IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

Mtoto mdogo kazimia'na mwandish wa habari apigwa na kukamatwa na polisi wakat anajulikana anaitwa alfhan
 
5_d26e3.jpg

POLISI YATUMIA NGUVU KUTAWANYA WANANCHI MTAA WA MASHINE TATU, WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MAARUFU KWA JINA LA MACHINGA WAKIWA NA MBUNGE WAO,
Wananchi wafunga Barabara na kuchoma mataili Barabalani Polisi nao wazidi kupiga mabomu huku wananchi wa kisema Pigeni yaishe tumechoshwa kunyanyaswa kwa sheria ya kuwadhibiti wadogo huku wakubwa wakikosea Sheria haipo.

Kweli jpili hadi wewe umeandika hivyo!
 
Tatizo la Iringa manispaa ni kua na madiwani wazee, wasio na elimu ndo maana bado tunaendelea kuendesha mji kwa mawazo ya kimgando. Mbona hapa Mafinga leo jumapili hii barabara ya kutoka NMB kuja hadi sokoni imefungwa na wamachinga wanafanya biashara hakuna gari kupita. Wanachoogopa viongozi wa iringa ni kua wakiruhusu tu wamachinga wafanye hapo biashara watakua wamempa umaarufu msigwa na CHADEMA. Tangu lini mkawapeleke wamachinga Kitwiru kwenye nyumba za kuhesabu eti ndo eneo la biashara? hayo ni mawazo mgando sana tena hapo utakuta katika kikao cha maamuzi alikuwemo na Mchumi na afisa biashara wa manispaa.
 
Ni fujo, mamlaka husika zimeshatoa maelezo ni sehemu gani za kufanyia biashara na ni sehemu gani haziruhusiwi! Kwanini wewe upingane na mamlaka? Kuna taratibu za kupinga lakini siyo kwa stahili hii ya CDM na ya mchungaji koko wao!

Huyu ---- akishapigwa njiti na kupewa elfu 7, anajiona amefika anaaza kubwabwaja !
 
Polisi wanafuata amri za wakubwa zao na wakubwa zao ni viongozi wa CCM ambao wapo madarakani,huwezi kumpongeza mtu ambaye anazuia wewe kupata mkate wako wa kila siku na nitashangaa kumsikia mtu yeyote aliyepo Iringa akiwapongeza Polisi kwa yale ambayo wameyafanya na wanayoendelea kuyafanya.
 
Serikali yetu mbona hawasomi alama za nyakati!!!!!
Dodoma machinga hawajahama mjini na wanaendelea bila fujo, Dar machinga walitaka kuwahamisha maeneo ya tazara kongo na mwenge lakini yote yaligonga mwamba baada ya fujo kibao na baadae wakaona wajenge machinga complex ambayo nayo ilishindwa kuzaa matunda na machinga kuendelea maeneo ya mwanzo, Mwanza yale yale.
wanawahadaa machinga wa iringa tu kwa sasa NINACHOAMINI SUBIRI UCHAGUZI UKARIBIE UONE KAMA KUNA CHINGA ATAFUKUZWA.
Ni vyema viongozi wetu kufikiria kwa kina kabla ya kuanza kusema na kufanya hayo yanayoendelea.
 
kwanini serikali ing'aninie kuwatoa wamachinga kwa majimbo yaliyo chini ya chadema tu au ndo hasira za kupingwa chini 2010!!!
 
Kuna gari mbili za ffu zikiwa zimejaa askali zinaondoka mbeya alasili hii kwenda iringa ziko kasi kwelikweli
 
Ngoja tusikie yatakayojiri huko maana naona nguvu inayotumika ni kubwa sana
 
Maneno ya sumaye yanatimia...unaingia madarakani kwa kalamu unatawala kwa mabavu maana huna uhalali
 
Mbona wameniacha?ningeenda kuongeza nguvu kwa machinga kudai haki zao,
 
Wale vijana ambao wamekosa ajira na kuamua kujiajiri huku fursa ya kufanya biashara hawaipati usidhani siku watakuja kukipenda chama kilichopo madarakani na bahati mbaya iliyopo sasa ni kuwa vijana wengi wameelimika na wanajua pumba zipi mchele upi.
 
