Ishara 9 za kutambua kama mpenzi wako anaku-control

Ethan Cruz

JF-Expert Member
Apr 29, 2021
231
331
shutterstock_139584320.jpg

#1 Wakati wowote mnapokosana, ni wewe ndiye unayelaumiwa.
Ukiwa na huyu mwanamke na kila wakati mkiwa mnagombana, mwisho lazima uchukue lawama hata kama kosa ulilofanya si lako. Na utapata mwanamke huyu ataushikilia msimamo wake na atatumia mbinu zozote zile kuhakikisha kuwa lawama inakuangukia wewe.

Hii ni ishara ya mwanamke anayekukontrol kwa kuwa anatumia mbinu hii kuishusha confidence yako mbele yake. Hivyo hii ni ishara kuu ambayo hujitokeza katika kila mwanamke anayetumbia mbinu ya kukontol mwanaume.

#2 Anakasirika haraka kama hakupata kile ambacho alikuwa anatarajia.
Hii ni ishara nyingine inayodhihirika kwa wanawake aina hii. Wao kila wakati wanatarajia mambo yao kuenda sawa, lakini ikitokea siku ambapo hapakwenda vile wanatarajia basi wanakasirika haraka.

Mfano labda umemuahidi kitu flani lakini hukukitimiza kwa wakati unaofaa, utamuona akikasirika bila sababu. Hii ni mbinu wanayoitumia ili kuifanyia ufidhuli akili yako ili uweze kutimiza wanachotaka wakati wowote wanapojiskia.

#3 Wakifanya jambo lolote, lazima wakujulishe.
Mwanamke anayependa kukontrol watu hupenda masifa ya kusifiwa wakifanya jambo zuri. Kwa mfano anaweza kuwa amepika chapati tamu hivyo atataka umpe sifa. Sifa hizi ndizo ishara ya kuonyesha kuwa anatabia za kukontrol watu.

Zaidi anaweza kutaka sifa hizi ziwafikie hata marafiki zako na familia yako ukimsifia jinsi alivyo mpenzi bora zaidi ya wote.

#4 Hakuna kitu unachofanya anakiona kizuri.
Hata umpeleke Dubai ama umtoe akaone shoo ya Fiesta, bado ataona ya kuwa hujafanya jambo ambalo linafikia kiwango cha kusifika. Mwisho wa siku utaendelea kufanya kila mbinu ili angalau uweze kumridhisha.

Lakini siri ni kuwa kile ambacho anachofanya hapa ni kukufanya uhisi ya kuwa haumfurahishi vile ambavyo inafaa. Hivyo utatia bidii kiasi cha kuwa utajiona haumfai ama haumtoshelezi.

#5 Anauliza kila kitu unachofanya.
Mwanamke anayekukontrol kwa kawaida hajiamini. Yeye hujiona kuwa na thamani ya chini hivyo kila kitu ambacho utakuwa unafanya atataka kujua ni nini. Hii hutokea kwa kuwa hakuamini na chochote ambacho umefanya ama utafanya. Yaani kiufupi hatakubali kuona unamshinda kwa chochote. Na pia atataka kujua mafanikio yako yote ili aweze kunufaika na kwayo.

#6 Anatumia ngono kama kigezo cha kukukontrol.
Wanawake wanajua umuhimu wa ngono kwa mwanaume. Hivyo mwisho wa siku kila mwanamke atatumia mbinu zake ili kutaka kile anachotaka kupitia mapenzi.

Lakini ukiona mwanamke anakunyima msifanye mapenzi kwa kuwa hujamnunulia kitu fulani ama hujamfanyia jambo fulani, basi uwezekano mkubwa ni kuwa mwanamke huyo anakukontrol.

#7 Anakutishia kukuacha.
Mwanamke anayekukontrol hupenda vitisho vya mara kwa mara vya kukuambia kuwa atakuwacha bila hata kumkosea ama kumfanyia jambo lolote baya. Mwisho wa siku kwa kuwa unampenda utakuwa tayari kumfanyia lolote lile ambalo anataka umfanyie bila hata kufikiria mara mbili.

