IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

Machinga wanataka barabara zifungwe wao wafanye biashara katika barabara hizo na mbunge msigwa anasuport hili, je sheria inaruhusu kufunga barabara kwa ajili ya wamachinga kufanya biashara?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

kwani hao machinga wamekuja stand kwenye uongozi wa msigwa tu? ccm wanatumia dola kuwanyanyasa machinga kwa kuwa wanajua vijana ndo walio ipigia kila chadema. mia
 
Ndugu wana jf. Kulingana na vurugu za machinga zilozo tokea, Tunisia. Mwanza, Mbeya na sasa Iringa ninajiuliza maswali mengi lakini kubwa ni je machinga hawa wangekuwa na mabomu wangechoma matairi barabarani badala ya kuyalipuwa mabom? Wangekuwa na Bunduki wangerusha mawe badala ya risasi. Kwanini viongozi wanapo shindwa kushawishi pia wanashindwa kukubaliana na wamachinga, ili asala na madhara yanayo jitokeza baada ya vurugu visitokee. Ndugu zangu Tunisha ilikuwaje.? Mwanza ilikuwaje? Mbeya ilikuwaje? Na sasa Iringa itakuwaji.? MUNGU atusaidie kupata majibu ya maswali yote tunayo jiuliza.
 
kwanini wasingekaa kutafuta njia nzuri na muafaka wa kutatua tatizo la wafanyabiashara hawa,Mchungaji Msigwa una mamlaka gani ya kuamuru wamachinga kurudi kwenye maeneo ambayo yamekatazwa?Hivi ubunge ni kufanya kile unachojisikia na kinyume na taratibu na sheria tena ambazo wewe kama mbunge na diwani umeshiriki kuzitunga?.Polisi waache wafanye kazi yao na wala wasilaumiwe wa kulaumiwa hapa ni mchungaji msigwa kwa kuwa chanzo cha tatizo.

Ifike wakati lazima watanzania tuwe tunasapoti mambo ya msingi na si kushabikia kila jambo hata kama ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.Mimi na wewe tumekaa nyuma ya pc zetu na kuandika kila aina ya maneno wakati wale ambao tunawajaza ujinga wana taabika kwa kupigwa mabomu,wengine kufariki na hata wale wasio na makosa wanaingia katika adha hii.Wito wangu kwa Mbunge Msigwa aache kufanya mambo yeye kama kiongozi hapaswi kuyafanya,kuchochea watu kufanya vurugu huo si uongozi,kiongozi makini ni yule atakayeumiza kichwa kutafuta njia muafaka ya kuwajengea wananchi wake misingi ya kujikomboa kutoka katika lindi la umasikini.

Watu wanasifia humu kwamba wamachinga wanaelekea kuwashinda polisi,hivi hao polisi wakiona hali inakuwa mbaya si wataamua kutumia nguvu kubwa kudhibitihali hiyo?mwisho wa siku ikitokea watu/mtu kadhuriwa vibaya utasikia humuhumu kwenye jukwaa watu wakisema ooh polisi wanatumia nguvu kubwa,mara wametumwa...jamani tusiwe watu wa kupenda mambo ya ajabu.

Kwangu mimi madhara yoyote yatakayotokea Iringa leo mtun wa kwanza kumlaumu itakuwa Mchungaji Msigwa (Mb.Iringa Mjini)

(IRINGA MY DREAM LAND)

haaaa!kama mnakubaliana kwenye kikao ila mawazo yenu yanapuuzwa kwajiri ya uchache wenu wazani nini kifanyike?unaijua Iringa vzzr bila shaka?kwann wapeleke machinga mlandege wakati kuna maeneo mengi tu ya jirani na mji?kwann wasiwapeleke pale uwanja wa mwembetogwa njia ya kuendea mkwawa?pia kumbka watu hawa wanataka sehemu ya kutumia kwa siku moja tu ya jumapili,kitu ambacho mikoa mingi kinafanyika, tatizo nali liona mimi viongozi wetu wengi wakipewa ushauri hata km ushauri ni mzuri,ila aliesema ni mpinzani basi wao watapuuza kisa tukifuata tutampa umaarufu.sasa mwisho wasiku haya yanatokea mkuu.watu walishatoa angalizo toka jana.kua mkumpuuza Msigwa itakua fujo wakaona tusipo peleka polisi itaonekana tumemwogopa,ona sasa mnatesa hata wasio na biashara then kesho mnataka hao nao wawaunge mkono?akili ndogo aiwez endesha akili kubwa hata cku moja
 
