Isiwe Makazini tu Iwe pia na Majumbani Mwetu

Oak

Member
Sep 6, 2011
33
18
Ni asubuhi njema natumahi.

Mara nyingi tumekuwa tukipata compliments nyingi makazani pale tunapokuwa tumefanya vyema kwenye kazi. Compliments zinaweza toka kwa wafanyakazi wenzako na hata kutoka kwa maboss wako pia.Tunajisikia vizuri tupatapo hizo compliments na kutufanya tuwe makini na kuongeza bidii. Ndiyo, ni jambo jema kwa mwanadamu kutambua kazi au kitu kizuri alichokifanya mwenzako kama hauna roho mbaya.



Mada yangu zaidi ni kutaka hizo compliments ziende pia hata huko majumbani tunako ishi. Mke/mme akifanya jambo jema na unaona ni kiwango na linahitaji kusifia , usimbanie acknowledge kwa alicho kifanya atajisikia vizuri. Tusiwe tunanyamaza kama vile hatuoni wakati unaona mwenzi wako kafanya kitu cha maana. Tusisubili tu pale anapofanya kosa ndo tucharuke na kutupiana lawama za ''kwa nini umefanya vile''. Tujikite zaidi kuangalia mazuri wanayofanya wenzi wetu na tuyape credits. Kwa kufanya hivyo kutamfanya mwenzi wako ajisikie kuwa anathaminiwa na unauona umuhimu wake katika maisha yako.



Tupende pia kuwajengea imani wenzi wetu kuwa wanaweza. hata kama ni makazini huko wana assignments ngumu na tights, tupende ku-acknoledge na kuwatia moyo kwa mfano‘' baba/mama Mary japo unalalamika assignment yako ni ngumu lakini mimi nakuaminia hiyo utaifanya vizuri tu,jitahidi '' Unajisikaje mumeo au mkeo akikwambia hivyo? Hii itamjengea moyo waubani wako na kuzidi kukuthamini, na pia inaongeza vionjo/radha ya mapenzi na ukaribu kwa mwenzi wako.



Kwa kufanya hivyo tutapunguza migogoro siziso za maana katika mahusianao na kuongeza upendo ambao na furaha ambao ndiyo tegemeo zaidi katika mahusiano ya kimapenzi. Tusitegeane kusubiri makosa bali tuyaangalie zaidi mazuri na tuonyeshe tumeyaona. Kutapunguza pia idadi ya mabaya amabyo yangejitokeza kwa kuogopa kumkwaza mwenzi wako.


It works to me it may also work to you…….. Jaribu.
 
Hiyo ni nzuri sana kiukweli na si lazima umpe chochote bali maneno tu kuonesha appreciation nayo yanafaa, lakin pia panapowezekana onesha kumkubali hata kwa kumtuza kwa chochote itaongeza hamasa zaidi na upendo wa dhati kwan hiyo itakuwa ni ishara tosha ya kujaliana na kujali mchango wa mwenza wako ktk maisha. Lakin haya yanawezekana tu kwa wale walioridhiana nafsi na kuishi kama wenza na sio kwa wale waishio kama vile wamelazimishwa kuishi pamoja.
Mpende akupendae, asiyekupenda pia usimchukie.
 
TANMO; Ushauri mujarabu kabisa, wahusika kazi kwenu!

Mkuu hii ni hata kwa GF/BF wako siyo lazima muwe mnaishi wote tu ndo u-appreciate mema anayokufanyia. Mkubali mtu wako usibanie.
 
F12: Hiyo ni nzuri sana kiukweli na si lazima umpe chochote bali maneno tu kuonesha appreciation nayo yanafaa, lakin pia panapowezekana onesha kumkubali hata kwa kumtuza kwa chochote itaongeza hamasa zaidi na upendo wa dhati kwan hiyo itakuwa ni ishara tosha ya kujaliana na kujali mchango wa mwenza wako ktk maisha. Lakin haya yanawezekana tu kwa wale walioridhiana nafsi na kuishi kama wenza na sio kwa wale waishio kama vile wamelazimishwa kuishi pamoja.
Mpende akupendae, asiyekupenda pia usimchukie.