Hao wake zao wanatibiwa hosipitali hizi hizi; na watoto wao wanasoma ktk shule hizi hizi za st Kanumba au wenzetu ni wa daraja la Apolo India na St Mrys.
Yangu macho kuna siku watagundua kuwa inavyotumiwa ile karatasi ya chooni ndivyo walivyogeuzwa na wao. Hapo ndo patakuwa pamenoga.
 
Majimbo yaliyochukuliwa na Chadema ndio majimbo yalioyoendelea kuliko yote tz
 
mkuu nashukuru kusikia kuwa wewe ni mwana Iringa ila hujajibu hoja yangu.mvutno haujaanza leo na machinga mlandege walishakwenda wakadai hakuna biashara na ndio maana wamerudi mjini,sasa kwa nn wasikae chini kuona wapi ni sehemu sahii mlandege c mbali kweli ila kwa mtazamo wa kibiashara mlandege ni mbali mkuu tena sana.vp kuhusu kuwapeleka hapo mwembetogwa pana ugumu gani?unadhani kulikua na sababu ya kutumia mabomu leo kwa issue iliyokua toka jana inajilikana tukifanya hivi iatakua hivi?
Msigwa mnamwonea bure maana kilichofanyika na viongozi wenu ni sawa na mtu kuomba ushauri huku unae mwomba ushauri unamwambia sitaki unishauri hivi.uwezi kutana na viongozi wa machinga na Mbunge alafu unawambia mimi ndio nasema itakua hivi asiefata ataona cha mtemakuni sasa hapo unatafuta suluhu au unatumia ubabe?unajua kunawatu wanaishi na kusomesha kwa biashara izo?tujifunze kufuata ushauri na kusikiliza nguvu azito tusaidia na hii ali itafika hatua itazoeleka sasa hapo ndipo utaja sikia usio yategemea maana watu wakishakua sugu na haya matukio tegemea hawatarusha tena mawe ila watajifunza kujiami iwe kwa mabomu ya kitengeneza ama la!tusipuuze ujinga wa viongozi wa chache wasiotaka kushaurika kisa tutampa Msigwa umaarufu kwa kufata ushauri wake.tukumbke tukifata ushauri wake na tukafanikiwa sifa ni ya mkoa wote na si yeye pekee mkuu.

Migogoro ya machinga na uongozi katika maeneo mbalimbali ya nchi hii hayajaanza leo wala jana,ni ya muda mrefu sana.Wamachinga wanapoondolewa na kuonyeshwa sehemu ya kwenda hupinga kwa madai kuwa hakuna biashara eneo hilo,sasa kinachotekea ni kwamba wanarudi kwenye yale maeneo ambayo walikatazwa na kuzua mtafaruku na mamlaka za nchi.

Tukiacha kila mtu afanye anachotaka katika miji yetu hakutakuwa na utaratibu tena bali vurugu,hebu fikiria leo hii iruhusiwe kuwa wamachinga ni ruksa kufanya biashara pembezoni mwa barabara,unafikiri hali itakuaje?mkuu unasema waruhusiwe kufanya biashara jumapili kwenye maeneo hayo ya barabarani na ihalalishwe barabara ifungwe ili waendelee na shughuli zao,hivi unajua ukishafanya hivo ni sawa na kuwapa ruhusa ya wao kuendelea kufanya biasahra maeneo hayo siku zote maana watasema walisharuhusiwa?

Nitakupa mfano mmoja tu😛ale ubungo mataa,songas palikuwa na wafanyabiashara wadogowadogo wengi sana pale,mwanzoni ilianza kama utani watu ikawa ikifika mida ya kuanzia saaa tisa wanaanza kujisogeza kufanya baishara maeneo yale,baadae ikawa watu wanaanza kuanzia asubuhi na mapema.Kero ikaja baada ya eneo lile ambalo sio rasmi kwa ajili ya biashara kwani ilileta msongamano mkubwa wa watu hivo kupelekea kuwa na foleni na adha nyinginezo,lakini baada ya kuwaondoa lile eneo limekuwa safi sana na wala hakuna bugudha yoyote ile.

sasa leo tukiwaruhusu hapa Iringa wafanye biashara wanavyotaka itakua vurugu sana na ukumbuke Iringa mjini ni eneo dogo sana.Ninachoomba mimi mipango miji izingatiwe na kila mmoja wetu atimize wajibu wake.
 
Back
Top Bottom