IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

Taratibu kijana, acha jazba.
Hamna mmachinga anayenyanyaswa na polisi. Polisi wanachofanya ni kulinda raia na mali zao, kwa case ya iringa wanazuia uvunjwaji wa amani unaosababishwa na wamachinga kupitia kwa mbunge ambaye ni mchungaji. Nilitegemea wachungaji ndio wahubiri amani, lakini kumbe siyo hivyo!
Ninashangaa sana watu mnavyoleta habari za CCM hapa, kisa mbunge wa Chadema ndio anahamasisha vurugu!!polisi wanafanya kazi yao na siyo kwa instruction za CCM!

Mkuu, post yako inathibitisha ni kwa kiwango gani umebinafsisha akili zako na kujivika upofu uliochanganyikana na ujinga. Yaani unataka kutuaminisha ya kuwa wamachinga ndo wavunjifu wa amani ? Wamachinga ndo wanalipua mabomu ovyo ? Wamachinga ndo wanafyatua risasi ovyo ?
 
Hivi mbona Dar wamachinga wanapanga bidhaa .paka njiani hawapigwi mabomu?. Nenda pale Karume,maeneo ya kariakoo,Mbagara Zakhiem,Buguruni,Ubungo mataa,Mwenge nk. Mote humo bidhaa wanapanga mpaka kwenye njia za kupita watu,na viongozi wa mitaa,jiji wapo na wanaona. Ndio maana hata vijana wa mikoani wanaona kama Dar jiji kubwa wanafanya nasi pia tufanye. Tuondoe unafki Dar kwanza ndio kunakoongoza kwa kuvunja taratibu na sheria. Tusiwe na double standards.
 
Kwa mwendo huu nchi hii siku moja itakuja kushuhudia balaa ambalo hatulitarajii,hawa vijana ambao wanakatazwa kufanya hizi biashara leo hii ndio hawa hawa ambao wanaweza kuwa majambazi na vibaka mitaani,yafaa kufikiria zaidi chanzo cha tatizo kuliko kuangalia yanayotokea sasa maana ukiangalia sehemu nyingine wanaruhusiwa iweje wao tu pale Iringa?Kuna tatizo gani kwa vijana wa Iringa kunyimwa fursa huku wengine wakipewa fursa hizo sehemu nyingine?
 
Mungu wangu! Hivi wamachinga ni aina gani ya wanyama? Mamalia, reptilia au amfibia? Hawana faida kama yule faru wa jk au yule mzungu mmoja aliyeuwawa kulee serengeti. Wakubwa hawawezi kugawana vitalu vya wamachinga. Eh jamani! Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee's!!!!!!!!!!!!
 
Huo sasa ni ujuha, sasa gari la zimamoto linahusika vipi na matatizo yao? Saa hizi wanaliponda, halafu baadaye moto unaunguza mali zao na wanaanza kulitafuta tena kwa ajili ya kuzima moto. Wehu huu jamani!

haaaaa!kwaiyo na kiongozi anae uza madini na wanyama nnje ya nchi yake kwa bei ya hasara huku mahosptalini hamna dawa,mashuleni akuna vifaa,wajawazito wanalala kitanda kimoja ama anae amrisha kubadili matokeo ya kidata cha 4.bila kutatua matatizo ya walimu kwa upeo wako yupi bora hapo?kiongozi ama huyu mwananchi anae aribu gari kuonyesha hasira zake.pia jiilize matukio ya moto mangapi yamekua solved bila hao zimamoto?TAFAKARI.usiruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa mkuu
 
Taarifa kutoka iringa:

Jeshi la polisi limezidiwa nguvu na wamachinga na sasa polisi wanatumia gas yenye harufu mbaya kwa kuipuliza gas iyo chafu kwenye mitaa ya iringa mjini hadi kwenye makazi ya watu.

Mpaka sasa wakazi wanajiziba pua zao lakini haisaidii kitu kwani gas iyo inayopulizwa kwa amri ya Kamanda Kamuhanda imekua ni gas inayoumiza mpaka watoto wadogo wanatapika na wengine wanazimia.

Kwa mujibu wa mpasha habari ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu ruaha aliyepanga nyumba maeneo ya Mwembetogwa Iringa, anasema gas hii chafu inayopulizwa inasabibisha watu wengine wanazimia na wengine wanatapika ovyo mitaani.

MY take:

Jamani Tanzania yetu imeanza kutumia mashambulizi ya kutumia mabomu ya gas yanaomiza wanadamu kinyume na haki za binadamu.
Serikali ya ccm imefika mbali.
Huu ni unyama dhidi ya binadamu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kwanini wasingekaa kutafuta njia nzuri na muafaka wa kutatua tatizo la wafanyabiashara hawa,Mchungaji Msigwa una mamlaka gani ya kuamuru wamachinga kurudi kwenye maeneo ambayo yamekatazwa?Hivi ubunge ni kufanya kile unachojisikia na kinyume na taratibu na sheria tena ambazo wewe kama mbunge na diwani umeshiriki kuzitunga?.Polisi waache wafanye kazi yao na wala wasilaumiwe wa kulaumiwa hapa ni mchungaji msigwa kwa kuwa chanzo cha tatizo.

Ifike wakati lazima watanzania tuwe tunasapoti mambo ya msingi na si kushabikia kila jambo hata kama ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.Mimi na wewe tumekaa nyuma ya pc zetu na kuandika kila aina ya maneno wakati wale ambao tunawajaza ujinga wana taabika kwa kupigwa mabomu,wengine kufariki na hata wale wasio na makosa wanaingia katika adha hii.Wito wangu kwa Mbunge Msigwa aache kufanya mambo yeye kama kiongozi hapaswi kuyafanya,kuchochea watu kufanya vurugu huo si uongozi,kiongozi makini ni yule atakayeumiza kichwa kutafuta njia muafaka ya kuwajengea wananchi wake misingi ya kujikomboa kutoka katika lindi la umasikini.

Watu wanasifia humu kwamba wamachinga wanaelekea kuwashinda polisi,hivi hao polisi wakiona hali inakuwa mbaya si wataamua kutumia nguvu kubwa kudhibitihali hiyo?mwisho wa siku ikitokea watu/mtu kadhuriwa vibaya utasikia humuhumu kwenye jukwaa watu wakisema ooh polisi wanatumia nguvu kubwa,mara wametumwa...jamani tusiwe watu wa kupenda mambo ya ajabu.

Kwangu mimi madhara yoyote yatakayotokea Iringa leo mtun wa kwanza kumlaumu itakuwa Mchungaji Msigwa (Mb.Iringa Mjini)

(IRINGA MY DREAM LAND)
 
Mkuu naskia watu 3 wamekufa,Manamke,mtoto wa miaka 9 na polisi mmoja,nikweli?

Mkuu, taarifa sijazipata maana nilitoka eneo la tukio baada ya kupata hekaheka hivyo kwa sasa bado napata huduma ya kwanza hapa geto kwa mshkaji
 
Eti polisi wapo kwa ajili ya kulinda amani,raia na mali zake!,.Unamlinda raia kwa kumpiga mabomu?,unalinda amani kwa kuhatarisha maisha ya raia?,unalinda amani kwa kuhalibu mali za wafanyabiashara,tena bila kujali mitaji duni ya mikopo walonayo?.Amani iko wapi?,ulinzi uko wapi?,hyo ndo njia sahihi ya kulinda amani na mali?.Kubali ukatae polisi ni chombo kilichogeuzwa kuwa kandamizo la wanyonge!.Mabomu,virungu,maji ya pilipili sio suruhisho.,bado zipo njia nyingne za kutatua migogoro ya wamachinga,sio Iringa tu,Tanzania kiujumla.
 
5_d26e3.jpg

POLISI YATUMIA NGUVU KUTAWANYA WANANCHI MTAA WA MASHINE TATU, WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MAARUFU KWA JINA LA MACHINGA WAKIWA NA MBUNGE WAO,
Wananchi wafunga Barabara na kuchoma mataili Barabalani Polisi nao wazidi kupiga mabomu huku wananchi wa kisema Pigeni yaishe tumechoshwa kunyanyaswa kwa sheria ya kuwadhibiti wadogo huku wakubwa wakikosea Sheria haipo.
 
Acha umbumbumbu wewe, hakuna mwenye akili timamu ataafiki machinga kufanya biashara eneo hilo. Barabarani no way. Hizi siasa hizi zinatupeleka kusiko.

Wanao wahonga suti mnawafuata Ulaya, vp raia wa nchi yake hana nafasi! Acheni unafiki waache wafanye biashara hata chumbani kwako cause nchi haina uongozi bali majangili.
 
Kwanin madai ya watu hayasikilizwi? Na kwanin kila panapokua na madai ya wananchi inageuzwa kua uchochezi na watetez kuwekwa ndan? Kamuhanda kama unasali hutaionja pepo
 
Tunashudia utetezi kwenye uvunjifu wa sheria....tunashuhudia utetezi kwenye uvunjaji wa haki za binadamu......hii yote ni kwa sababu sifa za kisiasa........
 
Back
Top Bottom