mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,640
- 21,973
Huu uzi nimerudia kuusoma tena nikakumbuka subtopic moja kwenye geography fm3 ya river profile. Kwamba mto wowote unaopitisha maji unakuwa na stage 3 hivi. 1. Young stage/upper stage.2.Middle stage/mature stage. 3.Lower stage/older stage. Stage hiyo ya kwanza mto huwa na kasi sana ya maji na pia kuna maporomoko makali sana ya maji,huko sio rahisi kukuta watu wanaogelea au kuvua. Hiyo stage ya pili ni kama pale mto wami darajani.Maji yake matulivu kiaina ila bado yana nguvu. Na stage ya mwisho ambapo mto huwa unaingia baharini unakuwa mtulivu na mnyonge sana na ndio hapo utakuta maji matulivu na watu wanaeza pita na mashua zao za uvuvi, meli zinaweza pita kuogelea na hayana kina kirefu n.K . Ukijaribu ku relate na maisha ya uhalisia kuna mengi ya kujifunza.