IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

IRINGA: Vurugu, Machinga na Polisi wapambana

Jamani Kamuhanda akuua tena leo?

Tiba
 
huu ujinga unatakiwa tuupige kwa nguvu zote nje ya hapo ccm watatutia madole
 
Tunaomba wanasheria wa CDM mtufafanulie sheria ya kukamatwa mbunge imekaaje,wapi,lini,wakati gani na kwa kosa gani? maana tumeshuhudia wabunge mbalimbali wa CDM wakikamatwa na kulala rumande kwa makosa ya kitoto kabisa.Mbona JK aliwasamehe wezi wa epa walioiba mabilioni ya UMMA?mambo mengine yanatia hasira kwelikweli...
 
Staili yao ndio ile ile kama ukweli ingetumika kwa wahujumu uchumi taifa letu lingekuwa kama ulaya
 
Mtaa wa Kongo,Karume,Tandika nk mbona hawa hawatolewi au ndo wapo maeneo stahiki!Hujitambui yaani upo upo like your chairman mr dhaifu.

Umeuona mtaa wa kongo peke yake mkuu, mbona mitaa karibu yote ya K/koo ipo busy tu hata kama kuna maduka lakini yamekiuka utaratibu kwa kupanga mpaka sehemu ya wapita kwa miguu
 
Hivi tanzania sio vinara wa kuagiza na kutumia mabomu ya machozi kwa nchi za africa mashariki?
 
Wamachinga wanaondelewa je?
1. Je mazingira hayo wanayoambiwa waende yameandaliwa kibiashara?
2. Kama hayakuandaliwa vizuri, lengo ni kuwatoa tu mjini stand?
3. Na je mtawapiga mabomu na wateja waende huko?
4. Na kama hapatakuwa na biashara, hatima ya hao na maisha yao nini? Kwa sababu na uhakika wana familia na wanasomesha, wanalipa kodi za nyumba na vitu vingine kwa biashara hiyo.
5.Hamuoni mnawakosesha watu ajiri?
6. Je wakikosa ajira, mnataka mpambane nao kama majambazi kama sasa hivi mna pambana wakati wanafanya kazi halali hata kama kwa mazingira yasiyo ruhusiwa?
USHAURI WANGU NI KUWA MSIKURUPUKE KABLA YA KUTATHMINI KIPI KIKUBWA KATI YA FAIDA NA HASARA YA JAMBO.
 
Sometimes CHADEMA wanaipeleka nchi hii jehanam.
Haiwezekani ukatetea watu kufanya biashara bila kufuata utaratibu,eti kisa unataka kura zao.
Ina maana,CHADEMA ikiingia madarakani,itaendesha vipi serikali?

Itaendesha nchi kwa kufuata utaratibu na kuwasikiliza wananchi wake na haitakuwa serikali ya kuendeshwa kwa remote. Suala wa machinga lina wigo mpana. Inawezekana wewe unaebwatuka unafanya kazi na unapata ujira wako mwisho wa mwezi hili hali mwenzako anategemea kutembeza bidhaa ndio apate riziki. Wateja wa machinga wako mijini maeneo ambapo wako watu wengi wenye mahitaji ya bidhaa zao. Haiwezekani umwambie aende akatembeze bidhaa zake makaburini ambako hata upige mbiu maiti hazita stuka. Suala hapo ni jinsi gani wafanye hz biashara zao maeneo ya mjini. Sasa hiyo ni kazi ya Manispaa. Njoo Moshi uone machinga wanafanya biashara zao mbele ya kituo kikuu cha Polisi (Central Police) na wala hakuna tatizo. Kikubwa ni kwamba wanadumisha usafi eneo wanalofanyia shughuli na kwa kawaida wanaanza kupanga bidhaa zao mida ya mchana. Tatizo hapo ni kukomoana kisa aliyesema warudi sio wa CCM na kwa kuwa jeshi la Polisi linatumika kama Toilet Paper ndio maana wanakurupuka kuyafanya hayo. Hapa Moshi mama Kinabo alijaribu kupambana na machinga wa hapa wakamwambia kama anataka aendelee kuona siku zake kama binti wa form two aendelee. Na jeshi la Polisi hapa lilikataa kutii amri yake kwa kuwa Manispaa haikuwa imewaandalia miundombinu na mahali pa kufanyia kazi. Ilibidi anyweee na Machinga wanaiga shughuli zao kituo kikubwa cha mabasi na mbele ya kituo kikuu cha Polisi. Labda kama mwenzangu wewe uko MBAMBABAY makwapani mwa Tanzania. Njoo Ms ujionee ustaarabu.
 
