Dar es Salaam: MKALI wa Mipasho Bongo, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ hivi karibuni alipata msiba wa baba yake Mzee Ramadhani Ally Makonga lakini baada ya mazishi ikadaiwa msanii huyo aliwafanyia kitu mbaya nduguze kiasi cha kusababisha mpasuko ndani ya familia.
Chanzo chetu kilicho karibu na familia ya Isha kilidai kuwa, baada ya msiba kutokea ulitokea mvutano mkubwa kati ya Isha na ndugu zake, yeye akitaka mwili uzikwe Dar huku ndugu wakitaka wasafirishe kwenda Musoma.
“Ulitokea mvutano mkubwa sana, baadaye kwa shingo upande Isha akakubali mwili usafirishwe, lakini akawa kama aliyejiweka pembeni hivi.
“Ndugu wakawa wamejipanga kwa ajili ya kusafirisha mwili, wa kuomba ruhusa makazini wakaomba na kujifungasha kwa safari, walipofika Mbezi Kwa Msuguri ambako ndiko msiba ulikuwa, wakashangaa tena kuona Isha ameng’ang’ania mwili uzikwe Dar.
Wanandugu wakiwa msibani.
“Ikawa tafrani! Na alisema hivyo akijua suala la fedha bila yeye kuwa mstari wa mbele litawakwamisha. Na kweli baada ya michango kupitishwa, pesa ikapelea, wakati huo Isha kajiweka pembeni.
“Ilipokosekana pesa ya kusafirisha, ndipo Isha akasema mwili uzikwe Dar, ndugu wakabaki wamepigwa na butwaa, kimsingi kawafanyia kitu kibaya,” alisema mtoa habari huyo.
Ikadaiwa kuwa, kufuatia Isha kutaka mwili uzikwe Dar kwa sababu anazozijua yeye, baadhi ya ndugu wakamsusia msiba na kuondoka Mbezi Kwa Msuguri na kwenda kujikusanya nyumbani kwa kaka wa marehemu, Mbezi Afrikana ambako waliomba dua.
Akizungumza na Ijumaa, shangazi wa Isha aliyejitambulisha kwa jina la Pili alisema, alichowafanyia Isha hakukitarajia na wamejisikia vibaya sana.
“Mimi nikiwa kama shangazi yake, tumbo moja na baba yake ni wazi amenidharau kwa hili, wazee wetu tumewazika Musoma na ndiyo sababu nilitaka na ndugu yetu tumzike huko, lakini mtoto kakataa katakata wakati mwanzo alikubali tukachanga michango, naamini kuna watu walimshika masikio na hawakuwa na nia nzuri kutokana na yale niliyoyaona yakitendeka pale msibani.
Ndugu wakiwa wamejiandaa kwa safari.
Mbali na shangazi yake huyo, dada wa Isha aitwaye Mwanaidi alisema: “Kitu ambacho kinaniumiza kichwa ni nguvu aliyoitumia kutaka mzee asisafirishwe, kwani ametudharau sisi ndugu zake kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa Isha aliyeomba hifadhi ya jina lake alimtetea msanii huyo wa taarab kuwa, hakuwa na nia mbaya bali ni kutokana na mama yake mzazi kuwa mgonjwa na pia ugumu wa kupatikana pesa za kusafirisha.
Kwa upande wake Isha, alipotafutwa kufuatia madai hayo aliporomosha matusi mazito ambayo hayaandikiki gazetini kisha akasema:
“Sasa ukishajua itakusaidia nini, mbona nilipofiwa hukunipa pole ndo unakuja kuniuliza huo ujinga?"
Chanzo: GlobalPublishers