Kwa kinachoendelea Iringa nadhani viongozi wanaohusika na wanyamapori watumbuliwe

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,248
22,320
Kwa masikitiko makubwa sana naandika huu uzi nikiwa sijui itakuwaje kwa wananchi wa Iringa wanaoishi kwa hofu kutokana na kundi la Simba lililopo kwenye maeneo yao. Vyombo vya habari kwa zaidi ya mwezi vimekuwa vikitangaza kila siku kuhusu hao Simba waliotoroka kutoka Ruaha na kuingia kwenye makazi ya watu.

Ng'ombe zaidi ya 30, mbuzi, kondoo, kuku na nguruwe wametajwa kuliwa na Simba hao. Hakuna kifo cha binadamu kilichoripotiwa. Mamlaka inayohusika imekuwa ikisema kwamba inawatafuta Simba hao na kuna siku waliwaona ila wakashindwa la kufanya kwa sababu wangeweza kuwajeruhi watu.

Taarifa ya mwisho ilisema kwamba mamlaka zimeamua kutumia helikopta kuwatafuta hao Simba.

Mimi siridhishwi kabisa na hatua zilizochukuliwa. Hata matamko yao siyakubali. Huu ni uzembe wa makusudi. Sio mara ya kwanza wanyamapori kuvamia makazi ya watu na kusababisha maafa.

Huko Karatu kumetokea matukio mengi ya binadamu kuliwa na fisi hadi mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mheshimiwa Cecilia Paresso alipeleka hoja bungeni kuhusiana na hilo. Tembo nao wamekuwa wakitajwa kusababisha majanga.

Mimi ninashauri wanaohusika na kuwaondoa hawa Simba kwenye makazi ya watu wapigwe tu chini na kuwekwa watu wenye uwezo. Wafukuzwe kazi. Hawa wameshindwa. Baadae unaweza sikia ilitumika bilioni 4 kutafuta Simba.
 
hadi wauwe watu ndio serikali itaamka kutoka usingizini na kujifanya tutagharamia mazishi etc...... hii nchi ya ajabu sana uwajibikaji 0 mpaka madhara yatokee ndio watu wanashtuka...... sijui ni lini tutakuwa serious na mambo
 
Sasa kama umeambiwa wamesitisha law sababu wangepiga watu unataka wafanyeje?

Na usichojua ni kwamba wananchi ndo wameendelea kusogelea na kuingilia makazi ya wanyama
 
Tutaiuza mbuga hiyo. Msipige tu makelele
 
Tuwape DP world Tanapa
 
Sasa kama umeambiwa wamesitisha law sababu wangepiga watu unataka wafanyeje?

Na usichojua ni kwamba wananchi ndo wameendelea kusogelea na kuingilia makazi ya wanyama
Simba wapo zaidi ya 130km kutoka Ruaha national park na zaidi ya 300km kutoka mikumi. Kuna mdau alisema hawa Simba walihamishiwa Ruaha, sasa pale ni wageni na Simba wenyeji hawawataki.
 
Back
Top Bottom