Kukariri kubaya sana..we unauliza swali unajibiwa unarudisha swali nyuma tena.
Nimeuliza, kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Jibu lake lingetoa sababu ya kueleweka, kuondoa mkanganyo wa mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye bado anaenda kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana. Huu ni mkanganyo huu, maana kimantiki mungu kama huyu angetegemewa aumbe ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, ndiyo nature yake, mazuri, si mabaya.
Lakini sijajibiwa jibu la kuondoa mkanganyo huo.
Nimepewa changa la macho tu, kwamba "mungu anaamua anavyotaka".
Hili si jibu, hili naliita ni changa la macho, kilatini "deus ex machina" unavurugwa akili kwa kutopewa jibu, unapewa fiat ukubali kwa nguvu tu.
Nikasema kusema mungu kaamua tu si jibu la swali langu.
Swali langu si nani kaamua, swali langu si mungu kaamua au hajaamua.
Swali langu ni, kwa nini mungu kaamua hivyo? Kwa nini kaamua uamuzi ambao unapingana na yeye mwenyewe alivyo?
Sijapewa jibu, naambiwa nikubali tu.
Halafu hao hao wanaosema mungu anajiamulia tu, haingiliwi, wanasema huyu mungu anapenda kuwapa watu "free will".
Eboo, sasa itakuwaje ajiamulie tu mwenyewe halafu hapo hapo tukubali kwamba anapenda "free will"?
Kila unavyozidi kufikiri unakutana na maswali yanayoonyesha kwamba hii dhana nzima ya mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni ujinga uliotungwa na binadamu tu.
Tena umetungwa na binadamu wasio na elimu, kiasi kwamba hata hii contradiction hawakuiona.
Sasa tumekuja katika the age of reason, watetezi wa huyu mungu wana kazi ya kumpachika bandeji kila anapopasuka na kutaka kuanguka under his own weight.