Makindi N; Wamarekani walishatulipiga campaign fulani ikawa inaonyeshwa sana kwenye TV, inaanza kwa kusema kutana na Bwana -------(jina nimelisahau). Akiwa ofisini anaheshimika, role model, anafuatwa kwa ushauri etc, akiwa nyumbani ni kivumbi hawaivi na Wife wake". Mwisho wa siku ujumbe ulikua ni ZUNGUMZA NA MWENZIO.......
Japo sikulipenda kbs lile tangazo, yaani umeoa hata kuzungumza na mwenzio nako hadi iwe campaign tena ya kulipiwa na wafadhili? Km nisivyoipenda campaign ya kunawa mikono.... Fifty years of independence?
Kimsingi zungumza na mwenzio... kama unavyozungumza na waofisini............
Makindi N, Tatizo liko hapo kwenye Red hapo, appreciation tunazitowa kwa wafanyakazi wenzetu maofisini lakini majumbani kwa wenzi wetu tunakaa kimya. Tunasubiri wakosee ndo tuyaseme hayo makosa. Wamarekani wanayafanyia matangazo maana wameona jinsi gani mambo kama hayo (mawasiliano) yalivyo ya muhimu katika jamii na watu wanayapuuza. Wanajaribu kutia changamoto kuongeza upendo kupitia mawasiliano bora ndani ya familia na hivyo kupunguza idada ya ndoa zinazovujinka kila siku. Kuna siku moja niliona bango moja ''Do you need a divorce? call 832......'' Hii inaonyesha ni jinsi gani kuvunjika kwa ndoa limeshakuwa jambo la kawaida kabisa katika jamii.