Mahusiano Yasipoteze Ramani ya Maisha Yako.

Mahusiano Yasipoteze Ramani ya Maisha Yako.

Deleted01

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2018
Posts
3,886
Reaction score
9,011
Salaam to everyone,
Its my hopes that wote mna weekend njema.

Kuna jambo limekuwa likinitafakarisha sana hivi karibuni kuhusu namna sisi vijana wa kiume tunavyoendesha mahusiano yetu ya kimapenzi. Well, kuwa kwenye mahusiano sio kitu kibaya na hata kumpenda mtu kimapenzi sio kitu kibaya. Kutokuwa na kiasi kwenye mahusiano na kipindi upo kwenye mapenzi ndio kitu kibaya.

Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu (vijana wa kiume) tunapoteza uelekeo, tunafeli kiuchumi, na wengine hata kupoteza peace of mind kwa sababu tu ya kuendekeza mambo ya mapenzi kupitiliza (kutokuwa na kiasi). Hata kuachana sio tatizo and Watasha wanasema break up is not an issue, what you lose from the break up is the issue. Kama mwanaume, ukiwekeza akili na mawazo yako yote kwenye mapenzi, unakaribisha umaskini na msongo wa maisha wa kujitakia out of your own faults.

Hapa kuna mambo machache ya msingi ambayo kila mwanaume anapaswa kuyajenga kichwani mwake when it comes to mahusiano,

1. Limit your Emotional Attachment; Kwenye mahusiano ya sasa, mambo hubadilika muda wowote. Ukiona mambo yameenda tofauti, mwanamke amebadilika au amekuacha, usichukulie kama mwisho wa dunia. Usiweke hisia zako zote rehani. Kubali ukweli, nenda na wakati, na maisha yaendelee.

2. Weka Nguvu Kwenye Kutafuta Pesa; Huu ni uhalisia wa maisha ya sasa, whether you like it or not, bila kuwa vizuri kiuchumi, ni ngumu sana kulinda heshima yako kwenye mahusiano. Badala ya kupoteza masaa mengi kulalamika au kufuatilia mienendo ya mwanamke, geuza nguvu hizo kwenye kutafuta chapaa na kujenga misingi ya maisha yako. Mahusiano bila pesa yanakuwa magumu. Kama unampenda kweli, nguvu nyingi and focus zielekeze kwenye kutafuta pesa.

3. Avoid Emotional Immaturity Characters; Mchezo wa mahusiano hauhitaji hasira za kitoto au tabia ya kuzila kila mara. Kama mwanaume, unapaswa kuwa na kifua cha kuhimili misukosuko na kufanya maamuzi ya kiutu uzima bila kufuata mihemko. Mihemko achia wanawake, Be bold and ukifanya maamuzi, yasimamie. Usiwe maji vuguvugu.

4. Yatawale Mapenzi; Hapa ndipo wengi tunapofeli. Uzoee ukweli kwamba mahusiano yanaweza kuwa na changamoto, lakini usiruhusu mapenzi yakuzoeee kiasi cha kukuharibia ratiba zako, kazi zako, au malengo yako. Jifunze kuwa "detached" kiasi kwamba hata likitokea la kutokea, unajikung'uta vumbi na kusonga mbele, kwani maisha yana nafasi ya kukupa mtu mwingine mzuri zaidi mbeleni.

Wakuu, maisha ni mafupi sana kuliwa kichwa na vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti kwa asilimia mia moja. Weka focus yako kwenye maendeleo yako kwanza. Nawasilisha.

Je, mnaonaje hili suala la vijana wa sasa kupoteza ramani kwa sababu ya mapenzi? Tushauriane.
 
Mishangazi wangu hawana time simu moja tu yanasema "Nina nyege nataka kutombana unakuja au nije"
Ukiwa na shida nambie
Kwako nahitaji furaha tu
Kama una madem zako sitak niwajue wala sitak uwqsiliane nao tukiwa wote😆😆
 
Back
Top Bottom