Is God fair ?

Is God fair ?

Hajafundishwa kujibu maswali Kiranga yeye kafundishwa ni uwezo + Upendo unaofanya Mungu afanye au asifanye jambo.

Nadhani tatizo sio Kufundishwa bali ni kule kuelewa. Kiranga anasema Hataki kuamini bali anataka kujua.
Namuuliza km yeye hataki kuamini anisaidie KUJUA Kifo ni nini!

Naona mpaka sasa hivi hajajibu.
Na huko ndiko ninako kuita kutokuelewa.
Na viumbe wa namna hii ni hatari sana kwa jamii isio na weledi wa mambo.
 
Last edited by a moderator:
Kama wewe hutaki kuamini na kila kitu kilichopo unataka kujua.
Hebu nisaidie Kujua "KIFO" ni nini?

Nipe Maana Halisi ya kifo Ambacho Hutokea Kila mara kwa viumbe hai.
Ili na mimi nijifunze kujua kila kitu
.
Na ukimaliza hili pia naomba unisaidie kujua "BUSARA au Intelligence) ni kitu gani.

Anza na hivyo viwili ambavyo UNA HAKIKA 100% kuwa vipo.

Hata nikikwambia sijui, hilo halithibitishi uqepi wa mungu.

Ninachotaka hapa ni uthibitisho kwamba mungu yupo.

Sio kusema kwamba najua kila kitu.
 
Hajafundishwa kujibu maswali Kiranga yeye kafundishwa ni uwezo + Upendo unaofanya Mungu afanye au asifanye jambo.

Hujajibu swali.

Imekuwaje mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo na upendo wote aumbe ulimwengu unaowezekanika kuwa na mabaya?
 
Last edited by a moderator:
Nadhani tatizo sio Kufundishwa bali ni kule kuelewa. Kiranga anasema Hataki kuamini bali anataka kujua.
Namuuliza km yeye hataki kuamini anisaidie KUJUA Kifo ni nini!

Naona mpaka sasa hivi hajajibu.
Na huko ndiko ninako kuita kutokuelewa.
Na viumbe wa namna hii ni hatari sana kwa jamii isio na weledi wa mambo.

Nimeshakujibu kwamba sijui, na hilo halithibitishi kwamba mungu yupo.

Uwepo wa mungu ndiyo suala la msingi, Kiranga hajawahi kusema anajua kila kitu kwa hiyo akikwambia hajui kitu hutakiwi kuahangaa.

Swali lako limekosa mantiki.
 
Last edited by a moderator:
God is Very fair my good friend.
You can't blame God For the faults of the creation.
Human beings are Nasty animals.
They tend to be very selfish, arrogant and Evil.

You can't blame a President for the Faulty of a Citizen! Can you?

Mungu katuwekea Free will. Tuishi tupendavyo.

Wewe kwesho ukiamua Kuwa muungwana thats good for you and the Society around you.

Lkn ukiamua kuwa jambazi huo ni uamuzi wako na hakuna wa kukuingilia ispokuwa Mkono wa sheria na vinginevyo.

Na mwisho wa siku Utakuja hukumiwa.

Hope you understand.

If god is very fair, and he has all powers and all love, why did he create a world in which unfairness is possible?
 
Kwa nini mungu muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote aumbe ulimwengu ambao kiumbe wake anaweza kuwa mwizi na kupigwa wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao wizi hauwezekaniki?

Ni swali lako la kijinga la siku zote, Ni sawa na kumlaumu mtu kwamba amefeli mtihani hali ya kuwa unachoelewa wewe ni kwamba hajafanya kabisa huo mtihani.
 
Ni swali lako la kijinga la siku zote, Ni sawa na kumlaumu mtu kwamba amefeli mtihani hali ya kuwa unachoelewa wewe ni kwamba hajafanya kabisa huo mtihani.

Hapana,

Unaacha kuongelea suala la kwamba kuna aliyeweka huo mtihani ambaye ana nguvu zote, uwezo wote na upendo wote.

Kama kuna mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini awape viumbe wake mitihani ambayo watashindwa kuikabili wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ama viumbe wake wanafaulu mitihani yote au hamna mitihani kabisa?

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote mitihani itamsaidia nini?
 
Ndiyo athari ya kukariri hiyo ambayo inakupunguzia hadi uelewa wa mambo.
Wapi nilipotaja mitihani ya Mungu?au nioneshe neno lenye kuashilia hivyo?

Wewe haukubali kwamba Mungu ndiyo aliyeumba huu ulimwengu, lakini unakuja kuhoji kwamba mbona Mungu kafanya hivi mara vile kwenye huu ulimwengu,ilitakiwa kwanza tuthibitishiane kuhusu upatikanaji wa huu ulimwengu maana huko ndiyo kiini cha haya yote.
 
Ndiyo athari ya kukariri hiyo.

Kati yangu ninayetoa maswali kwa habari za mapokeo na kukariri vitabu vya dini, na wewe unayeshindwa kuyajibu maswali hayo nani anakariri?

ambayo inakupunguzia hadi uelewa wa mambo.

Kama kweli una uelewa wa mambo mbona maswali yangu hunijibu?

Wapi nilipotaja mitihani ya Mungu?au nioneshe neno lenye kuashilia hivyo?

Hata mfano wako mwenyewe huuelewi. Ukishatoa habari ya kufananisha matatizo ya maisha kuwa sawa na habari ya mtihani kwa mwanafunzi, umeshafananisha aliyeruhusu matatizo hayo na aliyeruhusu mtihani kwa wanafunzi.

Kwa wanafunzi mtihani unaletwa nawalimu wasio na uwezo wote wala ujuzi wote wala upendo wote, hivyo ukiuliza kwa nini wanaleta mitihani, wanaweza kusema wanataka kufundisha.

Huyo mungu anayeleta matatizo (sawasawa na mitihani) kashindwa vipi kufundisha viumbe vyake bila matatizo wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Wewe haukubali kwamba Mungu ndiyo aliyeumba huu ulimwengu,

Nitakubali vipi kabla ya kunijibu swali langu?

Imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aende kuumba ulimwengu ambao unawezekanika kufanyika mabaya ya kila aina?

lakini unakuja kuhoji kwamba mbona Mungu kafanya hivi mara vile kwenye huu ulimwengu,ilitakiwa kwanza tuthibitishiane kuhusu upatikanaji wa huu ulimwengu maana huko ndiyo kiini cha haya yote.

Kiini cha yote ni uwepo wa mungu.

Uwepo wa mungu unaweza kupimwa kwa kuangalia nature yake mungu na kuilinganisha na dunia iliyopo.

Nature yake mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote.

Mungu kama huyu ana uwezo wa kuumba ulimwengu wowote, hata ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki.

Ulimwengu tunaouona mabaya yanawezekanika.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kiasi kwamba aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniki, kwa nini hakuumba ulimwengu huo na kaumba huu ambao mabaya yanawezekanika?

Hujajibu swali hili.
 
Nimeshakujibu kwamba sijui, na hilo halithibitishi kwamba mungu yupo.

Uwepo wa mungu ndiyo suala la msingi, Kiranga hajawahi kusema anajua kila kitu kwa hiyo akikwambia hajui kitu hutakiwi kuahangaa.

Swali lako limekosa mantiki.

Kama wewe hujui KIFO ni nini! Kitu ambacho kinatokea mbele ya macho ya walimwengu kila siku.
Vipi utaweza kutambua MUNGU NI NANI?

Na kumbe juu ya wewe kusema kuwa Hutaki Kuamini bali unataka kujua Pia Hapa UNAKUBALI KUWA HUJUI Kifo ni nini Lkn UNAKUBALI KUWA KIPO!

Huoni km unajichanganya Mwenyewe Rafiki kiranga?

Hebu jisome maneno yako kidogo huenda ukapata weledi bila tabu.
 
That is HIS choice my friend.

Hujajibu swali.

Swali si "whose choice is that?".

Swali ni "why did god make that choice?"

Kama hujui sema tu, sijui.

Jibu ambalo litamaanisha kwamba humjui mungu wako.

Jambo ambalo litamaanisha huenda hayupo ni maruweruwe tu unayoyaamini.
 
Kifo kina uhusiano gani na mungu?

Unaweza kuthibitisha uhusiano wowote kati ya kifo na mungu?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo at all?
 
Kiranga Usichagulie watu namna ya kujibu.

Wewe unapoamua Kujisaidia bila kujisafisha nani ana haki ya kukuuliza KWANINI umefanya hivyo?

Mungu ANAPOFANYA maamuzi yake WEWE na mimi Hatuna Uwezo wwt wa KUMUULIZA ni Kwanini KAAMUA alivyoamua.

Maswali yako Yanaonyesha Dalili za kukosa hoja ya maana hapa.

Jipange kidogo rafiki.
Hili swali lako la "KWANINI MUNGU AAMUE HIVYO" Halina Maana hatta kidogo.
 
Kifo kina uhusiano gani na mungu?

Unaweza kuthibitisha uhusiano wowote kati ya kifo na mungu?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo at all?

Swali unauliza wewe halafu kabla ya kujibiwa Unauliza swali lingine.

Wapi nimetaja kuwa kifo kinahusiana na Mungu?
Hebu nionyeshe na mimi nijifunze kwako.

Au umekosa Hoja baada ya Kupata majibu ya hakika?
 
Kiranga Usichagulie watu namna ya kujibu.

Wewe unapoamua Kujisaidia bila kujisafisha nani ana haki ya kukuuliza KWANINI umefanya hivyo?

Mungu ANAPOFANYA maamuzi yake WEWE na mimi Hatuna Uwezo wwt wa KUMUULIZA ni Kwanini KAAMUA alivyoamua.

Maswali yako Yanaonyesha Dalili za kukosa hoja ya maana hapa.

Jipange kidogo rafiki.
Hili swali lako la "KWANINI MUNGU AAMUE HIVYO" Halina Maana hatta kidogo.

Kabla ya kusema "mungu anapofanya maamuzi yake..." thibitisha kwamba mungu yupo kwanza.

There is such a thing as putting the horse before the cart.

Kitu chenye mjadala hapa ni uwepo wa mungu.

Unatakiwa uthibitishe uwepo wa mungu.

Unathibitishaje kwa kusema "mungu anapofanya maamuzi yake wewe na mimi hatuna uwezo wa kumuuliza" wakati hata hujathibitisha kwamba yupo?

Vipi kama hiyo habari yako nzima ni changa la macho lililotungwa na binadamu tu, wakakwambia "mungu anapofanya maamuzi yake mimi na wewe hatuna uwezo wa kumuuliza" ili kulinda siasa zao?

Kama hatuna uwezo wa kumuuliza mbona mimi nishauliza swali hilo?
 
Hata nikikwambia sijui, hilo halithibitishi uqepi wa mungu.

Ninachotaka hapa ni uthibitisho kwamba mungu yupo.

Sio kusema kwamba najua kila kitu.

Where's your arguments and evidence? ...or were you lying - like the other diabolical 16 non theists who lied about having arguments and evidence when they had none?
 
Swali unauliza wewe halafu kabla ya kujibiwa Unauliza swali lingine.

Wapi nimetaja kuwa kifo kinahusiana na Mungu?
Hebu nionyeshe na mimi nijifunze kwako.

Au umekosa Hoja baada ya Kupata majibu ya hakika?

Mara tu ushasahau ulichoandika?

Au ubongo wako hauna uwezo wa kujua kwamba umetaja uhusiano wa kifo na mungu?

Uzuri wa JF kila kitu kipo hapa, maandishi.

Umeandika

Kama wewe hujui KIFO ni nini! Kitu ambacho kinatokea mbele ya macho ya walimwengu kila siku.
Vipi utaweza kutambua MUNGU NI NANI?

Na kumbe juu ya wewe kusema kuwa Hutaki Kuamini bali unataka kujua Pia Hapa UNAKUBALI KUWA HUJUI Kifo ni nini Lkn UNAKUBALI KUWA KIPO!

Huoni km unajichanganya Mwenyewe Rafiki kiranga?

Hebu jisome maneno yako kidogo huenda ukapata weledi bila tabu.

Hapo nilipoweka bold umehusisha kujua kifo ni nini na kutambua mungu ni nani.

Nimekuuliza, uhusiano wa kifo na mungu uko wapi?

Kwa nini utegemee nijue kifo ni nini kabla ya kumjua mungu?

Na je, unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?
 
Kama yupo basi hayuko na hajawahi kuwa fair na haitakaa itokee aiseee.
 
Mara tu ushasahau ulichoandika?

Au ubongo wako hauna uwezo wa kujua kwamba umetaja uhusiano wa kifo na mungu?

Uzuri wa JF kila kitu kipo hapa, maandishi.

Umeandika

Hapo nilipoweka bold umehusisha kujua kifo ni nini na kutambua mungu ni nani.

Nimekuuliza, uhusiano wa kifo na mungu uko wapi?

Kwa nini utegemee nijue kifo ni nini kabla ya kumjua mungu?

Na je, unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Lugha inakupa tabu rafiki.

Nadhani itakuwa kazi kubwa kukufundisha lkn tutakwenda tu polepole.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom