IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

Gari la zima moto limeshambuliwa sana kwa mawe eneo la hall fare, gar la polisi limebondwa sana, matairi yamewashwa barabarani
 
serikali inaongozwa na wajinga hii. kwani pale mashine 3 hawa walalahoi wakiweka gulio lao mara 1 kwa wiki wapate fedha za kujikimu nyie manispaa mnapungukiwa nini? Na kodi wanalipa hao wafanyabiashara. anaejua kwanini wanazuiliwa naomba anijuze.
 
Wacha watembezewe kichapo ndio waujue iwepo wa serkali.
 
Eneo la jamati uhindini kuna magari ya raia yako hatarini kuharibiwa vibaya kutokana na mapambano makali kati ya polisi na wananchi.
 
Wamachinga wanadai kule waliko hamishiwa hamna biaasha, wateja wala miundo mbinu yoyote kiasi kwamba mitaji inakata. so wameamua kurudi eneo la stand hadi hapo serikali itakapo wajengea miundo mbinu na soko kulihamishia huko. Mch. Msigwa yupo nao sasa hivi polisi wanamtafuta. amesema hadi kieleweke. machinga wanamlinda kama rais kiasi kwamba polisi pamoja na kuziba njia zote/kumzunguka hadi sasa hajakamatwa. Muda si mrefu ataongea na vyombo vya habari. wamachinga wamesema wawamalize kwanza ndo wamshikw. mia

Nimeipenda hiyo mkuu.

The nation that destroys its destroys itself.
 
sababu za kukatazwa ni nini? hilo ndio swali la msingi. sio tu kisa uongozi wamesema. Nchi yao au yakwetu sote? Wako kwa ajili ya maslahi yao au ya wananchi sote. Kuwa na gulio pale kunamuathiri nani na kivipi kama sio ubabe wa kijinga wa CCM eti kuwakomesha. Watajikomesha wenyewe!
 
Barabara kuu itokayo Iringa mjini eneo la mshindo hali ni mbaya, matairi yanawaka, mabomu yanarindimb, watu wako ktk hekaheka...
Nikukumbushe tu ndugu msomaji wa jf kua mimi ni Skype naripoti tukio hili moja kwa moja toka Iringa mjini.
 
Last edited by a moderator:
Leo ni jumapili, nilikuwa nategemea huyo mchungaji awe kanisani sasa hivi!! Lakini matokeo yake yupo busy kuhatarisha usalama na amani ya nchi. Poor mchungaji, poor chadema!!
we p.imbi hiyo misa itasalika vipi wakati mtaani wapo raia wema wanaonyanyaswa na mapolice-CCM?au wewe unawachukulia wamachinga kama wakimbizi? Nyie magamba msipende kusahau kuwa hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho.
 
Leo ni jumapili, nilikuwa nategemea huyo mchungaji awe kanisani sasa hivi!! Lakini matokeo yake yupo busy kuhatarisha usalama na amani ya nchi.

Poor mchungaji, poor chadema!!

Imeandikwa ni nani awezaye kuacha kumwokoa ng'ombe wake aliyeingia ndani ya shimo kwa ajili ya siku ya sabato?
Usiwe mshabiki tatizo hamtaki kukubali kua mda umewakataa na ndio maana hata mfanye nn linazuka jipya.mda wenu umekwisha na mkiendelea pingana na mda mtaumia zaidi acheni mda uamue unataka nn mkuu.haijawai tokea mtu akaushinda mda ndio maana hata 'mwana wa Adamu mda ulipo fika alitundikwa msalabani na mda ulipo timia akafufuka'km shule ipo changanua kauli iyo utapata maana maana waswahili usema asiejua maana..........na siku nyingine usimwamshe alie lala maana ..............CCM BANA.
 
Tahadhari imetolewa kwa wananchi wote walioko makanisani, madukani, mahotelini, sokoni, majumbani au popote walipo wasitoke mpaka pale hali ya utulivu itakaporejea.
 
Acha umbumbumbu wewe, hakuna mwenye akili timamu ataafiki machinga kufanya biashara eneo hilo. Barabarani no way. Hizi siasa hizi zinatupeleka kusiko.

Tatizo mpaka muone wakifanya wazungu ndio na nyiemnafwata. unafahamu kitu kinaitwa flee markets?
Ile stretch ya barabara ikifungwa mara moja kwa wiki kuna hasra ipi wakati kuna access kutoka barabara kuu na hii yakuzungukia takrima. Kufunga barabara ajili ya midundiko na kukata viuno ni sawa lakini kufanya biashara....?
 
Vurugu zinaendelea hapa mjini baina wa wamachinga na polisi wa kuzuia fujo (ff). Wakati Mbunge (Mch Msigwa) ameruhusu wamachinga na wauza mitumba waendee na biashara zao, Meya wa Manispaa amezuia. Hali ni tete.
 
Gari la zimamoto limefika kuzima moto wa matairi lakin limebondwa mawe sasa liko nyang'anyang'a
 
Leo asubuh Iringa mjin si shwari .Polis na machinga hawaiv chungu kimoja baada ya mkurugenzi wa manispaa Iringa kushindwa kutumia maneno ya ushawish kwa wamachinga kuhusu sehemu ya kufanyia biashara yao. Mbunge Msigwa naye ameamua kudhihirisha kauli zake kuwa wamachinga hawawez wakaonewa yeye akiona. kwa hali ni tete shuguli zimesimama, umeme umekatwa kwa hyo ni tabu tupu.

kwanin hatujifunz kutatua migogoro kwa ushawish lazim tutumie mabom?

au kwa sababu unakuwa unalo bomu mkonon unaamua kutumia.
 
Watu mbalimbali wamekamatwa na kupigwa sana na wamepelekwa kituo cha polisi
 
Kituo cha redio cha ibon fm kinapotosha ukweli kupitia kwa ripota wao abduli kwa kusema kua eti hakuna aliyejeruhiwa
 
Jesh la polisi limeongeza gari aina ya karandinga ili kukamata watu
 
Askari wa jesh la uokoaji analalamika hapa kua gar lao limebondwa
 
Sometimes CHADEMA wanaipeleka nchi hii jehanam.
Haiwezekani ukatetea watu kufanya biashara bila kufuata utaratibu,eti kisa unataka kura zao.
Ina maana,CHADEMA ikiingia madarakani,itaendesha vipi serikali?
 
Back
Top Bottom