Is love a decision or a feeling?

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,688
Habari za saa hizi wanajamvi,

Nina rafiki yangu moja mzuri alinena na kuniambia "mapenzi ni mazoea". Maneno hayo machache nimegundua yamebeba uzito mwingi na yana maana kubwa na pana.

Katika mapenzi yoyote mwanzoni yananoga na yanakuwa na shamrashamra nyingi, kwasababu kipya kinyemi, hamuishi kumisiana, kila mtu hamu haimuishi ya mwenzie alimradi kila kitu kinaenda kama maji mtoni.

Mnaweza hata mjiulize kwanini hatukuonana mapema. Hii ni phase ya mwanzo ya mapenzi ambayo inaitwa falling in love. Baada ya muda kama miaka kadhaa hayo mapenzi yote yanaweza yachuje mtu akikugusa unaona kero, akikupigia simu anakubughudhi na kukufatilia,yaani mnakuwa mmechokana.

Hii inakuwa phase inayofuatia ya mapenzi ambayo zile chachu zote za mapenzi zinashikiliwa na chuki na ubinafsi fulani na katika wakati huu unaweza ujiulize pia je nipo na mtu sahihi?

Yaani yale yaloyojiri mwanzo yote yanakuwa kinyume chake, kama ni ndoa unaanza kuiona chungu. Unaweza hata ufikirie pengine nikipata mwengine mambo yatakuwa kama awali ufurahie mapenzi.

Lakini nikudissappoint jibu ni hapana kwasababu hata ukipata mwengine baada ya muda fulani mapenzi yatachuja. Kwahio suluhisho ni nini? ukitaka mafanikio kwenye mahusiano yako mpende mtu ulompata/ulo kuwa nae kama ni mtu sahihi au lah kuna sababu zilizokufanya umchague yeye.

Jenga mazoea ya kumpenda yeye kama yeye, mapenzi yanahitaji wito, kujitolea, nguvu, wakati, muda na kikubwa zaidi busara. Unatakiwa kujua nini chakufanya na kwa wakati gani ili unawirishe mapenzi yako.

Usikosee katika hilo. Mapenzi ni zaidi ya hisia ni maamuzi na ni mazoea.

Au mnasemaje wenzangu?




Cc utafiti
 
Asante kwa kuniita, na asante kwa mada nzuri. Nikweli yote. sasa tunafanyaje ili hali ya KUZOEA isituchoshe?
 
Ila sio wote, me mpenzi wangu akinambia anaumwa ndio hua nazidi kumpenda
 
Yes, love is a decision. Nikiona mdada amefall in love na mwendawazimu anaeokula jalalani huyo ataniambia ni feelings. But heey, falling for a handsome guy with a nice job or promising future is a choice.

Mbona mimi I am not handsome na no promising future na ume fall ? Lol
 
Yes, love is a decision. Nikiona mdada amefall in love na mwendawazimu anaeokula jalalani huyo ataniambia ni feelings. But heey, falling for a handsome guy with a nice job or promising future is a choice.

Si unaona ehhh....unaonaje inawezekana ikawa feeling but very rare!
 
love is decision....feeling kwa mbaliii sana jaman
 
kuna vitu naviona kama
1.choice
2.decision
3.feelings
 
Falling in love is one of the biggest mistakes most people make!!!...
Even our mamas stopped loving us unconditionally, then kwa nini nimpende mtu...alafu iwe unconditional love..!!
 
Falling in love is one of the biggest mistakes most people make!!!...
Even our mamas stopped loving us unconditionally, then kwa nini nimpende mtu...alafu iwe unconditional love..!!
can you explain why it is a mistake?
 
just a few words; you don't reason out like a complete human being; you stop thinking and let someone else think for you... Yapo mengi my dearest!!
do you believe in love Eli79?have you ever loved someone?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…