Hapana,huwezi kutoa majibu ya kirahisi kiasi hicho. Kifo ni jambo ambalo linatambulika na kila mtu na hakuna njia ya kukwepa kifo,ni fumbo kwetu na hakuna anayejua ni lini atakumbwa na kifo,ni jambo ambalo liko nje ya uwezo wetu si jambo la kirahisi kama unavyotaka kulichukulia.
Sasa Mungu tunayejadili uwepo wake ndiye anayesema yeye ni mwenye kutoa uhai kwa kiumbe na ndiye mwenye kuchukua huo uhai(kifo). Hiyo ni sifa yake pekee hakuna mwenye uwezo kama huo.
Kwahiyo hiyo ni sifa yake kama sifa yake ya uwezo wote na ujuzi wote.
Hivyo huwezi kusema hata kidogo hili jambo la kifo liko nje ktk vitu vitakavyoweza kutusaidia kujua uwepo wa Mungu,wakati hili nalo ni jambo ambalo linyekufanya kuamini uwepo wa Mungu.