#8 Mwivu.
Kila mtu anakuwa na chembechembe za wivu ndani yake. Lakini mwanamke anayekukontrol anakuwa na wivu uliopita kiasi, na mara nyingi chochote unachofanya lazima aone wivu.

Mfano unaweza kuwa unapiga simu za kikazi na ni mwanamke unayeongea naye utamkuta anatega maskio kutaka kujua ni nani unayeongea naye na ni kwa nini.

#9 Anakuaibisha.
Mara nyingi mwanamke huyu yuko tayari kukushusha hadhi ujione ya kuwa haufai. Pia anaweza amekubandika jina la kimajazi ama ukifanya jambo anaweza kukuangalia na uso wa kuonyesha kuwa unafanya upumbavu. Lengo lake kuu hapa ni kuhakikisha kuwa anashusha confidence ndani yako.

Ok. Kama umejikuta katika mahusiano na mwanamke na ameonyesha moja ya ishara hizi usiharakishe kuona kuwa anakukontrol, lakini ukiona ameonyesha ishara zaidi ya tano ya hizi basi fahamu mwanamke unayempenda anakukontoli.
 
#1 Wakati wowote mnapokosana, ni wewe ndiye unayelaumiwa.
Ukiwa na huyu mwanamke na kila wakati mkiwa mnagombana, mwisho lazima uchukue lawama hata kama kosa ulilofanya si lako. Na utapata mwanamke huyu ataushikilia msimamo wake na atatumia mbinu zozote zile kuhakikisha kuwa lawama inakuangukia wewe.
Huu utafiti nakupa Zaid ya 100% nimejiona kabisaaa
 
Mkuu safi sana.
hii kitu nilitaga nianzishie uzi ila nilikuwa na mambo mengi sema sio mbaya acha nikuongezee madini

10.mara nyingi unagombana na watu wa karibu yako inaweza kua ndugu,wazazi,marafiki ambao kabla haujakuwa na huyu mpenzi wako wa sasa mlikuwa na mahusiano mazuri.hii kwa sababu katika process ya huyo mpenzi wako kucontrol anachofanya ni kukuchonganisha na watu wako wa karibu ili yeye awe na sauti juu yako na ukose wa kukushauri kwa vile ushagombana na ndugu zako

11.unajihisi hauna maamuzi juu ya vitu vyako na life style yako.hii kitu unaweza ukagundua kwanzia mavazi,vitu unavyopenda,miondoko ya maisha yako unaona kabisa sio wewe na ukichunguza vizuri unakuta hayo mabadiliko yanasukumwa na mpenzi wako

12.pale unapotaka kuamua jambo lolote kuna hofu inakuja moyoni mwako ikuambia lazima mpenzi wako ajue na atoe maamuzi,mara nyingi hapa ukienda kuomba mchango wake unabeba ushauri wake na wazo lako unalitupa bila hata kufikiria sana

13.watu wanaozunguka wanasema unaburuzwa.hii kwa sababu mara nyingi watu wanaokuzunguka ndio wana kujua ulivyo kuliko hata wewe unavyojitambua,kuna msemo unasema aliye uwanjani ni ngumu kujua makosa ya timu ila yule aliyeko nje ya uwanja ndio anajua vizuri

14.anajiamini sana juu yako.saikolojia inasema mara nyingi binadamu huwa hajiamini vizuri akiwa kwa watu asio wafahamu ila huwa anajiamini sana kwa watu anawajua vizuri kwa sababu anakuwa anajua siri zaki ,udhaifu,kufikiri kwako na anakucontrol

Asante mtoa mada nina mambo mengi ya kueleza ila bora nieshie hapa maana isije kawa uzi ndani ya uzi
 
Kuna wimbo unaitwa DALILI sijui kaimba nani ukiusikiliza nadhani unaamisha hayo yote hapo

#1 Wakati wowote mnapokosana, ni wewe ndiye unayelaumiwa.
Ukiwa na huyu mwanamke na kila wakati mkiwa mnagombana, mwisho lazima uchukue lawama hata kama kosa ulilofanya si lako. Na utapata mwanamke huyu ataushikilia msimamo wake na atatumia mbinu zozote zile
 
Back
Top Bottom