Ni kweli F12 wengi kupo kujisahau au kutojuwa jinsi gani maneno madogo madogo ya kumkubali mwenzi wako alivyo chachu ya kuongeza upendo na kukumbukwa. Hii siyo itoke kwa wakaka tu bali hata kwa wadada kwenda kwa wakaka. Mumeo/BF wako atajisikia vizuri kama unamkubali kwa kile anachokifanya. Siyo mambo ya nabii hakubaliki kwao, mkubali huone sura itakavyombadilika na kuonyesha tabasamu la nguvu.
 
  • Thanks
Reactions: F12
Husninyo; we huusiki?

Ahsante kwa ushauri.

Husninyo, huyu nimeshamwambia hata kwa GF/BF wake nako pia anatakia kuonyesha appreciation. Siyo tu kwa wale alioko kwenye ndoa.
Hata kwenye signature yake kasema ''Do something'' kwa hiyo hiyo something ndo appreciation yenyewe
 
Mkuu hii ni hata kwa GF/BF wako siyo lazima muwe mnaishi wote tu ndo u-appreciate mema anayokufanyia. Mkubali mtu wako usibanie.

Mkuu Oak heshima mbele, ushauri wako nitaufanyia kazi pindi nitakapo husika..
 
TANMO; Mkuu Oak heshima mbele, ushauri wako nitaufanyia kazi pindi nitakapo husika..

TANMO, sawa mkuu tunapeana chachu katika haya mambo maana yakialibika huko nyumbani yawezekana pia huko kazini mambo yasiende sawa.
 
Wamarekani walishatulipiga campaign fulani ikawa inaonyeshwa sana kwenye TV, inaanza kwa kusema kutana na Bwana -------(jina nimelisahau). Akiwa ofisini anaheshimika, role model, anafuatwa kwa ushauri etc, akiwa nyumbani ni kivumbi hawaivi na Wife wake". Mwisho wa siku ujumbe ulikua ni ZUNGUMZA NA MWENZIO.......

Japo sikulipenda kbs lile tangazo, yaani umeoa hata kuzungumza na mwenzio nako hadi iwe campaign tena ya kulipiwa na wafadhili? Km nisivyoipenda campaign ya kunawa mikono.... Fifty years of independence?

Kimsingi zungumza na mwenzio... kama unavyozungumza na waofisini............
 
Makindi N; Wamarekani walishatulipiga campaign fulani ikawa inaonyeshwa sana kwenye TV, inaanza kwa kusema kutana na Bwana -------(jina nimelisahau). Akiwa ofisini anaheshimika, role model, anafuatwa kwa ushauri etc, akiwa nyumbani ni kivumbi hawaivi na Wife wake". Mwisho wa siku ujumbe ulikua ni ZUNGUMZA NA MWENZIO.......

Japo sikulipenda kbs lile tangazo, yaani umeoa hata kuzungumza na mwenzio nako hadi iwe campaign tena ya kulipiwa na wafadhili? Km nisivyoipenda campaign ya kunawa mikono.... Fifty years of independence?

Kimsingi zungumza na mwenzio... kama unavyozungumza na waofisini............





Makindi N, Tatizo liko hapo kwenye Red hapo, appreciation tunazitowa kwa wafanyakazi wenzetu maofisini lakini majumbani kwa wenzi wetu tunakaa kimya. Tunasubiri wakosee ndo tuyaseme hayo makosa. Wamarekani wanayafanyia matangazo maana wameona jinsi gani mambo kama hayo (mawasiliano) yalivyo ya muhimu katika jamii na watu wanayapuuza. Wanajaribu kutia changamoto kuongeza upendo kupitia mawasiliano bora ndani ya familia na hivyo kupunguza idada ya ndoa zinazovujinka kila siku. Kuna siku moja niliona bango moja ''Do you need a divorce? call 832......'' Hii inaonyesha ni jinsi gani kuvunjika kwa ndoa limeshakuwa jambo la kawaida kabisa katika jamii.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom