IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

ndugu wan jf. Hivi punde kuna habari za kukamatwa kwa Mbunge wa Iringa Mjini,hivi polisi wa Iringa ni wa kulaumiwa au kupongezwa? Wakati ukijadili weka karibu Kumbukumbu za Mwandishi Mwangosi kuwawa tena mbele ya RPC. Asanteni
 
Pole kaka,fuatili utujuze,maana nna mshkaji yupo hapo Iringa ananiambia kuwa watu 3 wamekufa.

Duu! Very sad news aisee!
Kamuhanda, Lukuvi, Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa inabidi wawajibishwe kwa kukosa busara.

Namkumbuka sana kamanda Saimoni Siro kwa busara zake, alikua Mwanza mwaka 2010 na aliepusha umwagaji damu baada ya CCM kubwagwa majimbo ya Nyamagana na Ilemela.
 
haaaa!kama mnakubaliana kwenye kikao ila mawazo yenu yanapuuzwa kwajiri ya uchache wenu wazani nini kifanyike?unaijua Iringa vzzr bila shaka?kwann wapeleke machinga mlandege wakati kuna maeneo mengi tu ya jirani na mji?kwann wasiwapeleke pale uwanja wa mwembetogwa njia ya kuendea mkwawa?pia kumbka watu hawa wanataka sehemu ya kutumia kwa siku moja tu ya jumapili,kitu ambacho mikoa mingi kinafanyika, tatizo nali liona mimi viongozi wetu wengi wakipewa ushauri hata km ushauri ni mzuri,ila aliesema ni mpinzani basi wao watapuuza kisa tukifuata tutampa umaarufu.sasa mwisho wasiku haya yanatokea mkuu.watu walishatoa angalizo toka jana.kua mkumpuuza Msigwa itakua fujo wakaona tusipo peleka polisi itaonekana tumemwogopa,ona sasa mnatesa hata wasio na biashara then kesho mnataka hao nao wawaunge mkono?akili ndogo aiwez endesha akili kubwa hata cku moja

naifahamu sana Iringa,nimezaliwa hapo,nimeishi hapo na bado nitaendelea kuwa na Iringa moyoni mwangu,mkuu hebu piga picha tu pale maeneo ya miyomboni jinsi ilivyo,halafu uende hapo mashine tatu na jinsi barabara za iringa zilivyo nyembamba,sasa leo hii ukisema uruhusu wamachinga wafanye biashara kila mahali kweli tutaweza kupita iwe kwa miguu hata magari?stendi ya pale miyomboni magari yanapata tabu sana kupaki na kutoka kutokana na msongamano wa hao machinga.Mlandege sio mbali sana na katikati ya mji tena ni eneo ambalo halina msongamano wakienda kule watapata tu wateja,tatizo lililopo hapa ni mazoea na wala si vinginevyo.
 
Wewe inaonekana unakula na kulala bure kwa (baba au shemeji)yako,ungekuwa umeshakutwa na oparation Ccm,ungejua kwa nini wamachinga wanadai haki yao kwa nguvu,haki haiombwi ndugu,na muda umewadia,taratibu Tanzania inaambukizana kuifuta dhambi ya UOGA,Asante MAKAMANDA wa CHADEMA.

Hongera sana kwa kuishi kwako na unayekula kwa kujilipia,ila kumbuka hoja hujengwa kwa hoja,haya ndio mawazo ambayo huwa tunasema ni mgando siku zote,hebu tuambie wewe unaishi kwa nani?halafu utambie ni operesheni gani iliyokukumba?je kuishi na kula bure kwa wazazi/shemeji kama unavosema wewe hakumruhusu mtu kujenga hoja zake?basi niseme sawa,mbona mimi ninayeishi na kula bure kwa baba/shemeji sina mawazo mgando kama wewe,anyways ngoja niishie hapo maana sijazoea majibizano yasiyo na msingi mkuu,jumapili njema mkuu na pia ukumbuke MJENGA NCHI NI MWANANCHI NA KINYUME CHAKE NI SAHIHI KABISA.
 
Tanzania ukidai haki yako we ni mvunjifu wa amani... ipo siku tutafika!
 
Kazi ipo!
Ni lini polisi wataelewana na raia wa kawaida?
Lazima ifike kipindi Said Mwema akae na watu wake ili waweze kuendesha nchi.
Hizi ni dalili za kukosa weledi wa kuongoza na kulinda raia wake!
Shame on you.

Hata kama akikaa haitasaidia kwani inaonyesha mwema kashindwa hasa anapokubali kutumika kisiasa badala ya kusimamia sheria na wajibu wake
 
Kamanda Kamuhanda piga kazi kamanda kwa uhakika usiwe na huruma wala upendeleo na wahalifu pamoja na wavunjivu wa amani, lakini pia usirudishwe wala kuvunjwa moyo na maneno maneno ya watu, katika tukio hilo wahusika wakamatwe na kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na wasiohusika waachie wakaendelee na shughuli zao. msimuonee mtu kamanda piga kazi mzee
 
Jimbo la CHADEMA ndio maana wanafanya hivyo hawa polisi wapuuzi

Naweza kukubali ulichoandika kwani ukifuatilia majimbo polisi wanayokomaa na machinga kama hivyo ni majimbo ya CDM, kama Mbeya walikolianzisha na kushindwa kulizima na kwingineko kwingi
 
Mbona Dodoma wamejaa mjini, stend nayo popote baada ya kugoma kwenda nanenane?

Hata k.koo wamejazana hata waenda kwa miguu kwenda ni kazi, polic jamii walowekwa wanapita kukusanya rushwa na kwenda kuzitumia huku wamachinga wakizifunga barabara
 
tatizo kubwa la nchi yetu ni ccm....ambayo inajaribu kutumia polisi kama chambo,tumejua hujuma zao....na tunako elekea tuta anza kuzoea mabom.....na tukizoea hayo mabomu nchi hii haita kalika....
 
Kamanda huwa anapeleka mshiko kwa Nchimbi nadhani,why hatolewi hapo Iringa!?
 
Kamanda Kamuhanda piga kazi kamanda kwa uhakika usiwe na huruma wala upendeleo na wahalifu pamoja na wavunjivu wa amani, lakini pia usirudishwe wala kuvunjwa moyo na maneno maneno ya watu, katika tukio hilo wahusika wakamatwe na kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na wasiohusika waachie wakaendelee na shughuli zao. msimuonee mtu kamanda piga kazi mzee

Umetumwa?
 
Masikini vijana wa Tanzania. Nani atawatetea?

Kura yao ndiyo ya kuwatetea ila wakibaki kushabikia pasipokujiandikisha kupiga kura na kupiga kura yao ya kuwakataa hawa wanaowafanyia hivi basi tutegemee vijana ndo tutabaki kuyaishi haya maisha huku hawa wazee na vigogo walioko madarakani wakiwaandalia vitukuu vyao akiba............
 
Vijana wa Iringa komaeni kama wa Mbeya heshima itakuwepo.
 
naifahamu sana Iringa,nimezaliwa hapo,nimeishi hapo na bado nitaendelea kuwa na Iringa moyoni mwangu,mkuu hebu piga picha tu pale maeneo ya miyomboni jinsi ilivyo,halafu uende hapo mashine tatu na jinsi barabara za iringa zilivyo nyembamba,sasa leo hii ukisema uruhusu wamachinga wafanye biashara kila mahali kweli tutaweza kupita iwe kwa miguu hata magari?stendi ya pale miyomboni magari yanapata tabu sana kupaki na kutoka kutokana na msongamano wa hao machinga.Mlandege sio mbali sana na katikati ya mji tena ni eneo ambalo halina msongamano wakienda kule watapata tu wateja,tatizo lililopo hapa ni mazoea na wala si vinginevyo.

mkuu nashukuru kusikia kuwa wewe ni mwana Iringa ila hujajibu hoja yangu.mvutno haujaanza leo na machinga mlandege walishakwenda wakadai hakuna biashara na ndio maana wamerudi mjini,sasa kwa nn wasikae chini kuona wapi ni sehemu sahii mlandege c mbali kweli ila kwa mtazamo wa kibiashara mlandege ni mbali mkuu tena sana.vp kuhusu kuwapeleka hapo mwembetogwa pana ugumu gani?unadhani kulikua na sababu ya kutumia mabomu leo kwa issue iliyokua toka jana inajilikana tukifanya hivi iatakua hivi?
Msigwa mnamwonea bure maana kilichofanyika na viongozi wenu ni sawa na mtu kuomba ushauri huku unae mwomba ushauri unamwambia sitaki unishauri hivi.uwezi kutana na viongozi wa machinga na Mbunge alafu unawambia mimi ndio nasema itakua hivi asiefata ataona cha mtemakuni sasa hapo unatafuta suluhu au unatumia ubabe?unajua kunawatu wanaishi na kusomesha kwa biashara izo?tujifunze kufuata ushauri na kusikiliza nguvu azito tusaidia na hii ali itafika hatua itazoeleka sasa hapo ndipo utaja sikia usio yategemea maana watu wakishakua sugu na haya matukio tegemea hawatarusha tena mawe ila watajifunza kujiami iwe kwa mabomu ya kitengeneza ama la!tusipuuze ujinga wa viongozi wa chache wasiotaka kushaurika kisa tutampa Msigwa umaarufu kwa kufata ushauri wake.tukumbke tukifata ushauri wake na tukafanikiwa sifa ni ya mkoa wote na si yeye pekee mkuu.
 
Back
Top Bottom