Tatizo ni huyo mbunge, atawaruhusuje watu waende kufanya biashara eneo ambao limekatazwa? Alijua akifanya hivyo lazima vurugu itatokea kati ya halimashauri na wafanyabiashara, huo ni uchonganishi na vurugu inapotokea polisi kazi yake ni kuja kutuliza na kurudisha hali ya amani. Tuache mambo ya kisiasa katika suala la amani
 
kwanini wasingekaa kutafuta njia nzuri na muafaka wa kutatua tatizo la wafanyabiashara hawa,Mchungaji Msigwa una mamlaka gani ya kuamuru wamachinga kurudi kwenye maeneo ambayo yamekatazwa?Hivi ubunge ni kufanya kile unachojisikia na kinyume na taratibu na sheria tena ambazo wewe kama mbunge na diwani umeshiriki kuzitunga?.Polisi waache wafanye kazi yao na wala wasilaumiwe wa kulaumiwa hapa ni mchungaji msigwa kwa kuwa chanzo cha tatizo.

Ifike wakati lazima watanzania tuwe tunasapoti mambo ya msingi na si kushabikia kila jambo hata kama ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.Mimi na wewe tumekaa nyuma ya pc zetu na kuandika kila aina ya maneno wakati wale ambao tunawajaza ujinga wana taabika kwa kupigwa mabomu,wengine kufariki na hata wale wasio na makosa wanaingia katika adha hii.Wito wangu kwa Mbunge Msigwa aache kufanya mambo yeye kama kiongozi hapaswi kuyafanya,kuchochea watu kufanya vurugu huo si uongozi,kiongozi makini ni yule atakayeumiza kichwa kutafuta njia muafaka ya kuwajengea wananchi wake misingi ya kujikomboa kutoka katika lindi la umasikini.

Watu wanasifia humu kwamba wamachinga wanaelekea kuwashinda polisi,hivi hao polisi wakiona hali inakuwa mbaya si wataamua kutumia nguvu kubwa kudhibitihali hiyo?mwisho wa siku ikitokea watu/mtu kadhuriwa vibaya utasikia humuhumu kwenye jukwaa watu wakisema ooh polisi wanatumia nguvu kubwa,mara wametumwa...jamani tusiwe watu wa kupenda mambo ya ajabu.

Kwangu mimi madhara yoyote yatakayotokea Iringa leo mtun wa kwanza kumlaumu itakuwa Mchungaji Msigwa (Mb.Iringa Mjini)

(IRINGA MY DREAM LAND)

Wewe inaonekana unakula na kulala bure kwa (baba au shemeji)yako,ungekuwa umeshakutwa na oparation Ccm,ungejua kwa nini wamachinga wanadai haki yao kwa nguvu,haki haiombwi ndugu,na muda umewadia,taratibu Tanzania inaambukizana kuifuta dhambi ya UOGA,Asante MAKAMANDA wa CHADEMA.
 
Ndugu wana jf. Kulingana na vurugu cha machinga zilozo tokea, Mwanza, Mbeya na sasa Iringa ninajiuliza maswali mengi lakini kubwa ni je machinga hawa wangekuwa na mabomu wangechoma matairi barabarani ya kuyalipuwa mabom? Wangekuwa na Bunduki wangerusha mawe badala ya risasi. Kwanini viongozi wanapo shindwa kushawishi wanashindwa kukubaliana na wamachinga ili asala na madhara yanayo jitokeza baada ya vurugu visitokee. Ndugu zangu Tunisha ilikuwaje.? Mwanza ilikuwaje? Mbeya ilikuwaje? Na sasa Iringa itakuwaji.? MUNGU atusaidie kupata majibu ya maswali yote tunayo jiuliza.
 
Tanzania tunaelekea wapi?,ina maana sie ni wasafi kuliko wachina,wathailand?ambao serikali zao zimeruhusu ufanywaji wa biashara ndogo ndogo mitaani?,huku wakikusanya kodi na mapato toka kwa wafanyabiashara hao!.Ila haya ndo matokeo ya uongozi mbovu,usokuwa na watu wenye upeo wa kufikiri kwa kina na kupanga,uongozi ulojaa ubabe na unyonyaji dhidi ya raia,uongozi unachukulia mambo kinyume kwa maana kwamba,palipo na uhalali panawekwa uharamu.!
 
Kuweni Makini sana na Kamuhanda , hachelewi kurusha vitu vyenye NCHA KALI !
 
Hivi huyo mbunge ana matatizo gani?, anapata nini sasa watu wakiishi kwa hofu
 
Wanacho kifanya poliCCM hapo Iringa mjini, mie nachukulia poa tu, kwani wana tujengea chama chetu (CHADEMA) kwa kasi ya ajabu tena kwa gharama nafuu.

Hivi Iringa nayo imekuwa kasikazini ?

Huko ni kujenga chama,au kukibomoa?maana hizi vujo zinazosababishwa na uvunjaji wa sheria,mimi naona zinaipotezea credits chadema.mpaka sasa umeishakuwa wimbo kuwa chadema ni chama cha vurugu.sasa km mbunge ataongoza watu kuvunja sheria na kufanya vujo,kweli huko si kuuambia umma kuwa sisi ni watu wa fujo.
 
Tatizo serikali inapenda kulazimisha mambo,yapaswa kuangalia mazingira ya kufanyia biashara je yanaruhusu? Km ayakithi basi yawapasa kutengeneza miundombinu mizuri kwa ajili ya biashara kwa wamachinga.
 
.Najua hapo yupo kamuhanda hakuna busara itakayotumika,ukizingatia majuzi alisifiwa bungeni na lukuvi kwa 'kazi'nzuri anayoifanya.

Hapo ndipo Jeshi la polisi na intelijensia ya kibongo utakapoitaka katika matukio kama haya na ya kumfuatilia Dr Slaa na CHADEMA lakin ukija kwenye sensitive issues lazima waje FBI. Poor Tanzania and Tanzanian
 
Huko ni kujenga chama,au kukibomoa?maana hizi vujo zinazosababishwa na uvunjaji wa sheria,mimi naona zinaipotezea credits chadema.mpaka sasa umeishakuwa wimbo kuwa chadema ni chama cha vurugu.sasa km mbunge ataongoza watu kuvunja sheria na kufanya vujo,kweli huko si kuuambia umma kuwa sisi ni watu wa fujo.

kaka upo sahihi, maana watu wana hofu kubwa huko, ujenzi gani wa chama katika hali ya kuhamasisha fujo na vurugu au kwa kufanya hivyo ndio anazani atawapata wanachama wengi? wengine wataona vyama vinawaletea fujo hivyo hawataenda kushiriki katika mambo ya kujenga chama kwa kuwa kama viongozi wao wanaamini wanachama wengi wanapatikana wakati wa vurugu, wajue hakuna mtu anayependa vurugu hivyo watakosa wanachama kwa mtindo huo
 
Mkuu, taarifa sijazipata maana nilitoka eneo la tukio baada ya kupata hekaheka hivyo kwa sasa bado napata huduma ya kwanza hapa geto kwa mshkaji

Pole kaka,fuatili utujuze,maana nna mshkaji yupo hapo Iringa ananiambia kuwa watu 3 wamekufa.
 
Polisi wanasema machinga wasifanye biashara mjini ila machinga wanadai watafanya...kinachoendelea stend kuu imebaki nyeupe, watu wanahaha, mabomu na risasi vinarindima

Ukisha zowea kunawa na damu, huwa inakutuma kumwaga damu kila wakati. Kamuhanda damu ya Mwangisi inamsumbua anataka kumwaga nyingine.
 
Back
Top Bottom