Is Tundu Lissu a Moderate?

Wewe individually ni uhuru gani Umenyimwa? Siasa zimewafanya Mmekuwa Wajinga kabisa,
Umesingiziwa Kesi?
Umefanya biashara zako au miradi yako ikakwamishwa na Serikali?
Bila shaka hata maisha yako binafsi hayana mwelekeo, Jitume tafuta pesa zako, Huyo Tundu Lisu au Zitto kama unavyojiita Acount zao za bank zimejaa mabilioni wewe una nini? Acha ushabiki wa Kijinga unapoteza Muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi individual selfishness ndio zinaturudisha nyuma kwamba ukiwa na kila kitu/Huna kitu basi ya wengine hayakuhusu?. Nyerere angewaza hvi angejihangaisha na kudai uhuru wakati alikua msomi?

Unapojadili siasa za kitaifa unaangalia macro level maana ndio zinaathiri mpaka micro level. Yaani bunge likiminywa litatunga sheria mbovu zitaathiri mpka wewe na mimi. Kiufupi 80% ya maisha yetu ya kila siku yanaathiriwa na siasa kwahiyo hta nkiachana nazo bado zitaniathiri.
 
Kifungu cha 74 cha Public audit regulations ya mwaka 2009 inasema kuna entry na exit meetings ambapo CAG ataeleza malengo ya ukaguzi na matokeo na huwapa siku 21 kujibu zile hoja zake wakishindwa ndio zinafikishwa bungeni kwahiyo sio kweli kwamba maelezo yanatolewa kwenye kamati bali yanatolewa ofisi ya CAG asiporidishwa na majibu ndio anaandika kwenye ripoti. Kwahiyo hapa umepotosha tena.

2. Sheria namba 11 ya 2015 (sheria ya bajeti) kifungu 8 inatoa mamlaka kwa bunge kuidhinisha ukomo wa ukopaji yaani kma serikali imekadiria kukopa trillion 3 basi hiyo ceiling inafungwa na bunge ikizidishwa inatakiwa bunge lifahamu maana bajeti ni sheria!! Kasome CAG report 2016/17 anasema 10% ya fedha zilikopwa zaidi kuliko ukomo uliyoidhinishwa na bunge then wwe unasema ipo kisheria ina maana CAG hakufanya exit meeting kujua ni sheria inaruhusu hadi auite uzembe? Mbona unapotosha mkuu.

3. Kuhusu Mbowe hujaelewa context. Yaani CAG anakuta bodi imeidhinisha pesa ya gari la mtu binafsi na pesa inayoenda kwa mtu binafsi. Sasa ya gari ameona documents zina deviate alafu kwa Mbowe deni hewa hajaomba proof of payment/invoice ila akaridhika kuwa pesa ililipwa kihalali (If at all amejikopesha)?? Kwahiyo bodi ikiidhinisha malipo ya gari inakaguliwa documents ila kwa deni la Mbowe yeye anaishia kwenye ripoti za bodi tu hta kma deni ni hewa? Hvi tupo serious mkuu

NB: Naomba ukirudi uje na facts
 
Mbona mnataka kuforce kwamba urais ni jambo binafsi jamani. tulieni kampeni zianze basi.
 
Kaka naomba tuheshimiane kidogo.Usidhani kila unaejadiliana nae humu ni mpuuzi kiasi cha kujifanya unaquote vifungu vya sheria ili uonekane upo deep kumbe unadanganya. Wengine hivi vitu tunavifanyia kazi siyo tu kuvisoma.

Sheria ya Bajeti Na.11 ya 2015, kifungu cha 8 (a) - (g), kinaeleza kuhusu Responsibilities of National Assembly on The Budget Process. Ambapo kwa tafsiri fupi na rahisi inaeleza hivi;

Bunge litajadili na kuridhia makadirio ya awali ya bajeti; kupitia na kujadili mwongozo wa mpango wa bajeti na makadirio ya awali ya bajeti; kusimamia masuala yote ya Bajeti yanayoangukia kwenye mamlaka ya Bunge; Kupitia taarifa za kifedha na kutoa maoni kwa Serikali kuhusu fedha za Umma; kutoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu Miswada ya Fedha; na kufanya shughuli yoyote inayohusiana na bajeti ambayo sheria nyingine inaitaka kufanya hivyo.

Sasa hapo wapi kumeelezwa kuhusu Mamlaka ya Bunge kuidhinisha ukomo wa ukopaji kwa Serikali?

