Kama mungu yupo, muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote, kwa nini kaumba dunia ambayo ina uwezekano wa kuwa na mabaya, mateso, dhiki, etc wakati alikuwa na iwezo wa kuumba dunia ambayo hivyo haviwezekani?
Narudia tena kusema kwamba
Mungu angetaka kuumba ulimwengu ambao watu
hawafanyi maovu,basi yeye angejua kila kitu kuhusu hivyo viumbe kabla hata hayajatokea mwanzo hadi mwisho(sababu ni mjuzi wa yote).Na pia yeye ndiyo angepanga kila kitu kuhusu hao viumbe,hakuna ambacho
kingetokea pasina yeye kukitaka
kutokea,hivyo Mungu anaumba na
hufanya vile atakavyo sababu ndiyo mwenye nguvu na muweza yote. Sasa tunapokuja kwenye ulimwengu wetu ambao tunafanya maovu na mambo mengine,ni vilevile tu kwamba Mungu
anayajua yote ambayo tunayoyafanya na ambayo bado kuyafanya,Yote ambayo yanatokea ktk ulimwengu basi ni yeye(mwenye uwezo wa yote)
ndiyo ametaka yatokee hakuna
kinachotokea ambacho hakikuwa ni matakwa yake. Matakwa yake yapo aina:yapo ya aina mbili,kuna mipangilio ya kiulimwengu ambayo kama kuchomoza kwa jua na kuzama,mvu n.k(na ndiyo ktk dalili za uwepo wake), hayo yote ni matakwa yake..halafu matakwa ya aina ya pili ndiyo haya tunayofanya sisi kama hayo maovu na mengineyo,ametuacha tufanye
tutakavyo lakini ni ndani ya matakwa yake,kwa maana hiyo ambalo hatolitaka hatutoweza kulifanya.Ndiyo maana anasema kuwa anaumba na kufanya atakavyo. Nalaiti angependa hao wanaofanya maovu kutokufanya hayn maovu basi wasingefanya,kama alivyowafanya malaika.