Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,673
- 698,670
Inasemekana kwamba kabla ya kuingia baharini mto hutetemeka kwa hofu.
Unatazama nyuma kwenye njia ambayo umepitia, kutoka vilele vya milima, barabara ndefu yenye kupindapinda inayovuka misitu, vijiji na maporomoko
Na mbele yake, unaona bahari kubwa sana, kwamba kuingia huko inaonekana hakuna kitu kingine zaidi ya kutoweka milele.
Lakini hakuna njia nyingine. Mto hauwezi kurudi nyuma.
Hakuna mtu anayeweza kurudi nyuma. Kurudi nyuma haiwezekani kuwepo.
Mto unahitaji kuchukua hatari ya kuingia baharini kwa sababu ni hapo tu hofu itatoweka, kwa sababu hapo ndipo mto utajua sio kutoweka ndani ya bahari, bali ni kuwa bahari yenyewe...
Hofu yetu ya kifo ni kabla ya kuingia kifoni..! Ukishakufa hofu hutoweka kwakuwa hutakuwa wewe tena bali kifo chenyewe na wala hutajua kwamba umekufa
Lakini kama vile mto usivyolazimishwa kupanda mlima vivyo hivyo kifo nacho hakilazimishwi
Wote walazimishao kifo na kufa hawana mwisho mwema daima... Acha asili ichukue mkondo wake..!
Sent using Jamii Forums mobile app