Taarifa ya CAG ya Mwaka 2016/17 hakuna sehemu ambayo imeelezwa kwamba Serikali ilikopa zaidi ya 10% iliyoidhinishwa na Bunge. Kama ni kweli nitajie ni ukurasa wa ngapi wa taarifa hiyo? Bunge halitoi idhini kwa Serikali kukopa isipokua linaidhinisha ukomo wa bajeti.Ndo maana nikakuuliza sheria gani inalipa Bunge mamlaka hayo? matokeo yake umeenda kutuletea kifungu kisicho sahihi. Nilichogundua badala ya kusoma sources za taarifa uzielewe unakwenda kucopy taarifa za kina Zitto ambazo zimejaa siasa na upotoshaji.

Kuhusu Mbowe, nimekuambia CAG hajawahi kupewa taarifa za Mbowe kulipwa madeni na CDM. Alichopewa CAG ni taarifa za matumizi ya chama kwenye chaguzi. Lakini ukweli ni kwamba hizo fedha huwa analipwa mbowe kwa madai kwamba hizo fedha alitoa yeye kugharamia uchaguzi. Usichoelewa hapa ni nini?
 
Usitupangie......

Lissu ni Rais tunayemtaka
 

Wewe ndiye "mjinga" kwa kutaka kutuaminisha kuwa "URAIS" unatolewa na "mtu fulani" au "kikundi cha watu fulani" kwa vigezo vyao kama ZAWADI...

Hii imani na fikra hizi za kijinga na huu ujinga ndiyo unaopaswa kukomeshwa mwaka huu 2020...
 

Sijaelewa unachobisha ni mini; Kwamba bunge siyo butu na halitekekezi majukumu yake? Kwamba bajeti inayopitishwa na bunge haizingatiwi na serikali na bunge chini ya maspika wa CCM has a huyu wa jana Ndugai kuunga juhudi za kijinga kiaina?... Hebu sema unabishana nini na mwenzako?

Well, may be mwenzio ana argue kishabiki zaidi na hayuko subjective kwa mujibu wako....

Lakini kwako wewe pia, what is your subject? Are you really subjective?

Nikuhakikishie jambo hili, kuwa, hata wewe you are not subjective. Tena wewe ndiye unayeandika kwa ushabiki zaidi kwa mrengo wa ki - CCM na kima - Magufuli kuliko mwenzio...!!

Kama ni alama kwa kuandika kwa ushabiki kwa mrengo wa kiitikadi za kisiasa, wewe una 95% ushabiki na mwenzio 20% ushabiki kidogo....

Hata hivyo siyo ajabu hiyo, maana ndiyo maana linaitwa JUKWAA LA SIASA hili...

Kwa hiyo kila kitu siasa mtu kuvutia kwake, full ushabiki....

Twendeni hivyo hivyo, mwisho w siku KARMA itaamua nani ni nani.....
 
Unatoa uzi alafu unajibu mwenyewe acha watu wengine wajadili
 
Huu mwaka tutashuhudia mengi sana, Muda mi mwalimu mzuri tyuuuh.
 
Muda ukifika utazijua tu fikra Safi za Commander LISSU, ... au mnataka aanze kushusha nondo mapema m'copy' na ku'paste'?
😅
👊 ✌️✌️✌️💥
 
Hajatokea kiongozi anayejenga hoja kama Lissu, mtafute ndani ya CCM halafu weka mdahalo na Lissu uone mziki.
 
Sera huwa ni za chama
 
Mkuu hiyo sheria Namba 11 nililenga kifungu cha 41 (1) kwamba pesa isipotosha iwe ya mkopo au mapato ni lazima mini budget mpya iletwe bungeni. Kwahiyo kma ukikopa/kuongezewa fedha nje ya allocation bila ya kupita bungeni ni kuvunja sheria so naomba unipe sheria inayoruhusu waziri kukopa/kupewa fungu zaidi ya lililoidhinishwa bila kuidhinishwa na bunge.
Mfano bajeti ya 2017/18 wizara ya TAMISEMI iliidhinishiwa 8 Trl ila kufikia machi 2018 walipewa 17 Tri. Je huoni mamlaka ya bunge yaliporwa?

2. Pia Nmetoa provision hapo ya Public audit Act inayotoa fursa ya wizara kujibu hoja za CAG ndani ya siku 21 ila ww umedai eti fursa hiyo inapatikana ripoti ikifika kwa kamati. Je hizo siku 21 huwa mawaziri wanafanya nini? Je huoni kuwa querries za CAG mpaka kufika bungeni ni conclusive (At least kwa mipaka ya CAG) na sio provisional !!!

3. Kuhusu serikali kukopa zaidi ya ukomo bila idhini ya bunge. Kinyume na public finance act 2001 Sec. 18 (3-4) screenshot hiyo hapo ya CAF report 2016/17


4. Kuhusu Mbowe mpka ssa hujaja na kidhibiti chochote zaidi ya kelele tu ilihali hujawahi ona hta financial statement moja ya CHADEMA. Kwahiyo hearsay zako ni kelele tu bila ushahidi.

Nadhani my facts are straight mpka hpa ssa ningeomba majibu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…