Sheria ndio inayoongoza nchi,kama sheria inasema wamachinga wasifanye biashara hiyo sehemu lakini wao wakaendelea kufanya biashara hiyo sehemu hilo ni kosa,kama mbunge amaenda kuwaunga mkono wamachinga na yeye mkosa
 
This is the result of an illegitimate government.
 
Iringa. Mji wa Iringa uligeuka kuwa uwanja wa vita kati ya polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wafanyabiashara jana asubuhi. Watu 50 walikamatwa kutokana na tukio hilo akiwamo Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Katika vurugu hizo, gari la zimamoto lilivunjwa kioo na gari lingine dogo liliharibiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema Mchungaji Msigwa alikamatwa saa saba mchana kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo na kwamba watu wapatao 50 walikuwa wamekamatwa katika fujo hizo zilizochukua karibu saa tatu.
“Mchungaji Msigwa amekamatwa kwa makosa ya uchochezi, kufanya maandamano bila kibali na kuhamasisha watu kufanya biashara kwenye eneo ambalo limekatazwa kisheria.
Tumemkamata na hatutamwachia hadi uchunguzi wa suala hili utakapokamilika. Pia na hao watu wengine,” alisema Kamanda Kamhanda.
Alisema waliamua kufanya doria katika eneo hilo baada ya kupata taarifa za kiitelijensia kuwa wafanyabiashara walikuwa na mpango wa kuwashambulia mgambo wa Iringa kama wangekwenda kuwazuia.
Vurugu hizo zilichangiwa na mvutano uliokuwa unafukuta kwa muda mrefu kati ya Uongozi wa Manispaa na Mbunge huyo kuhusu amri ya kuzuia watu kufanya biashara kwenye Barabara ya Mashine Tatu, Iringa.
Uongozi wa Manispaa ya Iringa ulitoa tangazo Aprili 28, mwaka huu ukipiga marufuku kufanya biashara katika eneo hilo jambo ambalo lilipingwa na Mchungaji Msigwa na wafanyabiashara hao.
Alfajiri
FFU walianza kuimarisha ulinzi katika Barabara ya Mashine Tatu tangu alfajiri jana na wafanyabiashara hao walipofika kwenye eneo hilo walikuta limezingirwa na polisi.
Kusambaa kwa taarifa hizo kulimfikia Mchungaji Msigwa ambaye alifika hapo saa mbili asubuhi na kuanza kuzungumza na wafanyabiashara hao.
Watu walipomwona ndipo wakamzunguka na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu na kumshangilia: “Rais wetu... Rais wetu... Rais wetu.”
Maofisa wa Polisi walimfuata Mchungaji Msigwa na kumwomba aondoke lakini aligoma akidai ni mwakilishi halali wa wananchi kwa hiyo hawezi kuondoka.
Badala yake alipanda kwenye gari lake na kuanza kuzunguka eneo hilo huku akifuatwa na umati wa watu. Polisi nao walikuwa wakimfuatilia kwa magari yao.
Baada ya idadi ya watu kuongezeka kwa wingi barabarani na kuanza kufanya kitu kama maandamano wakiwa nyuma ya gari ya Msigwa, polisi waliwataka kutawanyika lakini waligoma huku wakizidi kuimba nyimbo za kumsifia mbunge huyo.
Mabomu ya machozi
Ilipotimu saa tatu na nusu asubuhi, polisi walianza kutumia magari ya kumwaga maji ya kuwasha na kutumia mabomu ya machozi na kusababisha watu kukimbia ovyo, huku wengine wakikusanya mbao, matairi na mawe na kuwasha moto ili kuwazuia polisi wasiwafikie.
Moto huo ulisababisha nyumba moja kuwaka moto ndipo gari la zimamoto lilipokwenda kuzima lakini nalo likashambuliwa.
Msigwa kukamatwa
Mchungaji Msigwa alikamatwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Kabla ya kukamatwa, aliwaambia waandishi kuwa polisi walikuwa wanawaonea wafanyabiashara hao na kwamba manispaa haikuwa na mamlaka ya kisheria ya kuwazuia wafanyabiashara hao.
Mei 15 na 16, mwaka huu Msigwa alifanya mikutano ya hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa na Magorofani na kuwataka wafanyabiashara kutokuogopa kufanya shughuli zao kwenye eneo la Mashine Tatu.

CHANZO: Vurugu kubwa Iringa, Mchungaji Msigwa mbaroni - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Sawa mkuu,serikali iwasikilize wananchi na itatue tatizo lao.Huyu mbunge hawezi kwenda kinyume kabisa na matakwa ya wapiga kura wake
 
Hongera Msigwa kwa kupambana na majangili bila hivyo ukombozi hatuna.
 
Back
Top Bottom