtanisamehe ndugu zangu nitakaokuwa nimewakwaza,lakini kwenye ukweli tuwe wakweli,mafundisho ya namna hii ndicho chanzo cha ugaidi.
 
Uislamu ni ugaidi hilo halina ubishi..Ugaidi ni imani yenye kumuabudu shetani ajulikanaye kam HUBAL ambaye ni mungu anayeabudiwa na waislamu wa leo kwa kuiga waarabu wa macca ambao humwabudu kwa kugusa paji la uso ardhini kuonesha ibada ya kuzimu,kwenda kwenye misikiti mara kadhaa kwa siku na kusali kuelekea ulipo mji wa makka..Kimsingi Hubal ni shetani ambaye alimwingia Mtume muhamadi SAW ambapo mtume hukiri kwenye quran kwamba alikuwa anaendeshwa na nguvu ya shetani(Google neno Hubal).Quraishi ambalo ni kabila la mtume walimfukuza baada ya kuchochea umwagikaji damu ili mungu mwezi aitwaye allah apate damu ya kunywa.Alama nyeusi kwenye paji la uso la muislamu ni chapa ambayo imeelezewa kwamba wamuabuo mnyama wa ufunuo watapigwa hivyo ugaidi ni ibada ya shetani iliyopandikizwa ktk uislamu na sio kweli kwamba uislam ni Amani hata kidogo.Islam=Submit.

Nakusikitikia kwa kutokua mdadisi na kuyachukulia mambo juu juu bila kufanyia utafiti wa kutosha... Nini maana ya uislam? Uislam una maana mbili ya kwanza: amani, ya pili: kufata maarisho ya allah(arabic) god(english) mungu(swahli) na kuacha yote yanayomchukiza..

Na ktk uislam yesu (masih) ametukuzwa na amesafishwa ktk yote ya uongo wanayomsingizia na wale wampingao; kuhusu waislam kuabudia shetani huo ni UONGO tena ni ujinga mkubwa... Huyo unaemsema (HUBAL) ndio alokua mungu wa watu wa makka enzi hzo kabla nuru ya uislam haijawafkia baada ya nuru ya uislam kuenea na kuweza kuukomboa mji huo wa makka kutoka ktk ujinga wa kuabudia masanam ndipo mtume muhammad (s.a.w) alipowaamrisha waislam wasafishe kaaba na waondoe kla aina ya uchafu ukiwepo masanamu yalokua enzi hzo na tangu hapo kaaba haina chochote ndan yake ni kweupeee na waislam wanatumia kuabudu kwa kuelekea hapo km ndio nyumba ya kwanz ya kuabudu mungu dunian kuwah kujengwa na ilijengwa kwa mara ya kwanz na nabii ibrahim (a.s) na pia hutumiwa km kiunganish cha waislam kote dunian: rejea ibada ya hijja-makka (pilgrimage at mecca) na kwa uthibitisho km waislam hatuabudii lile jumba kaaba waadhin (wanaowaita waislam ktk ibada ya sala) hupanda juu ya ile kaaba wanaikanyaga soo kwa akili ya mungu mmoja mungu hawez kufikiwa na binadam wa kawaida na kukanyagwa vle...

Sooo ulichoandika ni uongo mtupu na umekosea sana kama unataka kuujua ukwel uliza wanaojua wenye dini hyo(wasomi) na si mtu asiesoma na ktk mitandao articles nyingi ni za uongo soo ktk kufatilia information usiangalie link moja tu hutopata ukwel na undan unaoutaka .. Na shetan anapingwa vbaya mno ktk uislam kwa kupitia uthibitsho mbalimbali unaotoka ktk quran na quran imetoa maelekezo ya jinsi ya kujikinga na huyo shetan umsemaye..
 
La kujiuliza kwanza nani na wapi iliwahi kusikika kuwa kuna mkristo kajiua au kuua wengine
ili kutetea dini yake ya ukristo!!!!! ukiona hakuna jiulize Mungu ni wa upendo ndio maana alimuumba
mwanadamu,hawezi kufurahia mwanadamu mwingine amuue mwenzake eti kwa sababu ya kumtetea
yeye!!!huyu ni mungu wa dunia hii anayeitwa ibilisi au shetani ndiye anayefurahia kuona mwanadamu anatenda
dhambi kwa kuua au kujiua ili mpango wake wa kuwapeleka watu wengi motoni ufanikiwe.Ikumbukwe shetani
hana huruma na mwanadamu kabisa anafurahia kumuona anateseka;Ila ni ukweli ulio wazi kuna uhusiano mkubwa
kati ya ugaidi na uislam'
 
Hv nyinyi mnaojiita wakristo mnaakili dhaifu hamfatilii mambo akishasema mchungaj wenu bas mnayabeba hvyo hvyo nimeamin kwel mapreaches wanakupandikizien chuki na uhasama juu ya uislam na waislam na kukufichen ukwel juu ya uislam soma link hii ntayoitoa ndo utajua ukristo walipigana vp miaka hyo : fatilia hapa itakusaidia kukupa picha ya ukristo wako na km waliwah kupigana wakristo kwa wakristo na ugaid juuuuuu. European History/Religious Wars in Europe -
Wikibooks, open ...
 
mimi kama muislam naweza kukusaidia ni kwamba kuitwa magaidi na majina mengine kama hayo sio mwanzo leo wala jana ni tangu mtume, makafiri wamekuwa wakiwaita waislam majina mabaya na imeandikwa hata kwenye kitabu, sasa ss waislam hatushangai tunajua ipo hivyo.

kiongozi wa LRA (Lord Resistance Army) joseph konyi wa uganda kuanzia mwaka 1986 mpaka leo, akidai kuongozwa na roho mtakatifu (andika tu kwenye google joseph konyi) amewauwa watoto wangapi amewabaka wanawake wangapi lakini kwasababu anataka kuanzisha serikali inayofuata sheria za biblia na yeye ni mkristo basi sio gaidi. ila akifanya muislamu tu hatakama kamwagia mtu maji ya kunywa basi huyo ni gaidi.

Nchi za magharibi kupitia New World Order (Freemanson) wanataka wa control serikali zote dunian, na kuanzisha sheria za demokrasia kama vile ndoa za jinsia moja kuwa ni uhuru wa mtu (democracy). mmesahau sodoma na gomora, enzi za nuhu. nisikuchoshe usinichoshe kama unataka majibu zaidi kwanini alshababu wamefanya walicho kifanya tembelea aljazera kuna interview kati ya msemaji wa al shababu na wao link http://www.aljazeera.com/indepth/features/2013/09/2013923628350977.html
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom